Elections 2010 Ushauri wa bure kwa Slaa

Kwanza ni lazima tumpe Dr. Slaa hongera sana kwa kazi kubwa ya siku 71 ambazo amezitumia vyema kuipaisha bendera ya CHADEMA angani. Kupata wabunge zaidi ya ishirini (>20) na kukifanya chama kikuu cha upinzani sio jambo dogo. Kuwangusha vigogo kama Lau Masha na Anthony Diallo sio masihara.

Sasa kazi moja imebaki na ni ya kukijenga chama sehemu za vijijini na kwenye miji yenye uswahili mwingi na woga wa mabadiliko kama Tanga, Ilala, Tabora, Morogoro etc. Hakuna anayeweza kuongoza mapambano hayo zaidi kamanda Dr. Slaa.
 
Hilo neno umempatia huyo fisadi wa mawazo ndo size yake
''CRAP''an offensive term meaning to pass sold waste matter out of the body thruu the anus
 
Acha utani wa namna hiyo.Dr Slaa bado ana nguvu na hata kiumri bado sana, kwa hivi sasa ana miaka (62) tu, huo ni umri mdogo sana.Watanzania bado wanahitaji awe kwenye active politics, kuhamasisha, kuamsha na kuleta mabadiliko kwenye nchi yetu.Nina imani mwaka 2015 atafanya vizuri na kushinda uraisi.Na ukae ukijua kwamba alitembelea majimbo yasiyozidi 79 kati ya 232 ya uchaguzi.Hivyo cheche chake bado hazijawafikia wengi.Na ushauri ninaompa Dr Slaa na Chadema ni kwamba kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ajikite kutembelea na kukitangaza chama chake ili zaidi ya asilimia 80 wamjue.Na kwa kufanya hivyo nakuhakikishia uchaguzi wa 2015 ataibuka kidedea and the world will be taken by storm.God bless and give Dr Slaa long life.
 
Ujinga na uchokozi na ni matusi aliyesema Dr.wa ukweli atapata 20% nani, subirini firimbi ipigwe ndipo msikie kitakacho jiri !
 
Wana-JF wapenda mabadiliko ya kweli yenye manufaa kwa nchi yetu hatuna budi kumpongeza kwa dhati kutoka ndani ya nyoyo zetu Dk. Wilbroad Peter Slaa kwa kazi nzuri na kubwa mno aliyoifanya kwa Chama chake CHADEMA, kwa Tanzania yetu na Watanzania wanyonge kwa ujumla.

Awali ya yote, Dr. Slaa amejinyanyua na amekinyanyua chama chake juu kabisa. Dr. Slaa amekuwa tishio na mwiba uliowachoma viongozi wa CCM katika kipindi chote cha Kampeni na upigaji kura. Dr. Slaa aliweza kubadili hali ndani ya CCM na chama hicho kutokuwa na uhakika wa ushindi na hata pale viongozi wa juu wa CCM nyuso zao zilionyesha taharuki walipokuwa wakitumbukiza kura zao kwenye masanduku ya kura. Dr. Slaa amefanikiwa kuondoa kujiamini kupita kiasi kwa viongozi hao wa CCM na wanachama wa chama hicho kwamba ushindi kwao hauwezi wakati wote kuwa wa cheeeee kama ilivyokuwa huko nyuma. Dr. Slaa alipoingia ulingoni kila kitu kilibadilika. Asante Dr. Slaa kwa kuwaamsha viongozi wa CCM na wanachama wao kutoka lindi la usingizi la kudhani kwamba wakishavaa magwanda ya kijani na njano kwenye mikutano ya kampeni basi wataendelea kupata na kuchaguliwa kuwa watawala wa nchi hii daima dumu.

