Elections 2015 Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo, Vunja Kambi, Jisalimishe!

wanabodi,

mimi ni miongoni mwa watu tuliomuunga mkono kwa dhati, mwamba wa kaskazini, edward ngoyai lowassa, na tukaahidi humu akiondolewa kwa mizengwe, hatuta kubali, patachimbika. Kilichotokea ni kweli edward lowassa aliondolewa kwa mizegwe. Kuna watu humu hawakuuona uzi huu,
licha ya kukubalika, jina la lowassa halitafika hata cc!

hivyo lowassa alipokatwa walishangaa, kama wangeosoma uzi huu kabla, wasinge shangaa!.

Baada ya kuibuka jina john pombe magufuli, kuwa ndiye atakayepeperusha bendera ya ccm, kuna watu wanadhani amejiibukia tuu from nowhere!, no!. Na kuna wanadhani ameibuka surprisingly!, no!. Kama wangeusoma uzi huu,
mgombea wa urais kwa tiketi ya ccm, 2015 "could be" john

angalau wangeelewa ni magufuli!.

Kwa vile lowassa ndie kipenzi cha watu, na wengi waliitegemea ccm itimize mapenzi ya watu, lakini ccm wakaamua kutanguliza mbele maslahi mapana zaidi ya taifa, kwa kuwaweke pembeni 'the giants', wengi wa wafuasi wa lowassa wamekuwa take by surprise na wengine hata kuwa despaired, lakini laiti wangeusoma uzi huu,
edward lowassa sio lazima yeye tuu ndiye awe rais wetu

wasingekuwa surprized!.

Maadam sasa uchaguzi wa ccm umemalizika, na mgombea wa ccm ni dr. John pombe magufuli, natoa wito na ushauri wa bure kwa mhe. Lowassa, ayakubali matokeo, avunje kambi yake au ile team yake, ayarudishe nyumba majeshi yake na kujisalimisha rasmi kwenye chama kwa kumsupport mgombea rasmi wa ccm!.

Kama mgombea angekuwa ni membe, tungependekeza mapambano yaendelee kwa lowassa kuvuka upande wa pili, nasi tumuingize ikulu!, lakini huyu aliyepitishwa, john pombe magufuli, pia ni jembe la ukweli, hivyo lowassa hata akiamua ku cross, ataishia kupata kipigo kingine, yaani double tragedy !.

Kwa vile lowassa ni chaguo la watu, na ni sisi watu tulio mchagiza kuwa 2015, ikulu ni yake, kwa ahadi hata asiposimamishwa na ccm, then asimame nje ya ccm tumpeleke ikulu, lakini kwa vile alipita ni magufuli, ambaye na yeye ni jembe la ukweli, hakuna tena sababu kwa lowassa kuendeleza mapambano maana huu sasa utakuwa ni mpambano wa mafahali, ziumiazo zitakuwa ni nyika!.

Lowassa tulikupenda, ila ccm imempenda zaidi magufuli, teremsha silaha chini, kubali kushindwa, rudisha nyuma majeshi, jisalimishe!.

Nb: Hii sio mara ya kwanza kwa mimi kutoa ushauri wa bure kwa lowassa, huko nyuma niliwahi kumshauri,
ushauri: Lowassa asikanyage arumeru!, atamponza sioi!.

matokeo yake tunayajua, na huu ni ushauri tuu.

Pasco


hana jinsi zaidi ya kufanya hivyo
 
Kuchaguliwa kwa Magufuli kulikuwa orchestrated! 5 bora ya CC ilikuwa dhaifu sana. 5 bora ya CC ilikuwa na J. Makamba-naibu waziri kwa miaka 5 tu, tena bila mafanikio yoyote ya maana zaidi ya maumivu ya MB8 na muonekano kwamba anabebwa na mbeleko ya Ikulu.

5 bora ya CC ilikuwa na 'wanawake' wawili ambao licha ya nyazifa kubwa walizowahi kushika, hawana ukaribu wowote na wananchi wa kawaida. Hawajawahi kufanya kazi popote ikawakuna wananchi. Ni wanasiasa wa ofisini wa kusaini hundi na mafaili. Hawazijui kero za watanzania na hawajawahi kuzitatua.

Pia 5 bora ya CC ilikuwa ina Membe. Sasa hapa ndipo palipokuwa na karata dume. Yaani unamkata Lowassa halafu unamuweka hasimu wake ambaye anasaidiwa na Ridhiwani na Mama Salma! Membe naye hana lolote la kujivunia ktk uwaziri wake wa miaka 8 ktk wizara ya mambo ya nje. He is an average person. Huyu ni dhaifu lakini aliyekuwa kwenye mbeleko ya familia ya ikulu.

