Ushauri wa TRA na wizara ya Fedha, fikirieni kama watu wasomi kwenye kodi ya magari

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Ukifikiria mambo mengine yanayotendeka nchi hii unajiuliza kama wafanya maamuzi hua wanafikiri vizuri kweli?

Katika taasisi zinazochangia kuharibu mazingira na kusababisha magonjwa ya mapafu ni wizara ya fedha na TRA.

TRA na wizara yake wanahamasisha watanzania kununua magari ya zamani machakavu ambayo nchi wanazojali mazingira yao na usalama wa afya za watu wao walishayapiga marufuku kutembea barabarani, hayo ndio TRA inataka Watanzania waagize kwa sababu ndio yana kodi nafuu. Ni ajabu nchi kama Zimbabwe imepiga marufuku gari za zaidi ya miaka 5 kuingia nchini mwao ila Tanzania unaweza kuagiza hata gari la mwaka 1988 na bado ukadunda nalo barabarani kama kawaida.

TRA wanachoangalia wao ni kodi na sio uchafuzi wa mazingira, ukiagiza gari ya mwaka 2017 kodi yake unaweza kulia, ni bei ya hizo gari 2. Badala wapige kodi kubwa magari ya zamani ili kuzuia uchafunzi wa mazingira na afya za Watanzania wao wanahamasisha watu kuagiza mikweche iliyopigwa marufuku huko Japan kwa sababu ndio wamaipunguzia kodi.

TRA punguzeni kodi kwenye magari mapya, msiangalie kodi pekee, jalini na afya za watanzania. Mnataka kodi gani wakati mnaotaka kuwapelekea maendeleo watakua wanajifia kwa magonjwa ya mapafu kwa sababu ya mikweche mnayotaka waagize.

Jambo lingine, punguzeni kodi ya kuagiza magari mapya, watu wataagiza magari mwengi na mzunguko wa matumizi ya ndani utakua mkubwa, vipuli, mafuta, matengenezo, vilainishi nk hivyo mtakusanya kodi zaidi kuliko ilivyo sasa mnangoja mtu aagize gari mumkamue kwenye kodi, wanaagiza wachache ila kodi ikiwa kidogo wataagiza wengi na matumizi yatakua makubwa, mtapata kodi nyingi.

TRA fikirieni kama watu mlioenda shule.
 
Back
Top Bottom