Dr. Slaa amefanya tuelewe kwamba CCM sasa kimefikia ukingoni katika uhalali wa kuiongoza Tanzania yetu. Dr. Slaa ameweza kutuonyesha jinsi CCM kilivyooza na kuharibika kutokana na vitendo vya rushwa iliyokithiri tangu kwenye kura za maoni za chama hicho hadi kipindi chote cha kampeni. Je. CCM wanaweza kututajia ni mgombea gani wa chama hicho ambaye hakutoa chochote kuwashawishi wananchi wamchague? HAKUNA!

Dr. Slaa ametufungua macho, masikio na akili zetu kuelewa kwamba bila kutumia nguvu za ziada za rushwa na mabango kila kona, CCM si lolote kimepoteza mvuto na uhalali wake wa kuongoza wananchi. Wakati wote CCM imekuwa ikipanga mbinu mbalimbali za kujitafutia ushindi kwa nguvu, ushindi usio halali. Tumejionea wenyewe jinsi ambavyo kura za mijini na vijijini zilivyoweza kuwa na tofauti kubwa. Kwa nini? Kwa sababu CCM wametumia umaskini wa wananchi wa mijini na vijijini kama mtaji wao wa kupatia kura. Wamewahonga wananchi t-shirt, kofia, skafu, pombe, sukari, chumvi, kanga, pikipiki, baiskeli, vijisenti viduchu kiasi cha elfu moja ama mbili n.k. ili waweze kupata kura kutoka kwao. Ni aibu kubwa kwa Chama chochote cha siasa kufanya mambo hayo kwa makusudi ya kuwarubuni wananchi ili chama hicho kichaguliwe.

Wana-JF wapenda mabadiliko na wanaoitakia mema Tanzania yetu, hatuna budi kumshukuru sana Dk. Slaaa kwa kuweza kutufumbua macho na kuweza kuyaona maovu yote hayo kwa ukweli, uwazi na mwanga zaidi.

Tumuombe Dk. Slaa asife moyo kabisa kwa kukosa ushindi katika uchaguzi huu. Yeye ni shujaa na tena ni ‘Rais’ wa Watanzania wanyonge aliokuwa akijaribu kuwatetea kwa dhati majukwaani akionyesha dhahiri kuwa na uchungu wa dhati kwa Watanzania hao waliopigika. Tumuombe Dk. Slaa asherehekee ushindi wake yeye binafsi na ushindi wa CHADEMA na hata wa vyama vingine vya Upinzani vilivyoweza kupata viti Bungeni na kwenye safu ya Udiwani ambao tunaamini kabisa umetokana na yeye Dk. Slaa na si vinginevyo.

Tumuombe na tumuunge mkono Dk. Slaa aanze sasa kukijenga na kukiimarisha CHADEMA tayari kwa mapambano mapya ya 2015. Twendeni vijijini tumsaidie. Hatuendi huko tukiwa tumebeba mafurushi ya kanga, t-shirt n.k. lakini tunakwenda huko na dhamira ya dhati ya kuwaelimisha wananchi wenzetu kwamba maisha bora kwao yataweza kuja tu pale watakapoelewa nini maana ya utawala bora na haki yao ya msingi ya kuweza kugundua na kuchagua viongozi watakaoweza kuwasaidia kuyatafuta hayo maisha bora kwa kutumia raslimali ambazo ni mali ya kila Mtanzania kwa manufaa ya Watanzania wote na si wachache.

Zaidi ya hayo, ushindi wa CCM safari hii na amani na utulivu katika upigaji kura na kusubiri matokeo na kuyakubali vimetokana na kile alichokijenga Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Kinachoshangaza, CCM wamebaki kujisifia wao juu ya hali hiyo na kutaka kurushia lawama kwa vyama vya upinzani kila zinapotokea rabsha ndogo ndogo wakisahau kwamba wananchi wa Tanzania bila kujali vyama vyao ndio wadau wakubwa na wajengaji wa hali hiyo ya amani na utulivu iliyotamalaki kwa miaka mingi hadi kuonekana ni jambo la kawaida. Cha kushangaza zaidi ni kwamba CCM kwenye kampeni zao wameonekana dhahiri kunyanyapaa hata jina la Mwalimu Nyerere! Mgombea gani wa CCM aliyejaribu kuomba kura kwa kutumia jina la Mwalimu Nyerere zaidi ya Dk. Slaa wa CHADEMA?

