Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Hakuna anayepinga Dr. Slaa ni nguzo muhimu kwa CHADEMA, amefanya kazi kubwa sana hadi amekifikisha chama kilipo sasa, ambapo ndipo Lowassa alipokikuta na kuchagua kujiunga nacho badala ya vyama vingine.
Na pia, hakuna anaepinga kwamba Lowassa ni kete muhimu kwa CHADEMA kupiga hatua kubwa kutoka ilipo sasa, na huenda hata kuipa historia ya kushika serikali.
Kwa hiyo jambo la kwanza ni kwa CHADEMA kukubali kwamba wote Dr. Slaa na Lowassa ni watu muhimu sana katika kipindi hiki muhimu cha mabadiliko ya sura ya siasa Tanzania.
Hivyo basi, ili CHADEMA lazima iwe na suluhisho linalokubalika kwa Dr Slaa na Lowassa, linalowaenzi wote wawili, na huu hapa ni ushauri wangu;
Mwacheni Lowassa agombee uraisi, na Dr. Slaa ampe support yote. Ila sasa, Lowassa akifanikiwa kushinda uraisi, basi aongoze Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano tu. Hiyo inatosha kama heshima ya kuiweka CHADEMA katika kilele kipya cha siasa Tanzania.
Baada ya miaka mitano, Lowassa apumzike na kujiunga na Mtei kuwa walezi wa CHADEMA. Hapo ndipo Dr. Slaa ateuliwe kuwa mgombea mpya wa uraisi wa CHADEMA ifikapo 2020.
Ila CHADEMA wanapaswa kuwa waangalifu na suala la UKAWA. Inawezekana kabisa washiriki wengine wa UKAWA wakadai kwamba ifikapo 2020 itakuwa zamu yao kutoa mgombea uraisi. Hili litaleta vurugu, na dawa yake ni vyama vinaounda UKAWA kuungana rasmi na kuwa chama kimoja chenye nguvu.