Ushauri wangu kwa rais wa Tanzania

who


  • Total voters
    1
Jun 10, 2014
30
5
USHAURI WANGU KWA RAIS WA TANZANIA NAOMBA UUNDE BARAZA DOGO LA MAWAZIRI [MINI CABINET] NDANI YA BARAZA LA MAWAZIRI.

Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 18 kama Raia kama mtanzania inanipa uhuru na mamlaka ya kutoa mawazo yangu kwa kutumia ibara 18 naomba nitoe mchango wangu wa mawazo kwa Taifa langu na nchi yangu kwa ujumla. Naipenda nchi yangu nitaendelea kuipenda nchi yangu kwa moyo wote.

Pendekezo la kuanzishwa kwa Baraza dogo la mawaziri (mini cabinet) ndani ya Baraza la mawaziri una lengo la kuunganisha malengo na harakati za wizara hizi katika kuleta maendeleo ya haraka na kukua kwa uchumi unaoendana na kupungua kwa umaskini wa kipato. Ili kuhakikisha kuwa kunakuwepo na uendeshaji na usimamizi bora wa uchumi (Better Ecconomic Management) eneo la uratibu wa wizara na Taasisi mbalimbali za kiuchumi ni lazima liimarishwe.

Bado Tume ya mipango na wizara ya fedha, vyombo nyeti vya kuendesha uchumi hazijaweka utaratibu wa uratibu unaowezesha maingiliano (integration) na mashirikiano kiutendaji. Matokeo yake ni kila kitengo kufanya kazi pekee pekee na kukosa ni wapi MAAMUZI YA MWISHO yanafanyika. Linaweza kuonekana ni suala jipya katika muundo wa mabaraza ya mawaziri ya sasa duniani ni kweli lakini sisi tunaweza kufanya hivyo kwa sababu ya mahitaji.

Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa wakati wenzetu wanatembea sisi lazima tukimbie ili twendane nao. Tume ya mipango ni lazima ipewe nguvu juu ya wizara hizi (super ministry) kwa kupitia marekebisho ya sheria iliyoiunda ya mwaka 1989. Tume za mipango katika nchi nyingine zimepewa mamlaka makubwa ndani ya katiba zao.

Niamini kuwa unapokosea usimamizi na uendeshaji bora wa uchumi, utengemavu wa misingi mikuu ya uchumi mkubwa utakuwa dhaifu. Matumizi ya sera za kifedha na zile za kodi zitapata wakati mgumu kutatua na kuondoa vikwazo vya kimfumo (structural rigiditie) ambavyo sio tu vitapunguza kasi ya kukuza uchumi bali vilevile zitashindwa kuendana pamoja na mikakati ya kupunguza umaskini baina ya wananchi.

Hakuna atakaekataa kuwa swali kubwa linaloulizwa hivi sasa ni kama uchumi unakuwa mbona hali ya maisha bado ni ngumu? Mbona na moduli za uchumi mkuu kushuka kwa wananchi (trickle down theory) na ile ya kujenga usawa hivi sasa hazitaweza kupunguza matukio yetu kujenga uchumi na kuleta maendeleo.

Nadharia ya kwanza itaendelea kuendeleza ukuaji wa uchumi unaombatana na kupanuka kwa tofauti kubwa ya mapato kati ya matajiri na maskini ni ile ya pili inayoleta nchi (redistribution) badala ya kutoa kipaumbele kwenye masuala ya uzalishaji, na biashara na hivyo kutaka usawa bila ya kukua kwa uchumi, au usawa katika umaskini itaendelea kudumaza. uchumi wa nchi unaohitajika sasa ni ule utakoleta maendeleo ya kiuchumi na jamii wenye lengo la kukuza uchumi na upunguzaji wa umaskini kwa wakati mmoja.

