Ushauri wa bure kwa Shonza!

Ushauri wa bure kwa Shonza!

Patriote

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Posts
1,718
Reaction score
1,047
Habari yako

Nimejitolea kukupa ushauri wa bure baada ya kuona unazidi kujipaka matope!!Inawezekana hujui unachokifanya kwa sababu ya ushamba wako wa kisiasa, ila watu waliobobea kwenye siasa wanashauri uongee sana ila ukumbuke kubakisha na ya kuongea kesho.Nimekuwa nikufwatilia maandiko yako mengi sana toka wakati ule mmeanza kutoboa jahazi tulilopanda hadi sasa tulipoamua kuwatosa. Kwa tabia mnazozi onyesha, mtu mwenye akili timamu hawezi kushangaa kwanini mmemiminwa na CDM. Tena tunashangaa tuliwezaje kukupa uongozi mtu wa aina yako, hili linatukumbusha kuwa makini huko mbeleni ili tusijetukakabidhi uongozi watu wendawazimu.Kimsingi wengi tunaona chama chetu kilikuwa hatarini kwa kuongozwa na mtu wa aina yako na tunaushukuru uongozi kwa kukubaini mapema na kukutimulia mbali.

Haya unayoyafanya leo kwa CDM, unawezadhan yana kujenga huko CCM ila watu wenye busara hukohuko ulipo, wanaona NGETWA imehamiaCCM, wanaona hujakomaa kisiasa kwa hiyo tabia yako ya kuropokaropoka na hivyo hutoaminiwa huko CCM pia. Ndugu yangu unapoacha mke au mume si busara kupita kila kona nakuelezea yale ya ndani maana wakisikia wengine watakukimbia kuwa ukija achananao pia ndicho utachokifanya, basically you ruin your ownpolitical future. Siasa yahitaji uvumilivu, siasa inahitajiukomavu wa kifikra na wa kimaono.

CCM inakufurahia leo hii wewe kwao ni mpya nawanadhan kwa kuwa nawe wataibomoa CDM, hilo halipo na wengi tu ndani ya CCM wanaamini kuwa hutowezesha lolote katika kuizamisha CDM (you are just sisimizi as previously said) na wala porojo zako huzitowezesha lolote katika kuiinua CCM kulingana na hali ilivyo sasa.Porojo zako zitakapopoteza mvuto, utarudi kwenye shughuli za kawaida za chamachako kipya CCM na watarecall back tabia yako na kukuona you are unreliable and untrustworthy person. Siasa haichezwi hivyo ndugu, wewe sio wa kwanza kutimuliwa. Angalia wenzako wakina David Kafulila, sio kuwa hawajui mapungufu ya CDM, sio kuwa hawajui kuongea na kujenga hoja kama wewe ila wenzako wameamua kubakisha ya kuongea kesho.

Leo hii Kafulila akitimuliwa NCCR anaweza piga hodi CDM na akapokelewa tena kwa mbwembwe kama mwana mpotevu. Mrema akitimuliwaTLP anaweza akapokelewa CCM kwa mbwembwe km mwana mpotevu, unadhan ni kwanini??Hawa wote hata kama wamepinga vyama walivyotoka, wao walipinga vyama vyao kama taasisi na sio personal attacks. Unapoacha kuulaumu mfumo/CDM kama chama na kukurupukia watu na kuwatukana matusi ya nguoni, mara huyu Mr Zero, Mara huyu Mvuta Bangi, Mara huyu mpora wake za watu/mzinzi. Je huko uendako nani msafi???? Nchemba?? JK?? Mzee Mkapa??Mzee Mwinyi?? Hebu fikiria wazee wa CCM wenye busara wanapokusikia unabwabwaja hivyo majukwaan na kwenye media, wewe unadhan wanafurahia na kuthamini mchango?? Watanzania wa kawaida tu hawakuelewi achilia mbali mature politicians!

