Ushauri wangu kwa serikali kuhusu ada ya makazi (Property fee)

MKUNIRWA

Member
Jul 1, 2016
19
12
Natarajia kuwa kila mtanzania amesikia kuwa kila mwenye nyumba anatakiwa kulipa kodi ya jengo bila kujali kuwa hapo alipojenga hakuna huduma muhimu za kijamii zinazopatikana toka Serikalini kama vile barabara kuu na za mtaa, Maji, Umeme n.k kinachonishangaza mimi ni kuona kuwa Serikali inatoza kodi ovyo bila kuangalia mantiki. Mfano mimi nilipojenga sina maji na barabara ya mtaa tumechonga wenyewe pia sijui kama kibanda changu nimekijenga kwenye eneo la msikiti au kanisa au soko hivyo siku moja nitabomolewa sasa naishangaa serikali kukulupuka na kudai kodi bila kutafakali mambo yote haya.

USHAURI KWA SERIKALI YA MPENDWA WANGU JPM

1-Serikali ipime maeneo yote ya nchi hususani Dar es Salaam na kutoa ati za makazi
2-Serikali ijilizishe kwanza endapo watu walipojenga ni maeneo rasimi au la
3-Serikali ifikilie vyanzo vingine vya mapato kuliko kuwabana walalahoi kwenye vikodi
4-Serikali ione umuhimu wa kupitia upya mikataba ya madini ambapo nadhani ndipo itaweza kukusanya kodi ya kutosha( nashangaa serikali toka imeingia madalakani haijawai ongerea suala la madini sasa najiuliza huko kupo shwali? kama ni shwali basi tuelimishwe ni kwa kiwango gani

PONGEZI KWA SERIKALI YA JPM
Nampongeza JPM kwa kuwafichua mafisadi
 
Hizi ni vurugu mechi....

Mwenye nguvu mpige mnyonge

Sukari ilikuwa 2000 kawaida na inapatikana....wakapiga marufuku...ikaadimika...sasa ni 2500....Sijui na hiyo 500 ni kodi wameongeza? Mnyonge anaumia...huruma kwa wagonjwa hakuna?

Kodi kodi kodi tu....

Kutoa pesa benki au M pesa au Airtel Money au Tigo Pesa....Kamshahara kamepigwa PAYE kodi...bado kwenda kutoa unapigwa VAT bado ukienda kutumia bidhaa ni kodi

Kwenye utalii, VAT kwenye utalii ndo wameuwa business na employment zitapotea

Hundreds of cancellation recorded..... and

You kill Tourism and say you want rich tourists

Mbona matajiri wa Tanzania hawatembelei mbuga hizi?

Kuna mantiki gani kusema hutaki watalii, unataka matajiri....

Matajiri wangapi basi wameshatembelea Tanzania.......
 
Ukawa wataisoma namba bora walioko ccm hayo hayawahusu.
 
Heee, Watu wa CCM hawanunui sukari ya madukani...mnalewa yenu...

CCM mna mabenki yenu...

Maccm wanatumbuliwa....huwajui majina?
 
Ndiyo kwanza nasikia kuna property fees,nilikuwa najuwa kuna property Tax,au huelewi tofauti ya ada na kodi yaani fees na Tax.
 
Back
Top Bottom