Ushauri wa Wazi kwa CHADEMA/UKAWA

Sophist

Platinum Member
Mar 26, 2009
4,486
3,407
Huu ni ushauri kwa Chadema/Ukawa.

Siasa mnazofanya kwa sasa zinakizika Chama. Mkakati wa kisiasa mliokuwa mkiutumia enzi za JK haufanyi kazi tena nyakati hizi za JPM. Chama kinatakiwa kutumia mbinu za kisomi zaidi kuliko mbinu za kiharakati na physique. Kwa sasa mnatakiwa kuangalia namna nzuri ya kufanya convergent badala ya divergent political/government engaging strategy. Kwa mfano, UKAWA ingetumia convergent engaging strategy, impact ya KUB Bungeni juzi ingekuwa kubwa zaidi and more rewarding kuliko kilichotokea au matokeo yake huko tuendako.

Kwa sasa uongozi wa Chama unapaswa kufahamu kuwa sehamu kubwa ya vijana waliohamasishwa na kujiunga Chadema huko nyuma, sasa wako kwa JPM (siyo CCM). Kwa hiyo Chama kina kazi ya kuwarudisha hao, na wakati huo huo, kuhamasisha wanachama wapya. Kama uongozi hautatambua ukweli huo Chama kitaendelea kupoteza wanachama; wa-zamani na wapya.

Chama kinaweza kujikuta, katika muda mfupi ujao, kinachukua nafasi ya CCM ya enzi za JK, wakati JPM anachukua nafasi ya Chadema ya enzi za Slaa.

Kuna njia moja ya kuandaa na kutekeleza mkakati mpya; uongozi wa Chama unapaswa kutambua kuwa sasa umefikia turning point. Kwamba one way drive/linear political strategy is no longer working for Chadema. Groom/recruit new energetic youthful party leadership (kama mlivyofanya kwa Daktari Mashinji) then take back seats. Waachie viongozi wapya waendeshe upande wa pili wa parabola ya Chama (y= ax2 +bx +c).

Tafakari
 
Chadema iendelee kuikosoa serikali na chama tawala kwa umakini na nguvu kubwa ili tuweze kuongozwa kwa weledi kwawale waliopo madarakani,iwe Kama enzi za Jk ama zaidi yapale yote ni sawa.
Hakuna cha ajabu saana katika awamu hii chakufanya upinzani kubadilika,bado kutakuwa na dosari ambazo upinzani wanapaswa kuzikemea ili nchi inyooke vizuri!!
Kumpata rais tuliyenaye,anayeamini mengi ambayo upinzani wamekuwa wakiyasemea ni fanikio kubwa kwa upinzani...kamasio presha za upinzani siajabu rais angekuwa Sita ama mwandosya pengine hâta Chenge!! Lakini tizama kwa msukumo Wa upinzani tumempata mtu mahiri Magufull.
 
Huu ni ushauri kwa Chadema/Ukawa.

Siasa mnazofanya kwa sasa zinakizika Chama. Mkakati wa kisiasa mlioutumia enzi za JK haufanyi kazi tena nyakati hizi za JPM. Chama kinatakiwa kutumia mbinu za kisomi zaidi kuliko mbinu za kiharakati na physique. Kwa sasa mnatakiwa kuangalia namna nzuri ya kufanya convergence badala ya divergence political/Government engaging strategy. Kwa mfano, mngetumia convergence engaging strategy, impact ya KUB Bungeni juzi ingekuwa kubwa zaidi and more rewarding kuliko kilichotokea au matokeo yake huko tuendako.

Kwa sasa mnapaswa kufahamu kuwa sehamu kubwa ya vijana mliowahamasisha na kujiunga Chadama wako kwa JPM (siyo CCM). Kwa hiyo chama kina kazi ya kuwarudisha hao na wakati huo huo kuhamasisha wanachama wapya. Kama hamtatambua ukweli huo mtaendelea kupoteza wanachama wa zamani na wapya.

Mnaweza kujikuta, katika muda mfupi ujao, mnachukua nafasi ya CCM ya JK wakati JPM anachukua nafasi ya Chadema ya Slaa.