Kwa muundo wa baraza la mawaziri la sasa mawaziri wa baraza dogo (mini cabinet) wanaweza kuwa wafuatao. Waziri mkuu ambaye atakuwa ndiye mwenyekiti wa baraza hilo dogo (mini cabinet) waziri wa fedha na uchumi, waziri wa uwezeshaji na uwekezaji, waziri wa kilimo chakula na ushirika, waziri wa viwanda na Biashara, waziri wa uchukuzi, waziri wa ujenzi, waziri wa maji, na umwagiliaji, waziri wa Ardhi nyumba maendeleo na makazi, waziri wa nishati na madini, waziri maendeleo ya mifugo na uvuvi, waziri wa Tamisemi, waziri wa habari vijana, utamaduni na michezo.

Ni kweli kwamba hizi wizara zinapaswa kukaa pamoja kimkakati kutokana na wizara hizi zote kutegemeana uwezeshaji ili kukuza uchumi wa nchi na kupunguaza umaskini kwa wananchi.

Mfano: wizara ya kilimo chakula na ushirika ili iwe na ufanisi wa haraka na maendeleo kwa wananchi waliowengi sambamba na kukuza uchumi wa wananchi wanojishughulisha na kilimo nchini. Inategemea zaidi; wizara ya fedha na uchumi -> wizara ya uwekezaji na uwezeshaji->wizara ya ujenzi-> wizara ya uchukuzi-> wizra ya maji na umwagiliaji-> wizara ya Tamisemi pamoja na wizara ya Habri vijana, utamaduni na michezo. Utaona ni namna gani wizara zote hizi zinategemena na ni muhimu kuwa pamoja katika kuandaa mipango yao ya kibajeti na utendaji wa kila siku. Kilimo kinategemea Wizara ya fedha na uchumi –wizara ya uwezeshaji na uwekezaji->wizara ya maji na umwagiliaji-> wizara ya viwanda na biashara-> wizara ya uchukuzi= wizara ya ujenzi=wizara ya Tamisemi=wizara ya Habari vijana utamaduni na michezo.

Utaona ni kiasi gani hizi wizara zote zinategemeana ili kufanikisha wizara moja mipango yake ni muhimu kwendana kuliko kila wizara kupanga mipango yake bila kujua kipi kianze na kipi kifuatie kulingana na uwezo wetu mdogo wa kifedha kwa gharama nafuu – maeneo ya kilimo katika Halmashauri. Pia vijana ushiriki wao bado ni mdogo sana ukulinganisha na idadi yao na changamoto ya ajira nchini.

Mapungufu yaliyojitokeza katika program ya kilimo kwanza: yafanyiwe kazi haraka

1. Kuharakisha kutenga Ardhi kwa ajili ya kilimo kila wilaya

2. Kuboresha mfumo wa masoko ya mazao ya kilimo na taarifa zake (commodities exchange) mfano nchi ya Ethiopia imenufaika na mfumo huo. (Ethiopia commodities exchange)

3. Kuboresha miundo (barabara) maeneo yote ya uzalishaji hasa kwenye maeneo yote yanoyozalisha chakula kingi ambacho kinategemewa na Taifa na soko la nje ya Aridhi.

4. Serikali iweke msisitizo wa uanzilishaji wa viwaanda vya usindikizaji wa mazao ya kilimo (Agoo-based processing industrie) ili kuyaongezea thamani mazao ya kilimo na Ajira kwa vijana pia ihamasishe watu binafsi kupitia sheria na program ya public private partneership (ppp)

5. Kulinda mazao yanayozalishwa ndani mfano mazao yanayotoa mafuta ya kula Tanzania inaagiza kutoka nje mafuta ya kula nchini takribani tani 300,000 kwa mwaka . Hii ni sawa na asilimia 55 (55%) ya mafuta yote tunayotumia . Kwa hiyo tunatumia fedha nyingi za kigeni kuingiza bidhaa hii wakati nchi hii tunalima mazao ya ALIZETI, PAMBA MAWESE, KARANGA n.k. Serikali itoze ushuru mkubwa mafuta yanayotoka nje ili mafuta yetu yashindane kwa bei na yanunuliwe na kuongeza Ajira.

6. Kuwa na sera thabitisha na ya uwazi kuhusu uuzaji wa mazao hasa ya chakula nje ya nchi. Ili kuepusha wakulima na wasibabaishwe na msimamo wa serikali, serikali iweke sera ya wazi inayoruhusu wakulima kuuza mazao yao nje ya nje. Hata hivyo serikali ijiandae mapema kununua mazao ya wakulima kwa bei ya soko ikiwa ni kuwezesha mtaji kwa hifadhi ya chakula ya Taifa (NFRA) ili wakala awe na fedha ya kutosha kununua mazao. na kinachobaki ndicho kitakuwa kwa ajiri ya kuuza nje ya nchi.

7. Kuanzisha vivutio vya sera na sheria ili kukuza uwekezaji kwenye kilimo, kama kupunguza corporate tax kwa makampuni yanayowekeza vijijini kuinua kilimo vijijini.

8. Serikali ilibuni na ikaweke sera na mkakati wa uwezeshaji inayolenga kundi la vijana nchini ili wavutiwe na shughuli za kilimo.

Pamoja na serikali kuleta program na mikakati mbalimbali inayolenga kuwawezesha wananchi wenye vipato vya chini kama chini ya Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi kiuchumi lililoundwa kwa sheria Na.16 ya mwaka 2004 likiwa na dhamana ya kusimamia,kuratibu shughuri zote za uwezeshaji wote hapa nchini.

(1)mfuko wa wajasiriamari (2) Mifuko wa maendeleo ya vijana (3) Mifuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi (4) Mifuko wa uwezeshaji wa wajasiriamari wadogo.

Mfuko wa wanawake n.k bado kuna changamoto ya walengwa (targeting) il kuwasaidia wanaohusika. Fedha hizi zinapelekwa kwenye makundi/ watu wengi. Ni muhimu wenye vipato vy chini wahudumiwe na vyanzo mbalimbali vya mkopo.

Pamoja na kuwepo kwa mabenki mengi nchin bado wananchi wengi vijijini na mjini hawajafaidikia na huduma hii. Viwango vikubwa vya riba na mashrti magumu imefanya watanzania chini ya asilimia 13 ndiyo wamenufaika na hudumaza fedha . Hili ni changamoto kwa vijana ndiyo wanaanza maisha na hawana mitaji ya kutosha .

Ushauri wangu tukitumia mfuko wa maendeleo ya vijana na asilimia 5 (5%) kila Halmashauri tukatoa mikopo isiyokuwa na Riba ikasimamiwa na Baraza la vijana au ofisi ya vijana kila Halmashauri tutapunguza changamoto hizi. Wizara ya maendelea ya mifugo na uvuvi ili wananchi wanufaike ufugaji vizuri na wakuze kipato chao na kuinua uchumi wa jumla .

Wizara hii inategemea wizara ya fedha na uchumi-> wizara ya uwekezaji na uwezeshaji-> wizara viwanda na Biashara->wizara ya maji na umwagiliaji-> wizara ya Ardhi nyumba, maendeleo na makazi= wizara ya Habari vijana utamaduni na michezo. Wizara ya Habari, vijana utamaduni na michezo. Hii ni wizara yenye jukumu la kutoa kusambaza habari kwa wananchi zikiwemo habari za kitaifa, maelekezo na ushauri kutoka kwenye wizara zote kwenda kwa wananchi ili kuweka uhusiano wa serikali na wananchi katika shughuri zake pia wananchi wanufaike na tafiti pamoja wa ushauri wa wataalamu katika maisha na shughuri zao za uzalishaji.

Pia wizara hii ndio inayohusu vijana na kwa mujibu wa takwimu za sensa ya mwaka 2012 kuonesha idadi ya vijana na watoto kuwa na idadi kubwa katika nchi yetu. Wizara hii ni muhimu kushirikishwa katika Nyanja zote za mipango na utekelezaji wa wizara zote Kwa kuwa Serikali kupitia wizara ya habari vijana, utamaduni na michezo ipo kwenye maandalizi, mchakato, mbioni, mkakati wa kupeleka mswaada bungeni wa uanzishwaji wa baraza la Taifa la vijana.

Pamoja na swala hili kuchukua muda mrefu kwa serikali kupeleka mswaada bungeni wadau, vijana tumeanza kutilia shaka nia ya serikali kusaidia kuundwa kwa chombo hiki muhimu kwa mustakbari wa vijana wa nchi yangu. Kwa upande wa Zanzibari tayari serikali imeshapeleka muswaada bungeni na mchakato wao umefika mbali.

Wenzetu Afrika mashariki tayari wote wana vyombo hivi muhimu vya kusimamia na kuwaunganisha vijana katika kuyatumikia mataifa yao. Maazimio ya nchi wanachama wa Afrika ya mashariki ni kuwa ifikapo December 30 mwaka huu (30/12/2014) nchi wanachama ziwe zimekamilisha uundwaji wa mabaraza ya Taifa ya vijana na wanawake ili kutengeneza uongozi wao ndani ya jumuiya ya Afrika mashariki na kuelekea (SADC).

Hivyo chonde chonde serikali pelekeni mswaada bungeni ili chombo hiki kiundwe msije mkatukosesha fursa vijana wa nchi yetu ya kujumuika ya Afrika mashariki. Nchi nyingine duniani baada ya vita ya pili ya Dunia zilianzisha mabaraza ya Taifa ya vijana ili kuwaunganisha vijana pamoja na kuuwa na uwakilishi katika vyombo vya maamuzi mfano nchi za mwanzo kuunda mabaraza ya vijana: switzeland (1933) Sweden (1948) German (1949) I reland (1967) Belgium (1970) n.k Kuna vijana wenzetu wa kitanzania wamepata nafasi ya kuwakilisha nje ya nchi kuhudhuria mikutano ya vijana. Swali linakuja wanaporudi nchini wanarejeshaje mrejesho kwa vijana wote???

Inashindikana kwa sababu hakuna (proper forum) ya kuwakutanisha vijana kwa pamoja ili kuwaelimisha kile walicho kuja nacho. Juzi mkutano wa Dunia wa vijana kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya madola umemalizika siri lank. Uko wapi uwakilishi wa vijana wa Tanzania kwenye mikutano ya vijana nje ya nchi. Pili unapatikanaje tatu wakirudi majibu wanampa nani???.

Pia wakati huu tunasubiria uundwaji wa baraza la vijana la Taifa. Ni ushauri wangu kwamba kila Halmashauri ifungue idara ya vijana au ofisi ya vijana kila Halmashauri nchini kwa Ajiri ya kazi zifutazo:-

1. Kusimamia 5% ya mapato ya ndani ya Halmashauri inatengwa kwa Ajira ya vijana na wanawake maana hakuna msimamizi wa fehda hizi kama zina tengwa kila mwaka wa bajeti.

2. Kutoa elimu kwa vijana kuhusu mikopo hii namna ya kukopa, elimu ya ujasiliamali , na utaratibu wa urejeshaji mikopo hiyo na kutoa ushauri kwa halmashauri kupunguza kiwango cha Riba 10% katika mikopo hiyo ni kikwazo kwa vijana ni lazima kipunguzwe kiwe chini ya 5% ili vijana wasitumikie mikopo bali wazalishe na warudishe mikopo lakini na wao wabaki na salio.

3. Idara ya vijana kila Halmashauri zitaweza kupokea maelekezo na taarifa muhimu kutoka wizarani kwenda kwa vijana.

Pia fedha zinazotengwa wizara ya Habari, vijana utamaduni na michenzo itakuwa rahisi kuwafikia walengwa na wahitaji kuliko wizara yenyewe kushughulika na suala la kutoa mikopo. Kwa mfano: mwaka wa bajeti 2013/2104 wizara ya vijana ilitenga bilioni 6.1 kwa ajira ya mikopo kwa vijana .

