Elections 2015 Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo, Vunja Kambi, Jisalimishe!

Kama mgombea angekuwa ni Membe, tungependekeza mapambano yaendelee kwa Lowassa kuvuka upande wa pili, nasi tumuingize ikulu!, lakini huyu aliyepitishwa, John Pombe Magufuli, pia ni jembe la ukweli, hivyo Lowassa hata akiamua ku cross, ataishia kupata kipigo kingine, yaani double tragedy !.

Pasco

Nimeipenda hii Mkuu Pasco, Double Tragedy!
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Mimi ni miongoni mwa watu tuliomuunga mkono kwa dhati, mwamba wa Kaskazini, Edward Ngoyai Lowassa, na tukaahidi humu akiondolewa kwa mizengwe, hatuta kubali, patachimbika. Kilichotokea ni kweli Edward Lowassa aliondolewa kwa mizegwe,

hivyo Lowassa alipokatwa walishangaa, kama wangeosoma uzi huu kabla, wasinge shangaa!.
Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

Baada ya kuibuka jina John Pombe Magufuli, kuwa ndiye atakayepeperusha bendera ya CCM, kuna watu wanadhani
John Pombe Magufuli amejiibukia tuu from nowhere!, No!, Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John

Kwa vile Lowassa ndie kipenzi cha watu, na wengi waliitegemea CCM itimize mapenzi ya watu, lakini CCM wakaamua kutanguliza mbele maslahi mapana zaidi ya taifa, kwa kuwaweka pembeni 'the giants', wengi wa wafuasi wa Lowassa wamekuwa taken by surprise na wengine hata ku despaire, lakini laiti wangeusoma uzi huu,
Edward Lowassa sio lazima yeye tuu ndiye awe Rais wetu wasingekuwa surprized!.

Maadam sasa uchaguzi wa CCM umemalizika, na mgombea wa CCM ni Dr. John Pombe Magufuli, natoa wito na ushauri wa bure kwa Mhe.
Edward Lowassa, ayakubali matokeo, avunje kambi yake au ile team yake, ayarudishe nyumbani majeshi yake na kujisalimisha rasmi kwenye chama kwa kumsupport mgombea rasmi wa CCM!.

Kama mgombea angekuwa ni Membe, tungependekeza mapambano yaendelee kwa Lowassa kuvuka upande wa pili, nasi tumuingize ikulu!, lakini huyu aliyepitishwa, John Pombe Magufuli, pia ni jembe la ukweli, hivyo Lowassa hata akiamua ku cross, atai
saidia kambi ya upinzani kuongeza nguvu na kupata wabunge wengi, lakini yeye kama yeye ataishia kupata kipigo kingine, yaani double tragedy !.

Kwa vile Lowassa ni chaguo la watu, na ni sisi watu tulio mchagiza kuwa 2015, ikulu ni yake, kwa ahadi hata asiposimamishwa na CCM, then asimame nje ya CCM tumpeleke ikulu, lakini kwa vile aliepita ni Magufuli, ambaye na yeye ni jembe la ukweli, hakuna tena sababu kwa Lowassa kuendeleza mapambano maana huu sasa utakuwa ni mpambano wa mafahali, ziumiazo zitakuwa ni nyika!.

Pasco

Nafanya tuu tafakuri!.
P.
 
Hata kama angeshinda Membe,Lowasa asingehama chama. Kwanza,kulinda maslahi yake,maana CCM ni chama cha wafanyabiashara. Pili,kulinda historia yake ndani ya chama. Tatu,historia yake, anaijua kama ni mbaya ama nzuri. Nne,kuandamwa na vyombo vya dola mara tu atakapokuwa nje ya mfumo wa chama. Hawezi kamwe. Wachafu hawawezi kuhama ccm,makongoro alisema chama kimejaa vibaka alimaanisha.

Wasafi washahama hivyo wamebaki wachafu & Co.
 
Mwanahalisi pia walishasema
 
Attachments

  • 1445587269623.jpg
    1445587269623.jpg
    20.8 KB · Views: 220
Mwanahalisi pia walishasema

Tume imesitisha na kuwasimamisha wote waliokuwa wanaandaa karatasi za majumuisho ya matokeo ya upigaji kura. Inavyoonekana ni katika mikakati ya bao la mkono. Tume kwa sasa wengi hawaelewani kutokana na baadhi ya wakubwa kufanya mambo waliyoelekezwa na MaCCM tofauti na ilivyokuwa mwanzo na bila kufuata utaratibu wa Tume. Hawa wasimamizi wa Tume waliokuwa wanatakiwa wakasimamie upigaji kura wamesimamishwa na kuzuiwa kwenda kwenye vituo vya kupigia kura licha ya kupewa mafunzo ya siku mbili juu ya usimamizi wa kura. Sababu ya kusimamishwa kwao ni kutokana na wengi wao kuuliza inakuwaje unapoingiza matokeo ya waliopiga kura, kwenye system inatoa idadi tofauti??? Hamwoni kuwa mtatuletea matatizo tutakapokuwa vituoni??

Hawa wafanyakazi wa Tume wanadai malipo yao ya mishahara ya miezi mitatu mpaka sasa hawajalipwa na wamesimamishwa mpaka January 2016 bila kujua watalipwaje pesa zao. Kumbuka tume ilivyopewa mabilioni lakini wameshindwa kuwalipa hata hawa wafanyakazi wao. Wanafanya kazi katika mazingira magumu huku viongozi wao wakijilipa maposho kibao na wengine kuhama kwenye nyumba zao na kuishi mahotelini eti kwa kazi maalum. Mfano:- Waliopiga kura ni 100, Kinachotakiwa ukiingiza namba isomeke 100. Tofauti yake inasomeka 150,160, 200 na kuendelea.

Hivyo System inakuwa tofauti na namba ya uliyempigia kura. Yani inakuwa tofauti na makaratasi anayojaza mawakala. Karatasi inasema vingine na kwenye computer inasema vingine. Mfano kwenye ubao wa matangazo inaonyesha waliompigia Lowassa ni 50, Magufuli 45. Kwenye system ya Tume itaonyesha Lowassa 50, Magufuli 150. Wakaweka kuwa kila msimamizi wa Tume kwenye kituo cha kupigia kura atakuwa "Administrator"na anao uwezo wa kubadilisha kama kuna makosa kama hayo. Kitu ambacho hakiwezekani na haijawahi kutokea.

Huwezi kuruhusu kila moja kuwa na uwezo wa kuingilia system. Hii system ya Tume haitawezekana kwa sababu nijuavyo nchi yangu hatuna huduma za Internet nchi nzima watarudia kuhesabu kura kama kawaida. Ndio kisa cha kuagiza kuwa watu wasikae umbali wa mita 200. Kwa sababu wataona matokeo na kuwasiliana na wenzao kabla Tume hawajafanya yao.-Ndio maana yameingizwa magari 777 kwa kitu cha siku moja. Wapinzani wamefanya kampeni zao kwa amani bila matusi wala kumwaga damu. Jiulize fujo zitatoka wapi kama sio maCCM na Polisi wao ndio watakaoanzisha.

Kikwete hajiulize tangu alivyoingia madarakani 2005 watu walikaa mita 200 na mwaka 2010 ilikuwa hivyo hivyo. Jiulize iweje leo anaficha nini?? Anaficha siri ya Ritchmond, Escrow, Mikataba na wachina na wale wafanyabiashara wa Kihemen. Sheria inasema kuwa kaa mita 200 kusubiri matokeo. Na ni uamuzi wako kusubiri matokeo au kuondoka. Jiulize kwani wakati wa kuangalia matokeo vituoni utakuja peke yako na hata kama utakuja peke yako si mtakutana na wengine hata zaidi ya 100 wanaotaka pia kujua matokeo/kuona matokeo.-Mtashangilia wapi baada ya matokeo, uchaguzi unafanyika siku moja na watu kupata matokeo baada ya muda wa kumaliza kupiga kura.

NINACHOWASHAURI WAPINZANI MSIKUBALI MATOKEO, KATAENI ILI KURA IRUDIWE KUHESABIWA UPYA KUTOKA KWENYE KARATASI HALISI ZA VITUO ILIPOPIGIWA KURA.

Uchaguzi huu utakuwa siyo huru na haki na wengi watakufa yani watauwawa na Polisi CCM kwa kulinda utawala wao. Wananchi hawatakubali haki yao kuporwa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Mnafiki mwenyekiti Hewa
 
Attachments

  • 1445589263512.jpg
    1445589263512.jpg
    34.5 KB · Views: 177
Huwa sikusomi uko upande upi sababu uwa unang'ata na kupuliza,nahis wewe Si mwanachama wa chama chochote unasomaga upepo tu

@pasco haangalii Upepo yeye anachoangalia ni maslahi.Yaani yupo tayari Hata kuiuza hata nchi yake ilmradi tu apate maslahi kiduchu
 
Kuongoza watanzania ni sawa na kuongoza kundi la kondoo haijalishi ni wasomi au laa.
Pasco wewe ni mnufaika na huu utawala wa CCM kwa njia unazozijua mwenyewe.