Huoni kuwa hata huko wanakuona hamnazo???Unajiwekea mazingira magumu ya kucheza siasa, Siasa sio uadui. Hiv kwa unayoyafanya hata ukiwa mbunge huko CCM kweli utaweza salimiana na hawa unaowatukana matusi ya nguoni???Hii dunia tunapita tu si vyema kujitengenezea maadui bila sababu za msingi. Mimi nadhan unahaja ya kutafakari nyendo zako, sina hakika sana kama hayo uyafanyayo ni moja kati ya vigezo vya siasa safi. You are playing dirty politics and looking for cheap popularity.
 
ahachane na mambo ya kupaka mkorogo. huko CCM si wanamuona kituko Khaaa

521519_10200612899583842_2089472450_n.jpg
 
Ningeomba niongeze kidogo - tena kwa nia njema kabisa. Juliana, unayoyafanya sasa, hutaona madhara yake hadi giza liingie, na wakati huo utakuwa na limited options.

Hata kwenye sehemu za kazi, hakuna mtu atakuamini tena! Unaweza kudhani unapambana kwenye siasa, lakini hata nje ya siasa, reputation yako itakuhukumu. Haya ni makosa uliyofanya, na sielewi ni kwanini ulishindwa kuona mkakati uliopewa na 'watu' ulikuwa umejaa nuksi na mabalaa tele kwa maisha yako. Busara ndogo sana ilitosha kukuelekeza kwenye sera badala ya kutukana watu.

Kumbuka, money is not everything. Unaweza kuwa na hela sana lakini usiheshimike hata kidogo. Na hakuna kitu kibaya kwa mwanadamu kama kutoheshika. Vipande thelathin vinavyokuzungusha nchi zima kutukana watu -tena waliokuzidi umri, ni laana ya kujitakia. You made a very poor judgement, and you may well live to regret it. Kila la kheri.
 
Mnazidi kumpa huyu dada umaarufu.
Unajua tukikaa kimya anaweza akadhani watanzania wa leo tunapenda kusikia matusi ya nguoni anayoyatoa, ni vyema akajua tu kuwa vijana wa leo tunajua tunataka nini. Na yeye asijivike cheo cha kutusaidia kufanya maamuzi, we really know what we need. Hivyo asifikirie anaweza akatubadilisha kwa hoja za kijingjinga tu.

Watanzania hatujafunzwa kumheshimu mtu kwa kuwa amesoma sana au kwa kupata Division one, mtu wa aina hii si inamaana atakuja kuwacheka vijana wetu asilimia 60 waliopata zero form 4???? Au anataka kuwaambia nini waliopata Zero form 4??? Ndio siasa za CCM hizo????Nchi ipo kwenye msiba wa watu kupata zero afu yeye anajifanya mjuaji, ngoja wampopoe na mawe kwenye hayo majukwaa anayopanda na kutukana watu.

Tumefunzwa kumheshimu mtu kwa utu wake na sio mali/ elimu yake, sasa huyu anavyotuletea habari zisizo na kichwa wala miguu inapaswa tumpe elimu, after all akumbuke kuwa yeye ni mwanasiasa kijana anayecheza/atakayecheza siasa na karne hii sio siasa za kizamani za majitaka. Mimi nadhan ni bora angetumia muda huu kujua Katiba, Sera na Ilani ya chama chake kipya badala ya kutufundisha matusi.
 
Mkuu in battle you have limited resources. It is wise to pick your targets wisely. Mnalenga makombora kwa mtu ambae hana cheo ndani ya chama wala influence kwenye chama wala jamii. Sababu pekee tunaendelea kumsikia ni kwa sababu watu bado wanajisumbua kumuongelea. Ni sawa sawa na nzi anaekusumbua, jinsi unavyo hangaika nae ndiyo anazidi kurudi na ndivyo unavyo zidi kujipiga makofi. Ni mtazamo wangu tu...
 
please can we stop talking about her??

ok, watu wamwache, lakini aliyoambiwa leo hapa yanatosha kama ni sikio la kufa basi tunajua huwa halisikii dawa. halafu sio juliana peke yake hata hao wanaomfurahia kuwa anawapasha cdm nao wako kama yeye, shame on them, ukimtuma au kumfundisha mwanao kutukana watu, ni sawa kuwa na wewe pia umetukana
 
ni ujuha kumdhamini, azunguke nchi nzima kwa fedha za walipa kodi ili kutoa matusi kwa mpinzani wako, only juhaa can do it.
 