Kuna njia moja ya kuadaa na kutekeleza mkakati mpya; uongozi wa Chama kutambua kuwa sasa umefikia turning point. Kwamba one way drive political strategy is no longer working for Chadema. Groom/recruit new energetic youthful party leadership (kama mlivyofanya kwa Daktari Mashinji) then take back seats. Waachie viongozi wapya waendeshe upande wa pili wa parabola ya Chama (y= ax2 +bx +c).

Tafakari
Ushauri mzuri japo unaweza kukuletea matatizo hasa kama wewe ni mwenzao. Hapo mwisho naomba uniweke sawa; ina maana unataka Chama kipate Mlezi mpya pamoja na Mwenyekiti mpya?
 
Huu ni ushauri kwa Chadema/Ukawa.

Siasa mnazofanya kwa sasa zinakizika Chama. Mkakati wa kisiasa mliokuwa mkiutumia enzi za JK haufanyi kazi tena nyakati hizi za JPM. Chama kinatakiwa kutumia mbinu za kisomi zaidi kuliko mbinu za kiharakati na physique. Kwa sasa mnatakiwa kuangalia namna nzuri ya kufanya convergent badala ya divergent political/government engaging strategy. Kwa mfano, UKAWA ingetumia convergent engaging strategy, impact ya KUB Bungeni juzi ingekuwa kubwa zaidi and more rewarding kuliko kilichotokea au matokeo yake huko tuendako.

Kwa sasa uongozi wa Chama unapaswa kufahamu kuwa sehamu kubwa ya vijana waliohamasishwa na kujiunga Chadema huko nyuma, sasa wako kwa JPM (siyo CCM). Kwa hiyo Chama kina kazi ya kuwarudisha hao, na wakati huo huo, kuhamasisha wanachama wapya. Kama uongozi hautatambua ukweli huo Chama kitaendelea kupoteza wanachama; wa-zamani na wapya.

Chama kinaweza kujikuta, katika muda mfupi ujao, kinachukua nafasi ya CCM ya enzi za JK, wakati JPM anachukua nafasi ya Chadema ya enzi za Slaa.

Kuna njia moja ya kuandaa na kutekeleza mkakati mpya; uongozi wa Chama unapaswa kutambua kuwa sasa umefikia turning point. Kwamba one way drive/linear political strategy is no longer working for Chadema. Groom/recruit new energetic youthful party leadership (kama mlivyofanya kwa Daktari Mashinji) then take back seats. Waachie viongozi wapya waendeshe upande wa pili wa parabola ya Chama (y= ax2 +bx +c).

Tafakari
Ushauri mzuri, lakini kwa vile umetumia mtandao kuutoa, sidhani kama macho kumchuzi (Mbowe) atakuelewa.
 
Ukiwaambia Chadema wa inaelekea kuchukua nafasi ya CCM enzi za JK maana yake inaelekea kuchukua nafasi ya ushindi. CCM ilishinda chaguzi zote zilizofanyika kipindi cha JK.

Ukisema JPM anachukua nafasi ya Slaa unakosea. Slaa ni mshindwa. Sidhani kama JPM anaelekea kuwa mshindwa kama Slaa.
 
Ushauri mzuri, maana hata huku kitaa vijana wanasema mbona CDM inatetea wezi wanaotumbuliwa?

Wakitoka mtoni watakuja na matusi....jiandae.
 
Huu ni ushauri kwa Chadema/Ukawa.

Siasa mnazofanya kwa sasa zinakizika Chama. Mkakati wa kisiasa mliokuwa mkiutumia enzi za JK haufanyi kazi tena nyakati hizi za JPM. Chama kinatakiwa kutumia mbinu za kisomi zaidi kuliko mbinu za kiharakati na physique. Kwa sasa mnatakiwa kuangalia namna nzuri ya kufanya convergent badala ya divergent political/government engaging strategy. Kwa mfano, UKAWA ingetumia convergent engaging strategy, impact ya KUB Bungeni juzi ingekuwa kubwa zaidi and more rewarding kuliko kilichotokea au matokeo yake huko tuendako.

