Ushauri wa bure kwa Shonza!

Ushauri wa bure kwa Shonza!

Haloo halooo!
Mnalo, mtajuta kumfahamu Shonza
Na mtoto wa kike anamwaga razi watu wanapagawa!
Si mlimfukuza?
Ukitaka tusicomment mwandikie barua binafsi au PM.

Kunyweni juisi ya pilipili kukoleza koo!
Mtu wa hiv ukim-PM anaweza sema unamtaka kimapenzi, hivi we huoni kuwa matendo ya mtu huyu ni ya hatari!
 
Muonekano ktk picha ni kama zombie au vampire. JF mna vituko?!!
 
Huku mwanza tunamjua Juliana wa Uganda ambaye ni mwanamuziki, lakini huyo wa matusi namsoma JF tu wala sijawahi mwona akifanya jambo lolote la kumwekea kumbukumbu chanya hata alipokuwa CHADEMA,sasa kama siasa zake ni matusi tu hapo anadidimiza nafasi ya mwanamke katika jamii.Maana hata dini zinamtaka mwanamke ajiheshimu na kujisitiri kitu ambacho hata Mhe.Rais Kikwete anakiamini na kama amewaachia mabinti wa kukichafua chama kinyume na kina Bibi Titi Mohamed basi mwishowe tutajua nani ameteleza.Naomba kujuzwa kama CCM wako wengi kama Juliana au ni yeye tu na kwa nini?
 
Ushauri mzuri ni vyema aufanyie kazi kwa faida ya maisha yake.!
 
Mkimaliza kumjadili huyu MJINGA, let me know please.... I will be right back...
 
Atawamaliza nyie mnayekwenda naye peku peku.

Yote kwa yote,Juliana wacha aendelee kuzungumza,kwa kuwa ni mwanasiasa lakini anachokosea,kwanza kabisa anaihalifu hata sheria za nchi,unapozungumzia mambo binafsi ya watu,mfano aliwahi kuzungumza huko goba akiwa na NAPE,na MAGEMBE kwamba Dr.Slaa anaugonjwa wa kisukari na pressure.mambo kama haya it is beyond ethics kuzungumza ugonjwa wa mtu hadharani,hili ni kweli ni laana.pili hakuna uhusiano wa ugonjwa wa slaa au form 4,ya mbowe au form 6 ya myika na maendeleo wanayoyataka wananchi,kama maji,barabara n.k
 
Sisimizi anapewaga ushauri hahahaha muacheni bi dada aendelee kufumbua macho watanzania.....na unampa ushauri ili iweje wewe anakuhusu nn? tutolee UMBULULA HAPA
 
Nape tumesha zoea UROPOKAJI wako ulisema CDM ita sambaratika muda mfupi,mpaka sasa bado unaROPOKA tu CDM inazidi kukata mbuga.HEBU tuambia muda maalum wa tukio hilo.hatutaki ujinga-ujinga wako huu wa kila siku.
 
Copyright kabisa
juliana wa ccm ninae mjua ni huyu hapo chini. huyo wa kwako hapo juu sijawahi muona
th
th
 
Sisimizi anapewaga ushauri hahahaha muacheni bi dada aendelee kufumbua macho watanzania.....na unampa ushauri ili iweje wewe anakuhusu nn? tutolee UMBULULA HAPA
Taratibu kijana, wewe huna sifa ya kuniita mimi Mbulula.
 
Namuomba akawaulize watu hawa Ndg Masumbuko Lamwai na Ngawaiya na wangine wengi ,leo hii wewe ni kama muwa midomoni mwa CCM utakapo isha utamu utatemwa na kuwa makapi nakutupwa jalalani kazi kwako Binti
 
Ukitaka kumsema kama hivi usiweke hadharani, Shonza hakosi watetezi humu jamvini.
Lengo langu sio kumsema, ila ni kumpa political advice. Inaonekana anapenda siasa na angependa career yake iwe in politics, ila kwa uchezaji wa style hii hakika atatolewa, mana anahatarisha pia afya za wachezaji wengine. Sasa hiv anafanya hata wanawake wenzake wafikiriwe mara mbili mbili kuwapa/kuwachagua katika uongoz wa juu.
 
Lengo langu sio kumsema, ila ni kumpa political advice. Inaonekana anapenda siasa na angependa career yake iwe in politics, ila kwa uchezaji wa style hii hakika atatolewa, mana anahatarisha pia afya za wachezaji wengine. Sasa hiv anafanya hata wanawake wenzake wafikiriwe mara mbili mbili kuwapa/kuwachagua katika uongoz wa juu.
Mkuu unachoandika si ukweli.
Mtu mmemfukuza chama
Bado mnamsakama
Mnamtakia nini?
Kama hamumpendi si mumwachie afanye vitu vyake?
 
