Ushauri wa dharura

uyo tabia yake tu kuangaika,uo upuzi ulioueleza hauwezi kua sababu ya mtu kuachana na mtu anae mpenda!
 
It just shows how women can say one thing and mean the other. Anyway, it will only be a matter of time before she realizes she has shot herself in the foot.
 
Mapenzi sio siku zote yatakuwa kwenye peak tu, kuna wakati inatokea hivi ,na inataka akili ya ziada ili kuweza kuendelea kuwa na amani, sasa hapo dada ako anakaribisha vidonda vya tumbo, maadam kagundua hajabembelezwa kwenda kwenye pati, siku ingine ansilaze damu,vipimo vingine huwa havifanyi kazi kwa baadhi ya wanaume
 
Habari zenu?
Dada yangu anahitaji ushauri wa haraka kabla hajapata shinikizo la damu.
Dada anahisi shemeji hampi kipaumbele kama yeye anavyo mjali . Kwa kweli dada anampenda sana huyo bwana,
na shemeji naye anakiri kumpenda sana dada lakini inaonekana kuwa ni maneno mengi ya wanaume kuliko ukweli.
Juzi kati dada alimpa mitihani midogo kumpima kujua kama kweli ana mapenzi ya dhati. Shemeji bila kujua akarukia kwenye hiyo mitego ikamnasa.

Mtego mmojawapo ni kuwa badala watoke wote kwenda kwenye sherehe ambayo walialikwa, dada akamwambia shem aende tu mwenyewe, na shem akafurahia sana hiyo outing ya peke yake kitu ambacho dada alikitafsiri vingine.Shem hakujaribu hata chembe kumsihi dada waongozane kitu ambacho siku za nyuma ilikuwa haijawahi kutokea. Kwa kifupi dada anataka kufanya maamuzi magumu ya kuachana naye maana anahisi kuna mtu wa pembeni anayemzuzua shemeji.

Waungwana nyie mnaonaje hili?
kama majibu yake alikuwa hayapendi ya nini aliamua kumjaribu mkaka wa watu,nimependa sana kilichomkuta kwani itakuwa fundisho kwa wanawake ambao wako tayri kuharibu ndoa zao kwa kuwajaribu wenzi wao utadhani wao ni mashetani hata wawajaribu wenzao
ukome!!!!!!
 
Habari zenu?
Dada yangu anahitaji ushauri wa haraka kabla hajapata shinikizo la damu.
Dada anahisi shemeji hampi kipaumbele kama yeye anavyo mjali . Kwa kweli dada anampenda sana huyo bwana,
na shemeji naye anakiri kumpenda sana dada lakini inaonekana kuwa ni maneno mengi ya wanaume kuliko ukweli.
Juzi kati dada alimpa mitihani midogo kumpima kujua kama kweli ana mapenzi ya dhati. Shemeji bila kujua akarukia kwenye hiyo mitego ikamnasa.

Mtego mmojawapo ni kuwa badala watoke wote kwenda kwenye sherehe ambayo walialikwa, dada akamwambia shem aende tu mwenyewe, na shem akafurahia sana hiyo outing ya peke yake kitu ambacho dada alikitafsiri vingine.Shem hakujaribu hata chembe kumsihi dada waongozane kitu ambacho siku za nyuma ilikuwa haijawahi kutokea. Kwa kifupi dada anataka kufanya maamuzi magumu ya kuachana naye maana anahisi kuna mtu wa pembeni anayemzuzua shemeji.

Waungwana nyie mnaonaje hili?

Hiki kipimo na huu mtego yaani vinafaa kabisa kuwa script ya King Majuto! Dah! nimecheka mbaya aisee!
 
Naamini kuwa mapenzi ni imani, kile unachoamini ndicho hasa kitakachotokea. Dada yako ameshaamini kuwa hapendwi, ameweka mtego, amekwishaandaa hypothesis zake, lazma jibu atapenda liwe ndani ya hypothesis zake. Pia moyo wa binadamu unabadilika, hayo ni mabadiliko ya kawaida, na ndcho kpmo cha ukomavu wa mapenzi. Mwisho.. Asimuwazie vibaya mume wake. Asifikirie kukimbia hiyo sio suluhisho.
 
Hujui kuwa wanawake wengi vichwa vyakuku? Kama yy ndo alimruhusu shemu wako kutoka peke yake we ulitaka afanyaje? Never say sorry to a lady.
 
avumilie kidogo tu. akikua atajua maisha si kupimana na maisha si vipimo. kuna mengi ya maana na mazito katika maisha kuliko hivyo vipimo na hata kushinda hicho anachohisi ...kuwepo na mtu wa nje.
 
Kuachana ni kutatua takizo kwa muda mfupi wala si la kudumu, kwanza huyo dadako mshauri ajiamini, kuwa na wasiwasi juu ya mumewe ni dalili ya kutojiamini kuwa yuko peke yake, mwangalie vizuri dadako kama ni mjamzito wala usihangaike, huwa mama zetu wakati kama huo wanapata negative psychological dispositions hasa kuona kuwa hawapendwi na waume zao.

Unaweza kukaa na shemejio kama wa2 wazima muongee juu ya hilo. Yote tisa, kumi ni kuwa huo unaouita uamuzi mgumu atakuja ujutia akigundua kuwa hisia zake hazijawahi kuwa za kweli.

MSHAURI AKAE KWENYE NDOA YAKE, akubali kuwa kuna milima na mabonde kwenye ndoa na si maziwa na asali kama wengi wanavyodhani!

Take ii or leave it!
Kujiamini huwa maana yake nini?
Unapohisi au kujua mtu wako anacheat, ina maana ndio kutokujiamini?Usipohisi ndio kujiamini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom