Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,825
- 730,231
Tasnia ya sanaa kwa kasi Tanzania, sanaa imekuwa ni ajira rasmi kwa vijana wengi, na wengi wamefanikiwa kimaisha kupitia maigizo, vichekesho miziki filamu uchoraji uremia nk
Kwasasa sanaa inayotamba sana ni sanaa kupitia muziki, hii Pengine ni kutokana na mafanikio waliyopata baadhi yao
Bila kumung'unya maneno asilimia 90 ya wasanii wetu wa fani wana vipaji lakini elimu yao ni ndogo.
Elimu humsaidia mtu kumpa mwanga zaidi maarifa zaidi ,ufahamu zaidi hekima na hata tafakuri...... Kipaji bila elimu ni tatizo
Ni kukosa huku elimu wasanii wengi wamejikuta wakiingia kwenye migogoro na serikali ama na jamii kutokana na kazi zao kukosa viwango ama kuvunja maadili.... Wengi wameshindwa kabisa kutumia nahau fasihi ngeli za kiarifa methali mafumbo na lugha kinyume.....
Msanii mzuri ni yule anayetengeneza kazi fikirishi
Bila kutaja jina la mtu moja kwa moja
Bila kutaja mahali
Bila kueleza kitu Kama kilivyo
Usanii huendana na ubunifu, ubunifu fikirishi, ubunifu kificho, kwa muktadha huo matumizi ya nahau fasihi na ngeli huwa murua na kuleta ladha fulani, kwa njia hii msanii hujiepusha na mengi huku akikwepa mishale mingi ya jinai kufungiwa na hata kunyooshewa vidole
Udhaifu wa kukosa ubunifu umewaweka wengi matatani na zamu hii ni ya Ney wa Mitego...... Vema awe funzo kwa wengine sanaa sio insha