Kwa sasa uongozi wa Chama unapaswa kufahamu kuwa sehamu kubwa ya vijana waliohamasishwa na kujiunga Chadema huko nyuma, sasa wako kwa JPM (siyo CCM). Kwa hiyo Chama kina kazi ya kuwarudisha hao, na wakati huo huo, kuhamasisha wanachama wapya. Kama uongozi hautatambua ukweli huo Chama kitaendelea kupoteza wanachama; wa-zamani na wapya.

Chama kinaweza kujikuta, katika muda mfupi ujao, kinachukua nafasi ya CCM ya enzi za JK, wakati JPM anachukua nafasi ya Chadema ya enzi za Slaa.

Kuna njia moja ya kuandaa na kutekeleza mkakati mpya; uongozi wa Chama unapaswa kutambua kuwa sasa umefikia turning point. Kwamba one way drive/linear political strategy is no longer working for Chadema. Groom/recruit new energetic youthful party leadership (kama mlivyofanya kwa Daktari Mashinji) then take back seats. Waachie viongozi wapya waendeshe upande wa pili wa parabola ya Chama (y= ax2 +bx +c).

Tafakari
Kiukweli zama zimebadilika...strategies zao pia zibadilike....naunga mkono mtazamo wako mkuu.....its time for new strategies. Pia wapime uzito wa mambo. Kuna mambo ambayo ni key na ukisusia watakaoathirika ni wapiga kura wako. Enzi za migomo ziishie vyuoni....
 
Mleta uzi umeleta ushauri mzuri ni vyema ukafanyiwa kazi. Ila kwa jinsi ninavyoona hali ya mambo, hao wapinzani hawana muda watapa tena uungwaji mkono maana naanza kuona makosa ya ccm yanaanza kujirudia kwa mtindo tofauti. Kinachofanyika sasa mpaka wapinzani waonekane hawapo ni covarage kubwa kwa rais huku wakihakikisha wapinzani hawasikiki kwa lolote. Hali hii naifananisha sana na mechi ya mpira unaanza kwa kupata goli 2 za harakahara tena magoli yenyewe wapinzani wako wanajifunga wenyewe. Lakini kadiri mechi inavyoendelea timu iliyo nyuma inarudi mchezoni.

Nasema hivyo kwanini? Ccm hii chini ya Magufuli siioni ikifanya vizuri kwenye mikakati hasa itakapokuja suala la uchumi. Sehemu kubwa naona ni ahadi zilezile tulizozizoea, kitisho kikubwa ni pale rais wetu anapotumia kauli za kibabe kwa mataifa yanayoweza kutupa technologia ya kisasa ili kuifanya nchi yetu kuwa ya viwanda. Lugha za rais wetu ni hatari sana hasa kwa nchi inayoagiza mpaka toothpick. Ni kweli atakusanya kodi kama anavyojinasibu, ila kama huzalishi toka viwandani ni kama kupaka rangi upepo. Sioni jitahada za dhati kukuza kilimo ambapo ndipo hasa tutapata malighafi za viwanda iwapo kweli tutavijenga hivyo viwanda. Nilitaraji wangalau 40% ya bajeti iende kwenye kilimo ili tuweke msingi imara wa malighafi zitakazotumika viwandani. Hivi unahubiri viwanda lakini huna msingi wa raslimali huoni kama hapo kuna nafasi ya upinzani mzuri kutumia udhaifu huo kujijenga na kuwin tena watu? Kumbuka sisi wnanchi sio wageni wa ahadi, hasa ahadi hizo zinapotolewa na kiongozi wa nchi tena kwa kauli za kibabe. Mugabe alipowagaia wananchi wake ardhi kwa kupora wazungu miaka ya mwisho wa 80 alipata uungwaji mkono sana. Leo hii yako wapi? Mfano mrahisi ambao wapinzani watapate tena nafasi iwapo watacheza karata zao vizuri ni haya makosa madogo madogo ya serekali, kama kutangaza bei ya sukari itakuwa sh 1800 lakini bei halisi ni 2300-2500 tena hiil linafanyika muda mfupi baada ya tamko la serekali. Nina mashaka sana na TZ ya viwanda tena kwa Lugha za kejeli za kiongozi wetu dhidi ya nchi ambazo zina techologia kubwa. JK pamoja na diplomasia yake nzuri hakufanikiwa kujenga viwanda vya maana hapa nchini. Tunajidanganya na hao wachina, je ni kweli wachina ni wa kuwaamini kiasi hicho? Mbona wana mazingira mazuri lakini mpaka leo hawajajenga viwanda vyao hapa nchini mbali ya mazingira kuwaruhusu? Sioni kama ccm inapaswa kujisifia dhidi ya upinzani eti kisa imepata magoli ya mapema na ianze kushangilia kombe kwani mechi ndio kwanza mpya.
 