Mkuu Pasco anacheza na ''kuwa mwanasiasa nje ya mfumo wa CCM nini''. Hapo ndipo utakapojua kweli Dr Slaa, Lipumba and co ni alfa na Omega. Lowassa hana guts za kutoka CCM hata kidogo. Hana lolote la kujivunia na hana ushawishi wa aina yoyote. Waliweza kum-black mail Mkapa ile 2005 akafikiria na hapa ataweza.

Nalipa heshima ya hali ya juu bandiko lako hili Pasco, uliloliandika kwa hekima na busara kubwa kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa letu.

Hata hivyo naona niongezee kidogo kwa kumkumbusha EL ule msemo wa busara sana unaosema asiyekubali kushindwa sio mshindani.

Kwa hiyo ni vyema akabwaga 'silaha' chini na kukubali yaishe.

System imemchagua mtu wake.....tumpeni tu space now afanye kazi

Mshauri kwanza arudishe vijana zaidi ya 4,000 aliotelekeza Dodoma,haya mengine badae,kuna watu wametelekezwa jamani

Mkuu mimi kwa mapenzi yangu kwa upinzani na Mabadiriko ya Ukweli, ninaomba usiku na mchana jamaa avuke upande wa pili wa barabara. Gepu lake atakalotokanalo kule ni msaada mkubwa wa Upinzani. Si kwamba Upinzani hatuna kura za kutosha, hapana!, Tunataka kura za ccm zigawanyike ili kura zetu zibaki imara.

Nikija upande wa pili, sioni ni namna gani Magufuli anaweza kufanya kazi na Lowassa. Magufuli ni mtu kaksi sana, haingiliki kirahisi. Itamuwia ngumu sana Mwamba wa kaskaz "Kutekeleza" mambo yake chini ya huyu jamaa, hapa pia tukumbuke, Nyuma ya Mwamba wa kaskaz kuna grupu la watu ambao wana makandokando yasiyoeleweka, machafu yasiyomithirika!. Hawa kamwe hawawezi kumshawishi mtu kama Magufuli kutekeleza mambo yao.!!!

So naona njia moja tu ambayo Team Lowassa wanayo ni ku-cross the way, waende upande wa pili Wakamwage Mboga.!! Bado mambo ya Richmond yako vichwani mwa watu, waitumie kete hiyo ili wakose wote..!!! Lowassa ni Mwanaume wa shoka, alianza kuutafuta Urais tangu enzi za Baba wa Taifa, ktk kinyang'anyiro cha mwaka 2005 walikubaliana na jamaa yake ambaye hawakukutana barabarani kwamba, atangulie yeye, mwaka 2015 ni zamu yake Mwamba wa kaskaz...lakini ndo hivyo mwenzie kamsaliti waziwazi.!! Naye akae kimyaaa..!!!

Kama Lowas hakuiogopa ccm ya Nyerere iweje aigope ccm hii chovu ya Kikwete..? Nitamshangaa sana.!!

BACK TANGANYIKA

Kweli kabisa, wameangukia pua sasa wanajifanya kujipendekeza kwa Magufuli. Hawa jamaa (Team Lowassa) hawana hata chembe ya aibu. Si, ndio hawa hawa walikuwa wanasema watu wasimame "wahesabiwe" ndio hawa hawa walikuwa wanasema "hakuna mtu anayeweza kuzuia mafuriko kwa mkono"?? Hayo mafuriko yako wapi?? Jamaa yao hata tano bora hakutokea, mafuriko gani sasa??? Nawapa pole sana!

Waungwana hebu kila mmoja afanye "correction" kabla ya J2 ili tuingie ktk Uchaguzi kumbukumbu zikiwa sawa.
 
Last edited by a moderator:
Waungwana hebu kila mmoja afanye "correction" kabla ya J2 ili tuingie ktk Uchaguzi kumbukumbu zikiwa sawa.

Mimi nimepiga kura na siogopi kusema nimemchagua Dk Magufuli kuwa Rais mpya. Naomba msikimbie humu JF hasa kuanzia kesho matokeo yatakapoanza kutangazwa.
 
Pasco Nakukubari wewe ni great thinker na mara nyingi una habari za uvunguni kabisa, kwa sheria ni kwamba Rais ni makomeo binafsi nashauri kwa vile hata wewe unajua kabisa kilichoendelea(goli la.....)kitu muhimu ni Kuendeleza mapambano ya kudai sheria mpya ya uchaguzi na katiba bora kwa Watanzania.Zile sheria za kuwa hakuna kupinga mahakamani,Uvamizi wa Tallying,na figisu nyingine nyingi zifanyiwe marekebisho ili Rais akichaguliwa kusiwe na malalamiko yoyote hapo itakuwa vema..
 
Back
Top Bottom