switishka
Asante kwa kujibu vyema binti kuna maelezo nilikuwa nataka niyapate kutoka kwako maana mazingira ambayo hutukutanisha na wapenzi wetu kwa kiasi fulani hueleza mwenendo wa mahusiano tuliyonayo...
Ukiachana na hilo nafikiri moyo wako umetokea kumpenda sana huyo mwanaume uliyenaye kutokana na mazingira mliyojijengea baina yenu kabla ya kuwa pamoja kama wapenzi...
Binti kuna jambo moja inabidi ujifunze kutoka kwetu wanaume, sisi wanaume tuna namna nyingi za kumtongoza mwanamke na katika njia zote njia pekee ya kuuchota moyo wa mwanamke ni kama hii aliyotumia huyu jamaa uliyenaye 'the office guy'...
Sasa mapenzi ni mkataba na sharti nambari moja la mkataba huu ni UAMINIFU baina ya wapendanao.
Mmojawapo anapofanya USALITI ni wazi kuwa kakiuka mkataba na pasipo kumung'unya maneno ni kwamba hakupendi tena.
Hebu jaribu kutafakari na kujiuliza maswali haya:
1. Mpenzi wako katumia muda gani kumtongoza huyo binti mwingine?
2. Wakati anamtongoza ulidhani alikiri kuwa ana mpenzi (ambaye ni wewe)?
3. Hata kama alitamka kuwa yupo kwa mahusiano, unadhani alikiri kuwa anakupenda sana kwa huyo binti?
4. Kama anakupenda kweli hivi hudhani kuwa dhamira ingemsuta na kuishia tu kwenye tongozo, lakini hakuishia hapo akaendelea hatua inayofuata ya kufanya mapenzi na binti huyo.
5. Je unadhani walifanya tu mapenzi siku moja na binti huyo akanasa mimba?
6. Kama anakupenda kweli ina maana alishindwa hata kutumia kinga ili asije akaukwaa ukimwi ambao mwisho wa siku angelikuambukiza wewe?
Binti lazima utambue kuwa mapenzi si utumwa wa nafsi, mwili wala roho.