Huu ni ushauri kwa Chadema/Ukawa.

Siasa mnazofanya kwa sasa zinakizika Chama. Mkakati wa kisiasa mliokuwa mkiutumia enzi za JK haufanyi kazi tena nyakati hizi za JPM. Chama kinatakiwa kutumia mbinu za kisomi zaidi kuliko mbinu za kiharakati na physique. Kwa sasa mnatakiwa kuangalia namna nzuri ya kufanya convergent badala ya divergent political/government engaging strategy. Kwa mfano, UKAWA ingetumia convergent engaging strategy, impact ya KUB Bungeni juzi ingekuwa kubwa zaidi and more rewarding kuliko kilichotokea au matokeo yake huko tuendako.

Kwa sasa uongozi wa Chama unapaswa kufahamu kuwa sehamu kubwa ya vijana waliohamasishwa na kujiunga Chadema huko nyuma, sasa wako kwa JPM (siyo CCM). Kwa hiyo Chama kina kazi ya kuwarudisha hao, na wakati huo huo, kuhamasisha wanachama wapya. Kama uongozi hautatambua ukweli huo Chama kitaendelea kupoteza wanachama; wa-zamani na wapya.

Chama kinaweza kujikuta, katika muda mfupi ujao, kinachukua nafasi ya CCM ya enzi za JK, wakati JPM anachukua nafasi ya Chadema ya enzi za Slaa.

Kuna njia moja ya kuandaa na kutekeleza mkakati mpya; uongozi wa Chama unapaswa kutambua kuwa sasa umefikia turning point. Kwamba one way drive/linear political strategy is no longer working for Chadema. Groom/recruit new energetic youthful party leadership (kama mlivyofanya kwa Daktari Mashinji) then take back seats. Waachie viongozi wapya waendeshe upande wa pili wa parabola ya Chama (y= ax2 +bx +c).

Tafakari
kamanda nakuunga mkono na mawazo mazuri sana. tatizo viongozi waliopo sio serious na mambo ya nchi. ukiwaona kwa nje utadhani hapo Tanzania itabadilika lakini cheki the inside part. utashangaa. sera za kupiga pesa tu. na mbaya zaidi chama kimepokea kundi la watuhumiwa wa ufisadi na kikaamua kuwasafisha. wakati wamekuwa wakiwasema hadharani miaka yote kuwa wameifisadi nchi hii. hivi unategemea nini kutoka hapo. ni lazima kwanza chama kijitumbue majipu ili kirudishe imani kwa wananchi kama kilivyokuwa enzi ya Dr Slaa. zama zile za ukweli na ajenda za ufisadi. sasa hivi usitegemee mwenye sera ya kusafisha mafisadi akamnyooshea mwingine eti fisadi. ni kichekesho.
 
Ondoka ondoka msaliti mkubwa..Chama hichi ni chetu hatuhitaji ushauri wa mtu..

Peoooplesssss poweeeer
 
Ngoja tumalize kunywa Mbege na viroba utatutambua wewe msaliti wa mabadiliko.
 
Sasa hivi wamegeuka kuwa watetezi wa mafisadi,eti wapewe muda wa kujitetea.Vijana wengi wamerudi CCM
 
Nyie washauri wazuri, kishaurini zaidi chama kinachotawala. Hiki ndicho chenye maslahi zaidi na maisha yetu. You are wasting too much of your time on CDM.
 
Mimi nahangaika zaidi na CCM. Hawa ndio wanaochukua kodi toka kwangu kila mwezi. Kwa nn kuhangaika na CDM? Naomba wanaohangaika na CDM kwenye mitandao kutwa nzima watwambie pia sababu zaoi za kufanya hivyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom