Ushauri wa bure kwako Michael Wambura

Prof Decentman

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
276
140
Nianze na kukupa pole katika kashkashi unazokumbana nazo katika kutimiza ndoto yako ya kuwa kiongozi katika taasisi za michezo katika nchi ya Tanzania.

Kwanza mimi binafsi si mwana michezo na sina interest zozote na michezo, sina timu ninayoshabikia japo ninatamani nchi yangu na timu zetu zifike mbali katika michezo. Yaani hata sasa kombe la dunia linapoendelea ninalala zako usingizi mzuri habari sina zaidi ya kusikia matokeo baada ya mechi kwisha.

Lakini nina kipande kidogo cha ushauri ambacho waweza kukitumia na ninajua yawezekana umeshaambiwa na mimi naongezea tu kidogo japo nilitamani kutoa ushauri huu mapema lakini nikasema ngoja nisubiri part three ya hii muvi sijui ndo ya mwisho au tusubiri kuna part 4 na 5, sijui.

Unajua najaribu kuwaza au kuingia katika viatu vyako. Nakuona ukiwa na ndoto, pengine uliianza hapo kabla (maana najua ulishawahi kuwa kiongozi wa soka) na unatamani kuimalizia au kuboresha zaidi.

Pengine una kitu ambacho umekiona na ukatamani sana sana kukitimiza kupitia nafasi yako kama kiongozi. Na kama mtu yeyote anayetaka jambo lake lifanikiwe haliishii katika ndoto hivyo umejaribu kuliweka katika vitendo.

Lakini bahati mbaya umekutana na 'rejection' ama kukataliwa. Najaribu kuwaza jinsi unavyojisikia kwa hao wanao kukataa ama kukuwekea mizengwe. Nina uhakika kwa hulka za kibinadam hakuna mtu ambaye atajisikia vizuri anapo kataliwa ama kupata changamoto za kufanya kile anachotamani.

1. Nina amini kuwa unayo dhamira ya dhati toka moyoni mwako kufanya mabadiliko ama kutimiza ndoto zako hizo. Ila kabla hujafanya jambo lolote unapaswa kufanya 'SWOC' ninajua wewe kama msomi unalijua hili.

Angalia (Kile unachoweza) strength zako, weakness zako (Udhaifu), Fursa zilizopo ( Opportunity) na Changamoto zilizopo (Challenge) ili ufanye maamuzi sahihi kabisa.

a. Strength zako: Nina imani hichi unachokiamini unaweza ndicho kinacho kusukuma kupambana miaka yote hii kutafuta uongozi katika vyama vya soka, yawezekana ni uzoefu wako a uongozi wa soka, yawezekana una network na wadau wa soka nje, yawezekana ni kutokupenda rushwa na kutenda haki katika mambo ya soka etc.

Cha kufanya: Endelea kujiimarisha katika mambo hayo na tafuta vitu bora zaidi ili uwe bora zaidi.

b.Wewe kama binadamu yawezekana una madhaifu yako ambayo hayo wenzanko au wanao kufahamu wamewekeza katika hayo kuhakikisha unashindwa kutimiza ndoto zako.

Cha kufanya: Anza sasa kujitathmini uone ni wapi kuna shida hivyo jipange upya kwa namna nyingine yoyote kutimiza ndoto yako.

c.Fursa: Nikitazama katika mambo ya michezo japo mimi sio mtaalam naona zipo fursa nyingi sana. Naona yapo maeneo makubwa nchi hii na ukanda huu wa pwani vinaweza kujengwa viwanja vikubwa vya michezo, naona vijana wengi wenye vipaji ambao wanaweza kutengeneza timu nzuri kwa mtu yeyote kumiliki tena bila gharama kubwa, naona maduka ya vifaa vya michezo na fursa nyingine nyingi katika sanaa, naona fursa ya kutengeneza shule za michezo ukauza wachezaji etc.

Cha kufanya: Achana na changamoto za simba na yannga zisikupotezee muda, ni wakati muafaka sasa uanzishe timu yako. Haitakuchukua miaka 10 - 20 utafurahia matunda ya timu yako na wewe mwenyewe ukiwa ni kiongozi mwenye kutimiza ndoto uliyo nayo kupitia watu wengine, angalia mfano wa Azam. Wapo vijana wengi sana wenye mapenzi na michezo watakachohitaji toka kwako ni uhakika wa chakula tu na mahitaji madogo madogo, nina uhakika timu yako itakuwa miongoni mwa timu nzuri Tanzania mnamo 2020.

Yawezekana unalo duka la vifaa vya michezo au gym ni muda muafaka wa kuendelea kuwekeza katika hayo.

Anzisha shule ya michezo, najua kwa network uliyo nayo na resource zako utafanikiwa sana katika hili.

Tafuta maeneo yapo mengi nunua na utafute mwekezaji mjenge kiwanja kizuri, simba na yanga hakika wana weza kuwa wateja wako, hope utawahudumia bila kinyongo.

d. Changamoto (Challenge) Angalia ni changamoto zipi zinaweza kufanya usifanikiwe. Ukiendelea kuwepo huko nadhani nafasi ya kufanikiwa ni ndogo kwa kuwa soka letu limetawaliwa na fitina, uzandiki na namna zote mbaya.

Zipo changamoto nyingi za ndani na nje unaweza kupitia ikiwemo kukosa fedha, kupata wa kukusapoti wenye ndoto kama zako, vifaa vya michezo, taratibu za kisheria, kutumia muda wako mwingi kufatilia mambo haya.

Cha kufanya: Tengeneza mkakati mzuri kukabiliana na changamoto zote hizi, tafuta best people wanaoweza kuelewa una maana gani kurisk muda wako, fedha zako, mali zako na akili yako simply because unataka kutimiza ndoto zako.Jiunge na wafadhiri wapenda michezo wenye mitaji yao waambie kama ilivyo Afrika magharibi, Afrika mashariki wapo vijana wengi wazuri wacheza soka wana oweza kuuzika katika soko la kimataifa.

Ili mwanadamu yoyote afanikiwe anahitaji mambo matatu:
1. Apende sana na kuwa na nia ya kitu anachokifanya (interest kubwa sana)
2. Awe na ujuzi ( technical know how) ya hicho anacho kifanya
3. Awe angalau na uzoefu wa hicho anachokifanya.

Ukiwa na vitu hivi hata kama huna mtaji fedha ni lazima ufanikiwe.

Mwisho nikukumbushe wapo watu walishindwa mara nyingi kuliko hata wewe, wengine ni katika siasa lakini kwa sababu walikuwa focused na ndoto zao mwisho walifanikiwa. Usikubali watu wa kukatishe tamaa, as long as you want to achieve your dream.

Kwa leo niishie hapo.
 
Wambula kma anayaka uongozi si aanzishe timu yake,?mbona ni simple tu.
 
Aanzishe timu yake...
Simba na TFF ni vichaka vya walaghai na mafisadi...
 
Mmmmhhh SWOC....!!!!! Au SWOT? Msaada kwenye kituo
huwa ni SWOT Analysis ila hatuna haja ya kukariri vitini vya darasani kama vilivyo, nimeona hata SWOC imekaa poa tuu maana T-THREAT na C-CHALLENGE ni concept zenye kuendana na zina maana zinazoshabihiana.
Challenges can be threat, and the same time Threats can be Challenges
 
FOS matapeli tuu, kama wana pesa na wanaona mpira ni pesa zaidi, waanzishe timu zao basi kama Bakhresa sio kuja kuweka vibaraka klabuni watakaondeshwa kama pangaboi!
wewe mgombea unapewa gari,unapewa pesa za kampeni, unapewa kila kitu unadhani atakuja kuwa na sauti huyo mgombea FOS hata akishinda? unadhani ataweza kupinga shinikizo za FOS?
 
Mtoa mada kanjanja na wachangiaji wanaosema Wambura aanzishe timu yake makanjanja, mbona haushauri hao wanaojitapa wana pesa akina Azim Dewj waanzishae timu zao? Acheni kutumika kama Kondom.
 
huwa ni SWOT Analysis ila hatuna haja ya kukariri vitini vya darasani kama vilivyo, nimeona hata SWOC imekaa poa tuu maana T-THREAT na C-CHALLENGE ni concept zenye kuendana na zina maana zinazoshabihiana.
Challenges can be threat, and the same time Threats can be Challenges

Ni kweli mkuu lakini mtoa mada hakutakiwa kumia abbreviation aliyoitumia coz kimsingi hiko kitu hakipo, kama angeongea maelezo tu hakuna shida ila kwa kuweka na capital letters kabisa kitu sicho
 
Hao marafiki wa mbumbumbu ni wahuni tu maana hakuna kitu walichowahi kufanya tangu wameingia hapo. ......wanambumbumbu wajiulize tangu 2000 mpaka leo wamefanya nn zaidi ya kuhujumu viongozi wanaopingana nao, hao ni umoja wa matapeli tu katu simba aka mbumbumbu haitafanikiwa ikiwa hao wauza unga wataendelea kuwepo
 
Nikiwa mwanasimba damu sitakanyaga mechi yoyote ya Simba.. Ubabaishaji mwingi.
 
Mtoa mada kanjanja na wachangiaji wanaosema Wambura aanzishe timu yake makanjanja, mbona haushauri hao wanaojitapa wana pesa akina Azim Dewj waanzishae timu zao? Acheni kutumika kama Kondom.

Hawa wengine wamedhamiria kufia simba ila yeye amedhamiria uongoz wavsoka ndo maana alipambana tff, mara na sasa karudi tena simba.
 
Ni kweli mkuu lakini mtoa mada hakutakiwa kumia abbreviation aliyoitumia coz kimsingi hiko kitu hakipo, kama angeongea maelezo tu hakuna shida ila kwa kuweka na capital letters kabisa kitu sicho
Soma vzr post yang maneno yote yamefafanuliwa...
 
Back
Top Bottom