Ushauri wa bure kwa Rais Magufuli kuhusu Air Tanzania

Masopakyindi......kumbukumbu zako ni sahihi lakini zinapandana.....Nijuavyo wakati wa MMASI hatukuwahi kuwa na ndege nyingi hivyo.Bw Yule ie MMASI unakumbukua sakata lake na George Hallack kuhusu kile dege lililogeuka mzinga wa nyuki pale KIA
Kweli mkuu, inaweza kuwa kumbukumbu si makini sana ila ni kweli.
George Hallack aliwaingiza mjini hao jamaa wa ATC, lile lidege lilikuwa uozo, halikuruka hata safari moja.
Ufiasdi ulianza zamani sana!
 
Huo ushauri unatakiwa wapewe ATCL wenyewe. Magufuli keshamaliza yake amewakabidhi ndege na anawaongezea nyingine. Washindwe wao tu sasa.
Kweli mkuu,
ATC kazi wanayo ila kwa kuanzia wangeiga kama Emirates kuingiza foreign management yenye ujuzi wa fani ya kuongoza mashirika ya ndege.
 
Kweli mkuu,
ATC kazi wanayo ila kwa kuanzia wangeiga kama Emirates kuingiza foreign management yenye ujuzi wa fani ya kuongoza mashirika ya ndege.
Ni kweli maana wakitegemea Magufuli awafanyie kila kitu wakati kwenye uzinduzi aliongelea mambo mengi wataanguka...ni Sasa na issue ya machinga hapa Mwanza. Wakati ule Magufuli amekuja ziarani alisema wazi kuwa wamachinga wasiondolewe mpaka maeneo rafiki kwa shughuli zao yapatikane kwa maelewano baina ya Jiji/uongozi wa mkoa na wamachinga. Viongozinwa mkoa/jiji sijui waliamuaje kuwaondoa wakati zuio la Magufuli lilikuwa bado hai. Ni kukosa ubunifu wakati maelekezo alishawapatia
 
Mkuu hukupaswa kusema hivyo. Je ulimsikia kwa makini Mh. Rais jana Ikulu? Alisema kuna baadhi ya mambo watendaji hawatakiwi kuyafanya wenyewe na wamekuwa watu wa matamko tu, na kwamba wao na (samia) ndio waliozunguka nchi nzima kuomba kura hivyo lazima maamuzi flani yasitokee bila kulia kwao.
Hilo linahusianaje na ATCL?
 
Huo ni wivu wa kisiasa..ila ndio tumeshaamua..
Uamuzi uliofanywa sidhani kama ulifanyiwa study ya kitaalamu, ila ni uamuzi wa kisiasa tu, kama ni suala la watalii kuna vitu vingi muhimu, kama jinsi tunavyojitangaza ndani na nje ya nchi, pia wanatizama zaidi ya usafiri, kikubwa ni usalama na huduma inayotolewa kwao kama katika mahoteli, sehemu wanazotembelea, usafiri wa ndani nk.
 
mimi nashauri management itokw nje kabisa.. isiyojua hata jina la mwanasiasa mmoja..

ili hata akileta siasa apande bure wamgomee
ATCL ilishakuwa na management ya nje na haikutoka ndio ikaingia kaburini kabisa. Suala sio Mgt. ya nje bali professional mgt. Hii ya Mh. Waziri na Ikulu kuhusika na daily mgt. ya ATCL si njia sahihi ya kuiendesha ATCL.
 
Hili la Hangar linatia hasira pale KIA kulikuwa na Hangar sijui kina Mkapa wakampa mwanamke gani tena kwa hela ya kutupwa badala yake huyo mama akawa anatumia kwa ajili ya private jets zinazotua hapo ,anavuta sijui dola ngapi kwa Private jet moja
Sijui kama tuna Ma Engineer wangapi wa ndege ili tukitaka pia kufufua moja ya hizi Hangar tuwe na wataalamu wa kutosha ..Magufuli asikimbilie tu kununua ndege waje na plans za kufanya viwanja vyetu viwe na access ya 24/7
Arusha kule jua likizama basi ndio hamna kinacho endelea kwa sababu runway ambayo inatumika kama taxway pia haina mataa sasa hili linasubiri nini kutekelezwa ?
Najua safari ni ndefu na yote hayawezi fanikiwa overnight ila basi jitahidi kutafuta funds za ku renovate viwanja vyetu na pia kusomesha wataalamu zaidi
Kweli mkuu
 
IMG-20161207-WA0029.jpg
 
Back
Top Bottom