Ushauri wa haraka unahitajika kwa Huyu Dada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa haraka unahitajika kwa Huyu Dada

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jibaba Bonge, Oct 15, 2010.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hii imetokea Dar. Dada mmoja amekuwa akiuguliwa na mume wake ugonjwa ambao ilibidi afanyiwe operation (medium). Pamoja na kwamba operation ilikuwa successful mume aligundulika kuwa ana ngoma (HIV+), ilibidi na huyo mdada ashauriwa na madaktari kupima, akakutwa negative.

  Amemuendea spouse wangu kumuomba ushauri, kwamba aendelee na hiyo ndoa au aivunge. kama akiendelea nayo maana yake mahusiano ya mke na mume yataendela na kama hatakubali hayo mahusiano then ndoa iko mashakani. Spouse wangu ameshindwa kumshauri na mimi pia nimeshindwa.

  Wana JF tusaidieni mawazo namna ya kumshauri huyu dada,
   
 2. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Akimuacha atakuwa amemnyanyapaa...

  Avunje Ukimya... akae waongee wapange maisha upya
   
 3. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  amesahau kile kiapo alichoapa kwenye ndoa?????kuwa katika shida na raha,ugonjwa n.k. bado mume na mke wataendelea kuambatana pamoja katika ndoa yao!
   
 4. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Dah...! Hadi JIBABA ameshindwa kutoa ushauri....!
  Aidha, mimi ningemshuri asivunje ndoa yake, bali akae chini na mmewe wajadili ripoti hiyo ya madaktari, na namna ya kuendelea na maisha. Hii ni iwapo tayari wameshazaa, na wana watoto sasa. La msingi ni kuwa makini sana na muangalifu sana katika mahusiano yao.
  Achunguze kama jamaa alipata kujua kuwa ameadhirika kabla, na iwapo alijua, lakini hakuwa wazi, basi ni vema akavunja hiyo ndoa bila huruma, lakini kama aliwahi kuwa muwazi kwa upositive wake, au hakuwahi kujua kama ameadhirika, then the above advice may apply...!
  Kama hawana watoto, then ni vizuri akaangalia maisha yake kwa utangulizi zaidi, japo mawazo ya jamaa nayo yapewe nafasi....!
  Aidha, pole zimfikie na amkaribishe Mungu katika maisha yake yote...!
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  kaka yangu ameishi na ngoma since 1995 na ameoa ana watoto watano na mwingine amempata last month. shemeji yangu (mke wa kaka) hana ngoma na walioana kitambo na wanashirikiana vyema kabisa kingono. na huwa anapima mara kwa mara na hajawahi kuupata. kuna ushauri mzuri anaupata kwa waelimishaji ambao umesaidia ndoa yao ikadumu. Ukimwona brother hana dalili kabisa kwamba anaishi na ngoma.

  Mshauri huyo mke wa jamaa aache kufuata ushauri mtaani, aende kwenye vituo vya ushauri nashaha akapate dozi namna ya kuishi na mwenza muathirika. Kama alisema watakuwa pamoja ktk raha na shida, ugonjwa na uzima basi hili ndo jaribu analopaswa kulishinda
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  nimekurekebisha kiswahili chako hapo juu
   
 7. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  ..asivunje ndoa bt asishirikiane nae tendo la ndoa
  asimkimbie amuuguze kwa upendo ...amwombe mungu sana ampe busara na hekima ili aweze kuhendo i stuation..bt pls asisepe ..aikubali hali na hamkubali mme wake ktk hali iyo (cz apo ni neema ya mungu tu imepta ya mme wake aumwe ili hali hali halisi ijulikane asngejua angeukwaa pia so kwa kuimrudishia mungu shukrani ASIVUNJE NDOA...dah i can fl t....
  ASIVUNJE NDOA.AMSAMEHE NA KUMPENDA+KUMVUMULIA MUMEWE KTK HALI HII.
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Jamani kale kemchezo kanaweza fanywa hata kwa mpira, I know a lot of them wa jinsi hiyo wanaishi vizuri, nawajua kwani nimefanya nao kazi and i have been part of thier life. Yapo mengine yanayotuunganisha sio lazima iwe pale tu.... lakini pia kuna uwezekano mkubwa wa mambo mawili kutokea
  1. Je, mwanamme amerudia vipimo mara ngapi au ilikuwa hiyo mara moja tu; hii ni kwasababu kuna baadhi ya nyakati hasa hapa kwetu vile vipimo havitunzwi katika mazingira yanayotakikan na ndio maana kumekuwa na case nyingi za mtu kukutwa positive leo na keshi kakutwa negative.

  2. labda huyo mwenzio yupo katika kipindi kinachoitwa, "window period" kwa kifupi ni kwamba inawezekana na yeye ni positive only that wale Virus hawajajidhihirisha bado.

  Mungu atuokoe na kutuponya. AMEN
   
 9. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,494
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  wasiachane kwanza ngoma yenyewe dawa imeshapatikana na production ya vidonge inaendelea kwa kasi ya ajabu siku wakiitangaza tu na supply ya vidonge inaanza hapo hapo kwa hiyo UKIMWI utakuwa kama kikohozi tu. Unaweza kumwacha huyo ukaolewa ukakutana na UKIMWI mwingine huko ulipoenda. Cha muhimu ni kuwaona wataalamu watawaelekeza jinsi ya kuishi na kufanya mapenzi bila kuambukizana na dawa ikitoka mwanzoni mwa mwaka kesho jamaa anapona jumla
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Kama ame-prove beyond reasonable doubts kwamba yupo negative, namshauri AVUNJE ndoa: Ninaamini wakiendelee kukaa pamoja lazima atakuwa infected : Kumbuka kuwa asilimia zaidi ya 80 ya wanawake waliokuwa kwenye NDOA ufanya tendo la ndoa bila ridhaa yao (in most of the time)
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Dah this is too sad
   
 12. C

  Chamkoroma Senior Member

  #12
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wote mliochangia mjadala huu nawashukuru sn kwani ktk watu waliofikwa na jambo hili mimi ni mmoja wao, nilikuwa safari ktk nchi fulani kwa muda. nikasikia mama anaumwa nikarudi akaniambia anaumwa na amepima kaona anao, nikaenda nae Amana nikapima nikaonekana nega, nikamuahidi mama kuwa sitomuacha hata iweje kwani hayo huwapata wote, sikupenda mlaum kuwa ameupata wapi japo alisema ni sindani yeye ni nesi,
  kifo sikia kwa jirani utamonsol, lkn kwako ni shida sn inauma sn,
  ninachoweza sema juu ya hili mama ajipe moyo mkuu na achukuwe tahadhri katk kila ngono au mwanzo wake asijeambukizwa, kuhusu kaka wa jamaa aliyesema kaka yake anao na wanapata watoto, sibishi lkn ingekuwa yeye mkeo anao yeye hana angekubali wazae watoto?
  Jamani mdundo wa ngoma kubwa ni mzuri lkn chunga usipoteze maisha hasa ukijua waliobaki wanao wanakusubiri wewe badala ya mkeo/mume.
  good day o all.
   
 13. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  asivunje ndoa,
  hii ndo nafasi yake ya kuonyesha upendo wa kweli kwa mumewe.
  mumewe anahitaji suport yake.hilo ni jaribu lake, waungane kwa maombi watashinda pamoja.
  pia itabidi wafundishwe jinsi ya kushiriki tendo la ndoa bila ya mke kuambukizwa.
  ,,,sijui mume kaupatia kwenye haya mainfidelity mnayoyafagilia kila siku??!anyway,nawaza tu.lkn mke asiondoka haijalishi kaupataje.
  inasikitisha.
   
 14. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Ushauri mwingi uliotoka ni kumtumbukiza mama wa watu shimoni.Kama kweli imethibitika kwa vipimo basi hapo mama ajitazamie mustakabali wake tu maana huyo jamaa inaonesha hakumjali mkewe tangu mwanzo na akaona za nje tamu,awaite basi waje kumuuguza.Misemo ya kizamani ya mchuma janga hula na wakwao tusiikaribishe,ukilichuma na kulila ulile peke yako.Kama huyo mke ataendelea kukaa hapo basi ajue naye ataukwaa tu,Ushauri wangu ni akimbie hata asigeuke nyuma aanze maisha mema kwa uangalifu zaidi.Kupata ukimwi kwa sasa ni uzembe na kujiendekeza maana tahadhari zote zinajulikana na asilimia kubwa huupata kwa kupitia ngono.Ukiona mwenzio kauleta ndani basi hapo ni sawa na kuambiwa uchague kifo na uhai sijui mwenye akili timamu atachagua kipi?
   
 15. dfreym

  dfreym JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mmh! kweli kazi. unajua some times mapenzi yanahitaji umakini ile mbaya. mi ushauri wangu ni kujifunza kuzoea kwamba maisha bila huyo mumewe yanawezekana. sa sijui kwa wazazi wa pande zote mbili. kuhusu dini je, lakini sidhani kama kuna dini inayoruhusu ndoa ya namna hiyo kuendelea. ushauri ni kutengana.
   
Loading...