Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,279
- 25,857
Kuna taarifa kuwa aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Phillemon Ndesamburo amefariki dunia. Kila mmoja, mwanachama na asiye mwanachama wa CHADEMA atakubaliana nami kuwa Ndesamburo alikuwa mzizi mkuu na ngome ya CHADEMA mkoani Kilimanjaro na kanda ya Kaskazini kwa ujumla.
Ndesamburo alikuwa mpigania chama, mjenga chama, mfadhili wa chama na kioo cha CHADEMA. Ndesamburo ndiye aliyekuwa kielelezo cha CHADEMA kwa kauli na matendo yake. Wananchi wa huko Kilimanjaro na Kaskazini kwa ujumla walivutiwa hadi kujiunga na CHADEMA na matendo na maneno ya Ndesamburo ndani na nje ya Bunge.
Nje ya maisha ya kisiasa, Ndesamburo alikuwa mlezi, mzazi, mnyenyekevu, mcheshi, muungwana, mwenye roho isiyo na inda wala mawaa na mtu mkweli. Aliwapenda waliompenda na hata wasiompenda. Alipendwa kwakuwa alikuwa akiendana na mazingira aliyokuwamo. Ndesamburo alisaidia panapohitajika na kubuni kwa kuwapeleka wananchi wa Tanzania mbele.
Kutokana na umuhimu wake ndani ya CHADEMA na kwa demokrasia ya nchi kwa ujumla, naishauri CHADEMA iahirishe shughuli zake zote na kujihusisha na msiba huo wa Hayati Ndesamburo. Hayo yatakuwa ni malipo yake stahiki kama mwanachama wao, mlezi wao, mpiganaji/kamanda wao, mfadhili wao, kivutio chao na wakujivunia wao.
Najua, Moshi Mjini, Kilimanjaro na Kaskazini yote itatikisika kwa maombolezo. Hakika, Ndesamburo ni nembo ya CHADEMA Bungeni na nje ya Bunge katika siasa za vyama vingi hapa nchini. Rest in peace the late Phillemon Ndesamburo aka Ndesapesa!