Ushauri wa bure: Usimpelekee mwanao wa kiume boarding school angali mdogo utakuja kulia na kusaga meno!

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Ushauri wa bure:Usimpelekee mwanao wa kiume boarding school angali mdogo utakuja kulia na kusaga meno!

Sisi kama wazazi yafaa kuambizana hili mapema boarding sio nzuri kwa watoto wadogo haifai kabisa sio kwa wasichana ama wavulana

Wenye hatari kubwa ni wavulana kwani boarding kule kuna hatari wa watoto kujifunza tabia za ajabu ajabu hata za ushoga na usagaji

Tafuta shule nzuri mwanao asome ambayo ataenda na kurudi kila siku ili uweze kupima tabia na kusimamia mwenendo wa mwanao na kumkuza vyema

Mimi wa kwangu wa kiume yupo Day ujinga wa boarding aliutaka mama yake nikaukataa kabisa hapa anaenda shule na kurudi kwa school bus mambo ya bweni niliyakataa

Kwanza huko ni kukwepa majukumu kama mzazi tokea chekechea mtoto anasoma boarding miaka 8 hadi anahitimu la saba (umri wa kubalehe) yupo boarding hivi hapo huoni ni hatari iliyoje?

Wazazi tuelewe majukumu yetu tembo hashindwi na upembe wake kama uliamua kuwa na watoto means unaweza kummudu kumlea mwanao kwani wazazi wengi huwapeleka watoto boarding ili kukwepa malezi ya watoto
 
Kweli kabisa mkuu boarding kwa watoto si nzuri vitu kama malezi mazingira ya shule. Mpangilio wakulala apa ndio hatali zaidi
 
Kama mwanao ana element za ushoga atakuwa nazo tu
Acheni kusingizia boarding school forhormonal imbalance
 
tatizo sio umri wala jinsia ya mtoto.
tatizo ni shule tulizo nazo za boarding hazina usimamizi makini kwa wanafunzi.

Nimewahi kwenda kwenye shule moja ya bweni ya wasichana tu siitaji jina, ila nilicho kishuhudia pale hakifai kupeleka mtoto.
hakuna uangalizi kabisaaa ni hatari.

Shule makini hakuna kabisaaa.
 
Mkuu binafsi nakubaliana na wewe kabisa, Kwanza uangalizi WA watoto sio mzuri Kwa baadhi ya shule na hivyo malezi ya watoto yapo hatarini Sana.

Lakini pili katika hili wimbi la mambo ya ushoga hakika ndio inakuwa mtihani kabisa, kwahiyo lililo jema ni kutowapeleka bweni katika umri mdogo
 
Kusoma boarding school kunaharibu sana kuna mshikaji wangu mmoja amesoma boarding kuanzia msingi mpaka A Level yaani mshikaji amekuwa kama broiler yaani saa moja kashaingia ndani kulala huwezi mkuta nje hata kwa bahati mbaya yaani mda mwingi yupo ndani tu boarding sio nzuri hasa kwa mtoto wa kiume
 
Back
Top Bottom