Tumuombe Mungu ampe Dk. Slaa nguvu na uwezo wa kuendelea kupambana kwa manufaa ya Watanzania. Mungu ampe ujasiri wa kufuata nyayo za Baba wa Taifa.

Dk. Slaa ni Mwanamume! Ameweza kuwanyima usingizi viongozi wa CCM waliodhani kuwa kwao uongozi wa nchi yetu ni haki yao ya kuzaliwa!

HONGERA SANA DK. SLAA, NA MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA!
 
Una posts 77 na huna thanks hata moja. That tells me what kind of a person you are.

Dr. Slaa hana uchu wa madaraka kama Dokta(mjanjamjanja) Mkwere. Slaa yupo kwa ajili ya taifa lake na sio kwa ajili yake binafsi na ndio maana kupitia yeye CCM wanagaragazwa mchana kweupeeee tena na watoto wadogo sana.

Dr. Slaa kaanzisha marathon ya mapambano dhidi ya mkoloni mweusi na vizazi vyote vinamfuata baada ya hapa.

Tatizo langu ni kuwa hawa wanafunzi waliokataliwa wasipige kura nna uhakika mwaka 2015 wengi wao watakuwa mitaani wakiwa na hasira ya kukataliwa na pia watakuwepo wengi tu huko kwenye vyuo ambavyo vinazaliwa kila siku. Ni kwamba CCM wameahirisha kimbunga, kingine kipo njiani kinajikusanya.

Hakuna bati ambalo halitaezuliwa.

Ni kweli Chesty sina thanks hata moja, sijui kwa nini watu wa hii forum hawa-appreciate contribution zangu.

Nalifanyia kazi.
 
Tuheshimiane wana forum. Tuache matusi.

Huu ni ushauri tu ,unaweza kukubalika au kukataliwa.
Ila naamini ni ushauri mzuri, akiupuuza matokeo yataonekana na Chadema itaathirika.

Acheni hasira tunapomshauri kiongozi.

Wewe Kishongo una wazimu kama siyo mtindio wa ubongo!!
Inaonekana wewe ndiye Riz1 a.k.a Kishongi . Ushauri wako ni pumba tupu. Hivi vijibabu na vijibibi vya CCM mbona hujavshauri vikapumzika???
Vikina Kingunge,Lowasa,Malecela,Mramba,Shein,Anne Makinda,Wasira na...................the list is too long!!!Kiwete(61) mwenyewe ni kibabu mbona hujamshauri akuteua kugombea hiyo nafasi yake????Go tell them to quit politics as they're elder than Dr.Slaa!!!

CCM mlie tu nchi inachukuliwa na CHADEMA hii, fanyeni mfanyavyo lakini mjue kabisa sasa hivi CCM KWEISHNE. Pambaf zenu.
 
Kazi bado ni ngumu kwa watu waliojikita miaka 50 mpaka ngazi ya shina {nyumba kumikumi} na kulisha wananchi sera na imani zao ni kazi kubwa kuwaondoa, tayari viti zaidi ya ishirini ilivyopata Chadema mpaka sasa kutoka 5, ni ushindi mkubwa usiotakiwa kubezwa na Dr Slaa amefanikisha ushindi huo kwa 100%, kugombea Urais kwa vyama vichanga haina maana ya kuingia Ikulu pekee bali kukieneza chama na kutangaza sera zake, ashindwe au ashinde bado ana kazi kubwa ya kukieneza, kukikuza na kukiongoza chama kwani bado waheshimiwa Wenje,Mdee,Sugu na wengine wanamuhitaji sana sasa kuliko mda mwingine wowote.
 
Back
Top Bottom