Ningeomba niongeze kidogo - tena kwa nia njema kabisa. Juliana, unayoyafanya sasa, hutaona madhara yake hadi giza liingie, na wakati huo utakuwa na limited options.

Hata kwenye sehemu za kazi, hakuna mtu atakuamini tena! Unaweza kudhani unapambana kwenye siasa, lakini hata nje ya siasa, reputation yako itakuhukumu. Haya ni makosa uliyofanya, na sielewi ni kwanini ulishindwa kuona mkakati uliopewa na 'watu' ulikuwa umejaa nuksi na mabalaa tele kwa maisha yako. Busara ndogo sana ilitosha kukuelekeza kwenye sera badala ya kutukana watu.

Kumbuka, money is not everything. Unaweza kuwa na hela sana lakini usiheshimike hata kidogo. Na hakuna kitu kibaya kwa mwanadamu kama kutoheshika. Vipande thelathin vinavyokuzungusha nchi zima kutukana watu -tena waliokuzidi umri, ni laana ya kujitakia. You made a very poor judgement, and you may well live to regret it. Kila la kheri.

leo ndiyo nimeamini kuwa juliana ameishika chdm pabaya. hahahahha! juliana anapigiwa magoti kwa kisingizio cha ushauri! bi juliana nakushauri ufanye kile unacho amii kina maslahi kwako na kwa taifa lako. kama unaona chdm ni uhuni mtupu chini ya kivuli cha demokrasia, huna haja ya kuwaonea aibu. pasua yote uliyonayo ili watu waelelwe upande wa pili wa shilingi
 
Huoni kuwa hata huko wanakuona hamnazo???Unajiwekea mazingira magumu ya kucheza siasa, Siasa sio uadui. Hiv kwa unayoyafanya hata ukiwa mbunge huko CCM kweli utaweza salimiana na hawa unaowatukana matusi ya nguoni???Hii dunia tunapita tu si vyema kujitengenezea maadui bila sababu za msingi. Mimi nadhan unahaja ya kutafakari nyendo zako, sina hakika sana kama hayo uyafanyayo ni moja kati ya vigezo vya siasa safi. You are playing dirty politics and looking for cheap popularity.ALWAYS TWO FOOLS COLLIDE.
 
Technically umecommit plagiarism/copy right offence, jenga utaratibu wa kurecognize source pale unapotumia ideas/maneno/maandishi ya watu. Huu ni utaratibu ambao jumuiya ya wasomi na nchi mbalimbali zimekubaliana kuutumia. Ni only really fools wasioona mantiki ya huu ushauri kwenye ulingo wa siasa za karne hii.
 
Mtoa hoja kama Binti ni wakusikia atakuwa amekuelewa.Tena siyo hayo tu naomba niongeze sentensi moja au mbili.
Juliana Shonza siyo tu anajidhalilisha yeye mwenyewe bali jumuia ya wanawake.Ametudhalilisha sana wanawake,wakati huu tunapohitaji kupewa nafasi halfu mwenzetu amekaa juu ya jukwaa anatukana mwanamke mwenzake ambaye siyo tu ni mwanamke bali ni kiongozi aliyechaguliwa na watu,kwa maana hiyo amewatukana hata wale waliomchagua kiongozi huyo.

Namuomba iwe imetosha tumechoka na historia za watu.
 
Shonza hajiuliza hata sisi tunaotukana watu huku jf kila siku kwa ninitunatumia majina bandia?
 
Back
Top Bottom