DALA
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 2,259
- 4,691
Heshima mbele wanajukwaa!
Sina sababu ya kutoa usuli mreefu kwenye hili maana kila mwenye macho anashuhudia kinachoendelea kwenye ulingo wa siasa. Natakiwa ku decleare interest though. Mimi ninaungamkono mabadiliko hivyo andiko langu linaegemea upande huo.
Tumeshuhudia matokeo ya tafiti za kura za maoni zikitolewa huku zikiashiria CCM kuongoza katika kinyang'anyiro hiki cha uraisi. Ukweli ni kwamba unaweza ukawa ni sahihi au usiwe sahihi inategemea nani amefanya utafiti na anamrengo gani hivyo ni swala la kujadiliwa kwa hoja.
Upande wa pili wa hili ni kuhoji utayari wa upinzani hususani UKAWA kujiwekea mikakati ya ku counter attack objectively na practically predictions. Ninavyoelewa ni kwamba umma unaandaliwa kisaikolojia ukiunganisha matukio mfano yule mzee aliyesema hawakotayari kuachia ikulu na haya matokeo. Mazingira yanaandaliwa ili bao la mkono litakapodumbukizwa watu warejelee matokeo haya ya tafiti hizi.
Ili kuwa realistic, nashauri UKAWA wasiangaike na kura za maoni ila waendeleze kampeni ya kiwango ambacho hakijawahi kutokea hapa nchini hilo la kwanza. La pili, nashauri UKAwA waandae timu ya mawakala/Walinzi wa kura kila kituo, Kata na Wilaya maana hapo ndo pana goli kwa wakati huu. Hawa mawakala wasiwe tu mawakala ikiwezekana watumie wanafunzi wa vyuo vikuu na wenye kujielewa, watu wenye hasira na umasikini, wenye uchu wa maendeleo ambao hawatanunuliwa vituoni.
Kusiwepo na wakala mmoja eti ndo analinda kura za UKAWA kila kituo kisa vyma vingine havijasimamisha mgombea kwa kuzingatia umoja wao.
Kwa njia hii tutashuhudia mtokeo ya utafiti halisi yakitolewa baada ya 25/10/2015 kwa upole ambao haujawahi kutokea.
Haya ni maoni yangu na siyo sheria.
Aluta continua