mwalimumzalendo1
JF-Expert Member
- May 19, 2014
- 1,098
- 407
Makubwa haya
Yakipatikani maji kimara yote mpaka mbezi,mwakani agombee tofauti na hapo atafute jimbo lingine.
Bpra mnyika arudi shule ubunge umemshinda
Bpra mnyika arudi shule ubunge umemshinda
Mnyika wana ubungo hawakukosea kukupa ubunge kamwe! Unawatendea mema wana ubungo, unawatendea mema watanzania!
Amefanya nini cha maana ktk jimbo lake tangu ameingia?
Mh. Mnyika,nilikufahamu tangu ulipogombea Ubunge wa Ubungo kwa mara ya kwanza mwaka 2005 dhidi ya Charles Keenja. Wakati huo nilikuwa mwanachuo wa mwaka wa kwanza UDSM nikichukua Sheria. Ingawa sikuwa mpigakura wako kwakuwa nilijiandikisha Kibaha,nilikuunga mkono. Ukiwa kijana na mwanafunzi mwenzetu UDSM,tulijivunia uwepo na ugombea wako.
Mh. Mnyika,mwaka 2010 nilihamisha kituo changu cha kupígia kura kwa ajili yako. Nikahamisha toka Kibaha hadi Ubungo. Nikakupigia kura Nkrumah Hall UDSM nikitambua uwezo,nia na sababu zako za kuwa Mbunge wa Ubungo. Safari hii nikiwa mwajiriwa wa UDSM. Ukamshinda Hawa Ng'umbi wa CCM na kuwa Mbunge.
Tangu kuwa Mbunge,hukuwahi kutuangusha kama vijana katika hoja na msimamo wa kitaifa. Umekuwa ukiongozwa na kauli zithibitikazo kwa nyaraka na tafiti mbalimbali. Hakika vijana wa Tanzania unatuwakilisha vyema na tunajivunia kukuchagua kuwa Mbunge wa Ubungo.
Nakushauri mambo mawili. Mosi,uanze upya au umalizie elimu ya juu yako. Tunahitaji ubongo wako ulioimarika zaidi kielimu. Elimu ya juu kwa nafasi na uwezo wako wa kiuongozi haiepukiki. Pili,endelea kuwatumikia wananchi wako wa Ubungo na Tanzania kwa ujumla kwa weledi,uwezo na bidii uliyojaaliwa. Asante
Hivi kwanini John Mnyika hana degree wakati amewahi kuwa mwanafunzi wa evening class udsm?
Una maana gani? Kufanya nini kama kipi?
Mnyika ni Mwakikishi bora kabisa wa wananchi ktk mkoa wote wa Dar es salaam.
Ktk Wabunge wote wa Dar, Wabunge vilaza kabisa ni wale wa CCM ukimweka kando Dk. Ndugulile wa Kigamboni, Wabunge kama Mtemvu wa Temeke, Mahanga wa Segerea, Mwaiposa wa Ukonga, Zungu wa Ilala na Idd Azan wa Kinondoni.
Vv
Watu huwa wanaongeza maarifa pale wanapoona kuwa kuna mahitaji,kuna wafanyabiashara wengi wamemaliza secondary tu wakawa succsefull kwa yale wanayofanya hivyo kuona hakuna haja ya maarifa mengine kuna nchi ambazo huwa wanakuwa awarded degrees sababu wamedemonstrate practical entrepreneurship bila shule,kwetu hapa kuna maprofesa wa dev.studies na entrepreneurship hata banda la kuku hawana,to me unamaliza undergraduate ukiona imeshindwa kukusaidia kufikia malengo yako, u opt for masters, uona bado unaendelea and so on,
Amelifanyia nini jimbo lake?
Kwa tunaoishi kimara tunajua angalau mabomba ya wachina cku iz yana mgao kidogo wa maji. Lakn ukiacha hilo kama govt hitoi hela ya maendeleo unataka atoe hela yake mfukoni we ----? ubungo upinzan hata waweke jiwe litachaguliwa jiwe habar ndo hiyo,utaki kula wembe ufe.
Kwahiyo aliacha kusoma baada ya kuona degree haitamsaidia kitu... au baada ya kuona kwamba haitaji degree ili kufanya shughuli zake? Don't get me wrong, mimi binafsi namkubali sana John Mnyika kwa utendaji wake. Tena yeye ni mfano mkubwa sana wa kuigwa na kuonyesha kwamba mtu haitaji kuwa na degree ili kuwa mwanasiasa mzuri. Swali langu tuu nilitaka kujua kama aliacha kusoma, alifukuzwa, au alikuwa "discontinued".