Ushauri wa kibiashara,mtaji wa tsh. Million 30

Bobo

Member
Aug 20, 2011
54
95
Habari zenu wana JF..
Leo nimerudi tena baada ya kupotea kwa muda mrefu nikiwa katika gurudumu la mchakato wa elimu. Nami natoa shukrani zangu za pekee kwa mwenyezi mungu kwa kuniwezesha kumaliza elimu yangu ya juu. Mdogo wenu nimekuja kupata ushauri ili kuweza kujikomboa katika umaskini unaoendelea katika bara za nchi za afrika. kama mnavyojua nchi yetu ta TZ kwa sasa imekumbwa na dhiki ya ajira kwa vijana kwa muda mrefu, mbali na ivo nimethubutu kabisa kukataa kuajiriwa na kutaka kuanzisha biashara ambayo hapo baadaye inaweza ikawa chachu ya ajira kwa vijana wenzangu.
Nimeweza kupata mkopo usio na riba wa TSH MILLION 30 kutoka kwa kaka yangu kwa ajili ya kuanzisha biashara nitakayoidumu, Ivyo basi nimekuja kwenu GREAT THINKERS kuomba ushauri juu ya biashara gani inafaa kwa sasa ukitegemea na mtaji husika.
Ushauri wenu ni muhimu sana.
Ahsanten.

MWEZI MMOJA BAADA YA USHAURI WA JF..!!
Nashukuru sana wana JF kwa mawazo yenu mlionipatia kipindi cha miezi ya nyuma,nami niliyachukua na kuyaweza kuyafanyia kazi kwa kufanya tafiti mbalimbali,kusema ukweli nimegundua mengi sana kwenye ulimwengu wa biashara.,nimejaribu kusafiri sehemu mbalimbali zisizozidi kumi kwa ajili kufanya uchunguzi,vilevile nimejaribu kukutana na watu mbalimbali waliopo kwenye huo ulimwengu wa biashara na kugundua faida na changamoto za biashara.,hata ivo sikuwa nyuma katika usomaji wa vitabu na vijarida mbalimbali kupitia internet na kwa bahati nzuri hizi huduma kwa sasa zinapatikana kwa ukaribu zaidi.

Ukweli ni kwamba biashara ni zaidi ya kile unachofikiria kichwani, ni zaidi ya kukaa nyumbani na kuamka kesho yake asubuhi na kufanya biashara,biashara inahitaji tafiti mbalimbali ili kuifanya biashara yako iwe bora na iwe tofauti na biashara nyingine.
Nashukuru sana,tayari nimefanya maamuzi ya biashara na tayari mwezi huu wa 11 tunaanza kuifanyia kazi,wengi watajiuliza ni biashara gani.!!,nami nahitaji kuwatoa hofu ya kwamba ni biashara ambayo kila mtanzania anaiweza kuifanya haijalishi una kipato kidogo ama kikubwa cha zaidi ni kufanya maamuzi. Sijatofautiana sana na wenzangu katika hiyo biashara nilichokifanya hapo wataalam wanasena n ku "add Value". natumaini nitarudisha mrejesho juu ya maendeleo ya biashara.
Ndg. vijana wenzangu acheni kulala nyumbani,sumbua kichwa na naamini hakuna kinachoshindikana. ni hayo tu kwa leo.!!! Nitarejea tena...
 
GEORGEMAS

Member
Jul 12, 2012
5
0
kwa huo mtaji unaweza kuuza nafaka mf mchele kutoka mbeya ukauza dar inalipa,au fungua pharmacy inalipa.
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,007
2,000
Tafuta vijana wenzako mchange mpate mil. 100. Then anzisheni biashara ya mafuta ya taa kwa lengo la kuikuza ili mfungue kituo cha mafuta in the future.
 
chash

JF-Expert Member
Jun 5, 2012
550
250
Umesomea nini mkuu? Mara nyingi knowledge ulionayo na profession uliyo somea ni foundation kamili ya biashara inayokufaa. Learning curve inakuwa fupi na losses associated na hiyo learning curve zinapungua.
 
C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
5,026
2,000
Uko wapi?? Kama uko mjini tafuta sehemu yenye ofisi nyingi then fungua stationary..target kuwauzia watu wa maofisini kwa jumla na reja reja anza kujipendekeza kwa watu wa ofisini kama wewe ni mwanamke itakuwa rahisi kwako kupata connection
 
Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
17,923
2,000
Uko wapi?? Kama uko mjini tafuta sehemu yenye ofisi nyingi then fungua stationary..target kuwauzia watu wa maofisini kwa jumla na reja reja anza kujipendekeza kwa watu wa ofisini kama wewe ni mwanamke itakuwa rahisi kwako kupata connection
ha ha ha ha ha ha! C.T.U, sijui ulikuwa una maanisha nini hapo kwenye bold!
 
Last edited by a moderator:

Bobo

Member
Aug 20, 2011
54
95
Shkuran sna mkuu C.T.U...ni mawazo mazuri na mimi bila shaka nnayafanyia kazi kwa kufanya ka research kadogo kabla cjaingia kwenye bussiness...
 
BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
4,060
2,000
....Nikopeshe shilingi Milioni Moja na baada ya Mwezi ninakurudishia Milioni Moja na Laki Tatu. ukifanya hivyo kwa watu wa Nne tu unakuwa kila mwezi una Shilingi Milioni Moja na Laki Mbili ya Matumizi yako bila Kugusa Mtaji Wako Wakati Ukiendelea Kutafakari cha Kufanya. NiPm kama Upo tayari.
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,397
2,000
Jaribu u agent wa mpesa,tigopesa, airtel money etc! Naamnini haihitaji mtaji mkubwa sana kuanzisha na hivyo itakufanya uwe na pesa ya kutosha kuzungusha! Say utatumia kama 5m kwa ajili ya miundo mbinu (hasa kukodi au kupata sehemu ya kufanyia biashara) na kubakiwa na 20m kwa ajili ya kuizungusha na 5m inabaki kama ya dharura.
 
truckdriver

JF-Expert Member
May 7, 2012
542
250
Kuna soko kubwa la mashudu ya alizeti na pamba huko Kenya. Kuna wakenya wanakuja kila siku Singida, Tabora, na Shinyanga kutafuta mashudu wao wenyewe sasa kama unaweza kupeleka hata mpaka Namanga wawe wananunua kwako. Fanya utafiti uone kama itakufaa hii biashara.

Nina lori (semi linaweza beba hadi tani 30) kama utahitaji usafiri au kushirikiana kama utachagua biashara yeyote itakayohitaji usafirishaji.

Kila la kheri
 
Bobo

Member
Aug 20, 2011
54
95
....Nikopeshe shilingi Milioni Moja na baada ya Mwezi ninakurudishia Milioni Moja na Laki Tatu. ukifanya hivyo kwa watu wa Nne tu unakuwa kila mwezi una Shilingi Milioni Moja na Laki Mbili ya Matumizi yako bila Kugusa Mtaji Wako Wakati Ukiendelea Kutafakari cha Kufanya. NiPm kama Upo tayari.

Mkuu.,kwa hilo sitaliweza. nitakuwa nacheza kamari. Nashukuru sana kwa huo ushauri
 
Bobo

Member
Aug 20, 2011
54
95
Jaribu u agent wa mpesa,tigopesa, airtel money etc! Naamnini haihitaji mtaji mkubwa sana kuanzisha na hivyo itakufanya uwe na pesa ya kutosha kuzungusha! Say utatumia kama 5m kwa ajili ya miundo mbinu (hasa kukodi au kupata sehemu ya kufanyia biashara) na kubakiwa na 20m kwa ajili ya kuizungusha na 5m inabaki kama ya dharura.

mkuu nitalifanyia kazi huo ushauri..nashukuru sana
 
Bobo

Member
Aug 20, 2011
54
95
Kuna soko kubwa la mashudu ya alizeti na pamba huko Kenya. Kuna wakenya wanakuja kila siku Singida, Tabora, na Shinyanga kutafuta mashudu wao wenyewe sasa kama unaweza kupeleka hata mpaka Namanga wawe wananunua kwako. Fanya utafiti uone kama itakufaa hii biashara.

Nina lori (semi linaweza beba hadi tani 30) kama utahitaji usafiri au kushirikiana kama utachagua biashara yeyote itakayohitaji usafirishaji.

Kila la kheri

Naomba nlifanyie utafiti hlo ikiwezekana unpe information zaidi kadri ya uelewa wako ktk hiyo biashara..
 