Swali ni je vijana wangapi wanajua hilo? Je vijana wangapi wamepata mikopo hiyo wenye mahitaji? Vijana wa Bukoba ndani ndani kama nyakibimbili, Mtwara ndani ndani wanajua kama wizara ilitenga fedha billion 6.1 kwa ajiri ya mikopo na wakajua utaratibu wa kukopa .

Jibu sahihi ni hapana. Wizara ya kazi na Ajira nayo mwaka huu wa bajeti 2014/2015 imetenga karibu billion 4. Kwa utaratibu huu ni vijana wangapi na wanaostahili watanufaika na fedha hizi zinazotengwa na serikali. Bila shaka utakubaliana na ushauri wangu huu wa kidharura wakati tunaendelea na mchakato wa uundwaji wa baraza la vijana la Taifa. Kwa sababu Tatizo la Ajira hasa kwa vijana ni kubwa la siyo Tanzania pekee ni la nchi nyingi duniani, Mfano: nchi ya Nigeria inayoonekana kuongoza kwa wastani wa pato lake la ndani.

Pato la mtu mmoja mmoja nchini Nigerai ni dola za marekani 2688 wakati huwo Tatizo la jira ni 23.9% mwaka 2011 na Benki ya Dunia inaonesha imeongezeka hadi 38% Huku Africa kusini ambayo inaweza kuwa Taifa la pili kwa Takwimu hizo za wastani wa pato la ndani ya nchi. Pato la mtu mmoja mmoja Afrika kusini ni dola za marekani 7,336 kwa wakazi wake karibu milioni 48 huku ikikabiliwa na tatizo la Ajira karibu 24% huku Tanzania takwimu zikionesha tatizo la Ajira 12% nimeyasema haya ili nieleweke vizuri kuwa pamoja na kuongezeka kwa wastani wa pato la ndani ya nchi na kukua kwa uchumi kama shughuri za uzalishaji, hazitahusisha namba kubwa ya watu tatizo la Ajira na umaskini unaweza kubaki pale pale.

Ushauri wangu kwa vijana wenzangu bila kujal itikadi za kisiasa, dini n.k. jamii imetuamini kwamba tunaweza kuongoza, tunaweza kuwa wabunifu, na kutoa njia mbadala juu ya changamoto zinazoikabili jamii yetu.

Tunaomba tusiangushe jamii yetu na tusiwakatishe matumaini yao kwetu. Kwa sababu ujana sio cv bali ni matumaini ya jamii yetu kuwa ile kazi iliyopaswa kufanywa ndani ya wiki moja na mtu mzima kijana anaweza akaifanya au akaifanikisha ndani ya siku 3 hadi 4 tena kwa ufanisi pia jamii yetu inaamini kuwa vijana ni utoaji huduma na uongozi kwa ujumla.

Lakini mambo yanavyokwenda lazima vijana tujitazame upya kama heshima na matumaini tulivyopewa na jamii yetu tunitendea haki. Leo hii mfano vijana wameshika nafasi za, Wabunge, madiwani, meya , wakurugenzi wa Halmashauri , mawaziri, wakurugenzi wa makampuni binafsi meneja wa mabenki wakuu wa shule, vyuo, makatibu wakuu wa sekta binafsi na umma, mashirika, wakuu wa wilaya na Asasi za kiraia (NGO) N.K. Wizara ya Tamisemi kutokana na uamuzi kwa ughatuaji madaraka kutoka serikali kuu kwenda serikali za mitaa mipango mingi inatekelezwa kupita Halmashauri lakini kunaitaji ushirikiano wa moja kwa moja katika mipango ya maendeleo na sera mfano:

Wizara ya viwanda na Biashara ndio inahusika na Biashara ambapo kuna kundi kubwa la wamachinga wanaohitaji sera nzuri ili kuirasimisha sekta ya wamachinga kama chanzo cha mapato kwa serikali lakini maamuzi ya kuwapangia maeneo ya kufanyia biashara ni Halmashauri pamoja majukumu mengi yanayofanywa na Halmashauri yanayohusu wizara zingine tofauti na Tamisemi.

Wizara ya ujenzi hii inahusiana mkubwa pamoja na wizara zingine ili kurahisisha usafirishaji wa watu, mizingo n.k. lakini ni inahitaji kusaidiwa na wizara ya uchukuzi katika kusafirisha mizigo husafirishwa kwa njia ya reli, anga, majini.Katika nchi yetu karibu asilimia 96.3 ya mizigo inasafirishwa kwa njia ya barabara badala ya reli kitu ambacho kinapelekea muda mfupi barabara zetu kuharibika na pia kuwa gharama kubwa kusafirisha mizigo. wa kusafirsha mizingo mfano: uwezo wa Bandari yetu takribani inaingiza tani milioni 3 lakini uwezo wa Barabara yetu ni kusafirisha tani laki 2 tu na tani milioni 2-8 zinabaki.

Wizara ya fedha haiwezi kupanga mipapango ya Nchi kazi yake kubwa ni kukusanya mapato na kusimamia mfumo wa matumizi. Mpango unakuwa "determined' na uwezo wa kifedha.

Wizara kazi yake ni kutafuta fedha za kugharamia mipango wakati huohuo serikali inabidi ijiepushe na matumizi ya makubwa kwa kigezo cha ufanisi juu ya matumizi ya Bajeti ya serikali; wapi tunapata fedha na wapi tuna tumia. Mwisho kabla ya mwisho nimechukua nchi moja Barani Africa kama mfano.

Nigeria imekuwa taifa kubwa zaidi kiuchumi barani Africa kwa kuipiku Africa kusini, baada ya takwimu mpya za nchi hiyo kupandisha pato la jumla la ndani la Taifa hilo kufikia dola za kimarekani zaidi ya dola 500# Takwimu hizo zinaonyesha kuwa Nigeria imeipiku Africa kusini ambayo pato lake la jumla la ndani la dola za Marekani biioni 353 na ambayo ndiyo nchi pekee ya kiafrika mwanachama wa kundi la mataifa 20 yalioendelea kiuchumi G.20 Sekta zilizochangia pato la ndani ni mawasiliano, Habari na Technolojia, mafuta, muziki,Biashara za mtandaooni na filamu za Nollywood.

Takwimu hizi zikizingatiwa ukuaji wa sekta ya kilimo na utalii. Tanzania tunaweza kujifunza nini? Ili kukuza uchumi ni lazima kuwepo na juhudi za makusudi za kuendeleza,kuboresha mazingira ya kufanya Biashara na uwekezaji. Eneo hili bado lina changamoto (Investment Drive) haujawa wa kutosha.

Kutokuwa na uhakika wa mwelekeo wa sera ilio endelevu urasimu,ucheleweshaji wa utoaji wa maamuzi, kutoboreshwa ipasavyo kwa mazingira ya Biashara na uwekezaji katika kuboresha Barabara zetu,Reli,Bandari upatikanaji wa umeme wa uhakika, maji n.k ni maeneo yanayohitaji mwendelezo wa kasi wa kufanyiwa kazi.

Mahusiano yaliyoanzishwa kisheria baina ya sekta ya umma na sekta binafsi chini ya utaratibu wa (ppp) hauna budi kuimalishwa ili kusaidia serikali kupata mitaji ya kutosha katika yale maeneo au ile miradi inayohitaji fedha nyingi. Pia ni ukweli kuwa uchumi wa nchi hauwezi kuendelea bila ya kupata msaada wa huduma za sekta ya fedha.

Uchumi vilevile hauwezi kuendelea bila ya wananchi wengi kuingia katika Biashara. Utendaji wa sekta ya fedha nchini pamoja na masoko ya fedha ndio inayopelekea tija na ufanisi wa kuweka bei katika masoko yua msingi na yale mengine (priamary and secondary markets) Swala la kujiuliza ni kwa kiasi gani ukubwa wa sekta hii unakidhi matakwa ya maendeleo ya nchi yetu.

Tunahitaji kukua kwa asilimia 10 tukitegemea fiscal 1 sector, na nje sekta ya fedha inachangiaje katika hili, kwa maana ya uwekezaji nchini n.k. Ukuaji wa sekta fedha ni lazima usaidie ukuaji wa uchumi. Tunayo mabenki 45 ya kibiashara lakini uwekezaji bado ni mdogo. Utitiri wa Benki uliopo hauendani na mahitaji (demand) halisi ya huduma za kibenki katika uchumi.

Eneo hii linahitaji kuimarishwa. Mwisho ushauri wangu wa kuwa na baraza dogo (mini cabinet) una lengo la kujenga uchumi wetu unaoendana na kupungua kwa umaskini kuongezeka kwa kipato kwa wananchi maskini na kuharakisha maendeleo katika Taifa letu.

Ni mategemeo yangu kuwa Mheshimiwa Rais ushauri wangu utachukuliwa uzito uanostahili na kufanyiwa kazi.


Wako katika ujenzi wa Taifa Fahami Matsawily.

fahamijuma@yahoo.com +255 717262629
 

Attachments

  • kazi mpya hiyo.docx
    30.7 KB · Views: 122
Ushauri wako mzuri lakini kwanini hiyo mini cabinet isiwe ndo cabinet? mfano unganisha maji, ardhi, kilimo na mifugo halafu ukawa na makatibu wakuu wasaidizi kwa kila idara na katibu mkuu anaecordinate chini ya watangaza sera? ie waziri? Fahamu mawaziri sio watendaji kinachotakiwa ni coordination ya utendaji, na watendaji wakuu ni makatibu wakuu. Hebu fanya evaluation ya performance ya presidential delivery unit, hiyo naona ndo muelekeo mzuri. uwaziri ni upepo tu unavuma na kutoweka mda wowote, na ndo reliance ya mawaziri inavyotucost, mara megji, mara maige, kagasheki, nyalandu, yule mama nk. consistence utaipata wapi?
 
Ushauri wako mzuri lakini kwanini hiyo mini cabinet isiwe ndo cabinet? mfano unganisha maji, ardhi, kilimo na mifugo halafu ukawa na makatibu wakuu wasaidizi kwa kila idara na katibu mkuu anaecordinate chini ya watangaza sera? ie waziri? Fahamu mawaziri sio watendaji kinachotakiwa ni coordination ya utendaji, na watendaji wakuu ni makatibu wakuu. Hebu fanya evaluation ya performance ya presidential delivery unit, hiyo naona ndo muelekeo mzuri. uwaziri ni upepo tu unavuma na kutoweka mda wowote, na ndo reliance ya mawaziri inavyotucost, mara megji, mara maige, kagasheki, nyalandu, yule mama nk. consistence utaipata wapi?
uhauri wako ni mzuri sana makatibu wakuu ni watendaji hapa zaidi nimeshauri kuhusu sera na mipango katika wizara zinazotegemeana ktk uzarishaji
 
kesho ntakuwa star tv asubuhi kwenye kipindi cha tuongee asubuhi kuanzia saa moja na nusu hadi saa tatu mada bajeti 2014/2015 ntatumia muda mwingi kutoa ufafanuzi wa ushauri wangu kwa rais pia jioni ntakuwa itv mada watoto wa mitaani panya road au mbwa mwitu nini source na solution usiende mbali na tv upate ufafanuzi zaidi.
 
Back
Top Bottom