Ushauri wa Haraka Juu ya Mradi huu wa Biashara

IZENGOB

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
323
317
Habari zenu wakuu mimi ni mfanya biashara wa stetionary na Money Transfer(tigo pesa,airtel,voda na luku)hivi sasa mtaani kwetu biashara hii imeingiliwa kila mtu akifungua biashara anacopy na kupest kutoka katika biashara yangu, hapo mwanzo ilinitoa kiaina kwa kujenga nyumba na kumudu gharama za hapa na pale.
Shida yangu kubwa ni kubadili biashara,naomba ushauri katika wazo la biashara nililonalo.

Nimenunua hekali 10 huko kibiti Mkuranga nataka kufanya mambo yafuatayo
1. Kilimo cha biashara ya ufuta ambacho kitachukua heka 4.
2. Kilimo cha biashara cha matikiti kitachukua hekali 2.
3. Kilimo cha maembe ambayo nitayapanda kwenye mipaka ya shamba.
3. Ufugaji wa ng'ombe wa maziwa itachukia nusu heka.
4. Nitakua nanunua ng'ombe wa kienyeji kwa ajili ya biashara kutoka dodoma hasa mwezi wa 1,2,3 huwa wanashuka bei na kuwaleta kibiti kuwalisha pumba kwa muda wa miezi 5 kisha kuwauza itachukua Ekali 2.
5. Nitafuga kuku wa mayai na wa kienyeji Hekali 1.
6. Nitafuga samaki kwa kuanzia nitachimba bwawa litakuwa na Urefu wa futi 40 x40.
Mfukoni nina 10M, naomba wataalamu wa hii kitu wanishauri.Je hii project yangu italeta manufaa au la Je mazingira niliyochagulia kufanyia ni salama mimi naishi Dar es salaam.Naombeni nizijue changamoto za biashara hii.
 
Hiyo hela haitoshi kufanya yote hayo labda uchague mawili au moja, pia Kwa hali ya sasa ilivyo unabidi uwe karibu na hapo unapofanyia miradi yako maana hukawii kwenda asubuhi ukakuta ng'ombe hawapo.
 
Hiyo hela haitoshi kufanya yote hayo labda uchague mawili au moja, pia Kwa hali ya sasa ilivyo unabidi uwe karibu na hapo unapofanyia miradi yako maana hukawii kwenda asubuhi ukakuta ng'ombe hawapo.
Asante mkuu nitaanza na machahe kama kilimo na kuleta ng'ombe kwani tayari nimeshawanunua, Je kuna changamoto gani za kimazingira kama ng'ombe ukiwatoa mkoa mwingine kuwaleta pwani?
 
Back
Top Bottom