Buza

Member
Aug 7, 2011
57
95
Huyo kaka yako ana matatizo, anawezaje kukupa au kukukopesha hela ya mtaji wa biashara isiyojulika. Labda hizo hela ni chafu.
 
CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
7,048
2,000
Wa Tanzania Bana, Utatujua tu,

Kwa kifupi ni kwamba Wewe Mleta mada Ulikuwa na Makosa, Uliwezaje kwenda Kukopa kabla ya Kujua unacho enda kukifanya? Au unachora watu Humu?

Mkuu kama Uko Dar wewe Tafuta watalamu wa Maswala ya Biashara wakushauli ni nini cha Kufanya na hizo pesa, Ila cha Muhimu ni Bora ukaenda na ,Mawazo yako kama matatu wakusaidie kuchambua ili ibakie Moja, Na ni bora ukae chini utengeneze wazo lako mwenyewe kulingana na mazingira ya sehemu ulipo,

Na ni lazima liwe wazo la Biashara Endelevu ya Miaka na miaka na si Biashara za Musimu mara leo Unanunua Mahindi, mara kesho uko kwenye Mafuta, kesho kutwa kwenye Nguo, So kaaa chini wewe mwenyewe na Umiza kichwa na utapata wazo Bora kabisa, NA WAZO BORA LA BIASHARA NI UNALO ANZISHA WEWE MWENYEWE
 
Mwanahisa

JF-Expert Member
Jun 29, 2012
1,388
1,195
Mkuu hongera kwa uamuzi wa kimapinduzi,
kiu uliyo nayo ya kujikwamua hata maji ya bahari hayatoshi,
Mkuu 30mil, ukiulizia ni biashara gani itakufaa, ni sawa na kuvaa suti yako mpya ukajipulizia manukato alafu ndio uende bafuni kukoga, mrudishie bro hela yake ili undugu wenu usiingie doa, alafu rudi kwenye nafsi yako ujihakiki kitaalam inaitwa monologue, kwani ulicho nacho kichwani ni zaidi ya million 30 ya bro. Nikutakie kila la kheri mdogo wangu.
 
Micha

JF-Expert Member
Sep 12, 2011
269
250
Wa Tanzania Bana, Utatujua tu,

Kwa kifupi ni kwamba Wewe Mleta mada Ulikuwa na Makosa, Uliwezaje kwenda Kukopa kabla ya Kujua unacho enda kukifanya? Au unachora watu Humu?

Mkuu kama Uko Dar wewe Tafuta watalamu wa Maswala ya Biashara wakushauli ni nini cha Kufanya na hizo pesa, Ila cha Muhimu ni Bora ukaenda na ,Mawazo yako kama matatu wakusaidie kuchambua ili ibakie Moja, Na ni bora ukae chini utengeneze wazo lako mwenyewe kulingana na mazingira ya sehemu ulipo,

Na ni lazima liwe wazo la Biashara Endelevu ya Miaka na miaka na si Biashara za Musimu mara leo Unanunua Mahindi, mara kesho uko kwenye Mafuta, kesho kutwa kwenye Nguo, So kaaa chini wewe mwenyewe na Umiza kichwa na utapata wazo Bora kabisa, NA WAZO BORA LA BIASHARA NI UNALO ANZISHA WEWE MWENYEWE

Mkuu mlata mada hajakosea kitu ila nafikiri hujamwelewa vizuri. Amemaliza kusoma na bro ameahidi kumpa 30m afanye biashara, kwahiyo kijana amekimbilia JF kuomba msaada. Kama una mawazao mazuri ya biashara mshauri, huwezi jua kesho anaweza kuwa mwajiri mzuri akaajiri na wadogo zako, wewe si unaona ajira zilivyo ngumu ziku hizi? Tunatakiwa tupeane support na siyo kukatishana tamaa na hasa kwa wajasiriamali.
Bobo kuna thread nyingi humu ndani ambazo zilikuwa na mawzo mazuri ya ujasiriamali, nakushauri search uzipitia zitakusaidia.
 
Nashukuru ndg Micha...nadhani umenielewa vizuri na kwa ufasaha kabisa...hiyo pesa ipo tayari ila sitaweza kuichukua na kuidumbukiza katika biashara isiyoeleweka. ndo mana nikaja JF kuomba ushauri nikitumaini kuwa wazo la biashara ni la muhimu kuliko kitu chochote kile katika biashara. Nashukuru kwa ushauri
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom