Kazini kwangu watumishi wenzangu hawanipendi kutokana na mimi kupendwa sana na wanafunzi kutokana na kuwafundisha vizuri na somo langu kufanya vizuri kuliko masomo mengine na wanafunzi hao kuonyesha kunipenda zaidi mimi kuliko wenzangu, sasa wenzangu wananitenga nifanyaje?
Kuna zaidi ya hilo. Hakuna mfanyakazi atakayekuchukia kwa wewe kufaulisha watoto, kwa sababu wanapofaulu wewe huongezewi mshahara wala wao kupunguziwa. Angalia ukaribu wako na uongozi na nini unazungumza uwapo na uongozi au wanafunzi.