Frankly speaking nilikuwa nimejitenga na uchangiaji wa hoja za vyama lakini kwa hoja hii nalazimika. Pamoja na mleta bandiko kuonesha kuwa pro CDM lakini ushauri huu kwa Bi. Shonza umekuja ukiwa haujachelewa sana. Nionavyo mimi tangu amefukuzwa uanachama wa BAVICHA amewekeza muda mwingi kwenye hasira na visasi ambavyo naamini kabisa kwanza si hulka ya mwanasiasa makini lakini pia anafanya kazi ya kurudia vitu vilevile ambavyo vimeimbwa muda mrefu na aliowakuta CCM na havijaweza kubadili au kuua nguvu ya CDM.

Strategically, siasa ni timing na mara nyingi inahitaji kuwa na moyo wa chuma na wenye uvumilivu sana. Binafsi nilitegemea Shonza baada ya kukutwa na fagio la BAVICHA angewekeza nguvu zake katika kusaka political strategies za kurudi ulingoni lakini option aliyochukua ya kuacha kabisa itikadi aliyokuwa akiitetea na kukimbilia kwenye itikadi tofauti kabisa tena isiyokaribiana na aliyoiacha ni ishara ya political suicide.

Yawezekana baada ya kupima tuhuma zake aliona hana jinsi ya kupambana tena ndani ya CDM lakini njia anazopitia sasa hivi za kuwekeza mtaji wake wa kisiasa kwenye matusi, visasi na hasira dhidi ya viongozi wa chama alichokiacha hakika hazimsaidii sana. Ni bora mifano ya akina Kaborou, Lamwai, Tambwe na wenzake ikawa mifano kwake. Hawajawahi kusikika wakishambulia mtu mmoja mmoja bali mifumo ya vyama walivyoviacha.

My advice to Shonza jikite katika udhaifu wa kimfumo na kimuundo ndani ya CHADEMA dhidi ya ubora wa CCM. Lakini pia kama una taarifa za matumizi mabaya ya madara ya viongozi wa CDM lakini si katika personal attacks maana zinakosa mantiki hata kwa mtu wa kawaida tu ambaye hajaingia darasani.

You just think at your age na hali halisi ya jamii yetu ilivyo mtu akukute jukwaani unamtukana Mbowe au Slaa matusi ya nguoni au familia yake, utaonekanaje? Ni mambo madogo ambayo wanasiasa wengi wamekuwa wakiyapa mkazo lakini kwa jamii ni out of touch na yanashusha hadhi kabisa.
 
[QUOTE=Patriote;580956 msamehe bure majibu keshayapata anakoita kwao kwenye ziara ya mboe mbeya
 
maccm yanajua ya kuwa wewe shonza kama siku ukitoka ccm utakuwa hivyo hivyo maana unapojaribu kuua kwa upanga na wewe utakufa kwa njia hiyo hiyo.
 
Bandiko hili na liwe wosia kwa muhusika na wengine wengi wenye mitazamo na akili za aina yake.
Tukidhamiria kulipa tafsiri pana suala husika,hatutaacha kuelekeza lawama zetu kwa wale wote wanaochukuliwa kama watawala ndani ya taasisi ya kisiasa,CCM.
Kwa vigezo vyote,hii si CCM iliyokuwa ikihimiza dhana za,heshima na usawa wa kibinadamu,chini ya imani kuwa ''Binadamu wote ni ndugu zangu'' wala si ile iliyopata kuamini ''fitina kwangu mwiko''.
Ya sasa ni CCM isiyoona umuhimu wa kuheshimiana wala kuishi kindugu na kwa hakika haioni uwezekano wa kufanya siasa pasipo kuwekeza katika fitina,uzushi, uongo na upuuzi.
Nikiisha kuekeza lawama zangu dhidi CCM kama taasisi ya kisiasa,muhusika anawajibika,kulingana na maneno na matendo yake,kubeba lawama.Ajiulize:kwa nini,iwe ni yeye na mwenzake mmoja-ambaye naye inaonyesha amebobea katika upuuzi usiomithilika-wamekasimiwa jukumu la kutamtaka maneno yasiyo na staha dhidi ya watu wanoheshimika katika jamii badala ya kueneza sera,itikadi falsafa za chama chao?Ni imani yangu kwamba wahusika wamekabidhiwa kazi hiyo baada ya kukidhi kipimo cha siasa za sasa CCM,zinazojiegemeza katika umahiri katika kubuni na kusambaza matusi badala ya hoja.
Kimantiki,kwa hulka,mtu mpuuzi hutenda upuuzi.Hatari moja ni kuwa ni kazi inayochosha mno kumsihi mpuuzi aachane na upuuzi.Bila kutenda upuuzi muhusika mara moja anapoteza sifa ya kuitwa mpuuzi.Kwa mienendo ya baadhi yetu,upuuzi ni sifa adhimu inayokumbatiwa ,kung'ang'aniwa na kutamaniwa.Kinachoogopesha zaidi ni kuwa,kwa sasa ,upuuzi ni ajira inayolipa na walipaji hawako tayari kukatisha ajira za wapuuzi maana,kwanza jamii ya wapuuzi haiishi na pili uwekezaji katika upuuzi unawahakikishia matokeo fulani hata kama ni ya kipuuzi.
 
Back
Top Bottom