Ktk 5 bora ya CC Magufuli peke yake ndo alikuwa ana afadhali katika utendaji na kutatua kero za wananchi. Yupo karibu na wananchi na amepata nafasi ya kukubalika toka apewe nafasi ya uwaziri. Chaguo la Magufuli lilikuwa dhahiri maana huwezi kumchagua kanjanja Makamba, wala kambi ya Lowassa isingekubali Membe apite kwa mbeleko ya familia ya ikulu wakati wao wanaamini walipaswa waungwe mkono na Kikwete. Mwisho, bila kuonyesha dharau kwa kina mama/wanawake, wananchi wengi wakiwemo wajumbe wa mkutano mkuu hawaamini kwamba umefika wakati wa kuwa na Amiri Jeshi Mkuu mwanamke. Tena kipindi ambacho Makinda amekuwa akibabaika na kupelekeshwa na wabunge katika nafasi ya spika. Kupwaya kwa Makinda ndiko kulikoua nafasi ya wanawake kenye urais. Njia ya Magufuli ilikuwa nyeupe!!

Hebu linganisha 3 za NEC 2005 (Kikwete,Salim, Mwandosya) kwa ueledi na uzoefu na hii ya sasa? Yaani Makamba ni zaidi ya Mwakyembe na Muhongo? Naona watu wamepitishwa kimakundi (vijana na wanawake) zaidi kuliko kwa kuangalia uwezo.
 
Inawezekana Kikwete sio rais mwenye akili kupita wote waliotangulia, lakini ni mjanja sana. Hakupenda kumtosa 'rafiki' yake Lowassa moja kwa moja. Akaamua kutumia mtindo wa kuuma na kupuliza. Akitaka kuuma anamtuma Nape, Makonda na Mangula, akitaka kupuliza anamsifia moja kwa moja kama alivyofanya bungeni hivi karibuni

Ukweli ni kwamba Kikwete hakumtaka Lowassa ndiyo maana akaitumia kamati ya usalama na maadili kumchomoa jamaa. Na hata Magufuli ni chaguo la JK maana unapomkata Lowassa na kumpitisha Membe kwenye 5 bora maana yake hata Membe hawezi kupita NEC. Kwa kuwaweka Magufuli katika kundi la kanjanja Makamba na wanawake wawili, alikuwa tayari amesafisha njia ya Magufuli.
 
Mkuu mimi kwa mapenzi yangu kwa upinzani na Mabadiriko ya Ukweli, ninaomba usiku na mchana jamaa avuke upande wa pili wa barabara. Gepu lake atakalotokanalo kule ni msaada mkubwa wa Upinzani. Si kwamba Upinzani hatuna kura za kutosha, hapana!, Tunataka kura za ccm zigawanyike ili kura zetu zibaki imara.

Nikija upande wa pili, sioni ni namna gani Magufuli anaweza kufanya kazi na Lowassa. Magufuli ni mtu kaksi sana, haingiliki kirahisi. Itamuwia ngumu sana Mwamba wa kaskaz "Kutekeleza" mambo yake chini ya huyu jamaa, hapa pia tukumbuke, Nyuma ya Mwamba wa kaskaz kuna grupu la watu ambao wana makandokando yasiyoeleweka, machafu yasiyomithirika!. Hawa kamwe hawawezi kumshawishi mtu kama Magufuli kutekeleza mambo yao.!!!

So naona njia moja tu ambayo Team Lowassa wanayo ni ku-cross the way, waende upande wa pili Wakamwage Mboga.!! Bado mambo ya Richmond yako vichwani mwa watu, waitumie kete hiyo ili wakose wote..!!! Lowassa ni Mwanaume wa shoka, alianza kuutafuta Urais tangu enzi za Baba wa Taifa, ktk kinyang'anyiro cha mwaka 2005 walikubaliana na jamaa yake ambaye hawakukutana barabarani kwamba, atangulie yeye, mwaka 2015 ni zamu yake Mwamba wa kaskaz...lakini ndo hivyo mwenzie kamsaliti waziwazi.!! Naye akae kimyaaa..!!!

Kama Lowas hakuiogopa ccm ya Nyerere iweje aigope ccm hii chovu ya Kikwete..? Nitamshangaa sana.!!

BACK TANGANYIKA

respect wa boda, nimependa maneno yako. Ninavyoombea Lowasa angekuwa anapitia hapa akapime hayo maneno moyoni mwake. Kwanza sasa hivi wanataka kumchinjilia mbali zaidi hadi kwenye ubunge asiwemo. Akiwa mjinga kukaa akifikiria atapita CC atapoomba ubunge wa Monduli imekula kwake.

Bila ubunge ataanza kuandamwa na TRA na PCCB kitachofata hapo ni imagination - sad imaginations....
 
Mzee Pasco,

Mwenzako Lowassa matokeo hajayapata or rather hataki kuyapata, mpaka sasa hivi anajua mchakato unaendelea
 
Wanabodi,

Mimi ni miongoni mwa watu tuliomuunga mkono kwa dhati, mwamba wa Kaskazini, Edward Ngoyai Lowassa, na tukaahidi humu akiondolewa kwa mizengwe, hatuta kubali, patachimbika. Kilichotokea ni kweli Edward Lowassa aliondolewa kwa mizegwe. Kuna watu humu hawakuuona uzi huu,
[h=3]Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC![/h]hivyo Lowassa alipokatwa walishangaa, kama wangeosoma uzi huu kabla, wasinge shangaa!.

Baada ya kuibuka jina John Pombe Magufuli, kuwa ndiye atakayepeperusha bendera ya CCM, kuna watu wanadhani amejiibukia tuu from nowhere!, No!. Na kuna wanadhani ameibuka surprisingly!, no!. Kama wangeusoma uzi huu,
[h=3]Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John[/h]angalau wangeelewa ni Magufuli!.

Kwa vile Lowassa ndie kipenzi cha watu, na wengi waliitegemea CCM itimize mapenzi ya watu, lakini CCM wakaamua kutanguliza mbele maslahi mapana zaidi ya taifa, kwa kuwaweke pembeni 'the giants', wengi wa wafuasi wa Lowassa wamekuwa take by surprise na wengine hata kuwa despaired, lakini laiti wangeusoma uzi huu,
[h=3]Edward Lowassa sio lazima yeye tuu ndiye awe Rais wetu [/h]wasingekuwa surprized!.

Maadam sasa uchaguzi wa CCM umemalizika, na mgombea wa CCM ni Dr. John Pombe Magufuli, natoa wito na ushauri wa bure kwa Mhe. Lowassa, ayakubali matokeo, avunje kambi yake au ile team yake, ayarudishe nyumba majeshi yake na kujisalimisha rasmi kwenye chama kwa kumsupport mgombea rasmi wa CCM!.

Kama mgombea angekuwa ni Membe, tungependekeza mapambano yaendelee kwa Lowassa kuvuka upande wa pili, nasi tumuingize ikulu!, lakini huyu aliyepitishwa, John Pombe Magufuli, pia ni jembe la ukweli, hivyo Lowassa hata akiamua ku cross, ataishia kupata kipigo kingine, yaani double tragedy !.

Kwa vile Lowassa ni chaguo la watu, na ni sisi watu tulio mchagiza kuwa 2015, ikulu ni yake, kwa ahadi hata asiposimamishwa na CCM, then asimame nje ya CCM tumpeleke ikulu, lakini kwa vile alipita ni Magufuli, ambaye na yeye ni jembe la ukweli, hakuna tena sababu kwa Lowassa kuendeleza mapambano maana huu sasa utakuwa ni mpambano wa mafahali, ziumiazo zitakuwa ni nyika!.

Lowassa tulikupenda, ila CCM imempenda zaidi Magufuli, teremsha silaha chini, kubali kushindwa, rudisha nyuma majeshi, jisalimishe!.

NB: Hii sio mara ya kwanza kwa mimi kutoa ushauri wa bure kwa Lowassa, huko nyuma niliwahi kumshauri,
[h=3]Ushauri: Lowassa Asikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.[/h]matokeo yake tunayajua, na huu ni ushauri tuu.

Pasco

Nakubaliana na wewe kuhusu kuvunja kambi kwa 100%. Ila Lowasa hakuwa kipenzi cha watu, alikuwa kipenzi cha wala rushwa, wanafiki, waahidiwa vyeo etc. Ndiyo maana hata amina alipata kura chache zaidi baada ya kuomba kura kambi ya Lowasa. Lowasa ajue watu ni wanafiki hata wewe Pasco toka moyoni ulikuwa humpendi ulikuwa unawaza ukuu wa wilaya etc, au akina olivia sanare walikuwa wanawza viti maalumu, uwaziri n.k., hakuna anayepinga umahili wa jk ktk hili, ccm iko kwenye line sasa
 
Last edited by a moderator:
Mzee Philip Mangulla na team yake wameliepushia TAIFA hili balaa ya kuwa nchi ya matapeli, wauza madawa ya kulevya, wezi, walaghai na majangili kwa kuwaengua Lowassa na Membe!!! VIVA Mangulla ; VIVA ccm!! Tuone sasa hawa wezi wa HOME SHOPPING centre watapitishia wapi makontena yao bila kulipa kodi kwani DHAIFU ndio anaondoka hivyo ingawa kuna uvumi kuwa atang'ang'ania kuendelea kuwa mwenyekiti hata baada ya Magufuli kuapishwa ; tofauti na walivyofanya watangulizi wake kwa kuachia kofia zote!!!
 
Pasco The President kiloriti, MUSSA ALLAN na wengneo, mfikishieni ujumbe huu Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Najua mnampenda ingawa Wajumbe wa CC hawakumpenda. Najua mnamkubali lakini CC haikumkubali. Najua mmeumizwa na yaliyotokea lakini wapo walioshangilia hadi kukesha kwa jambo hilo hilo. Hata mimi sasa,roho yangu kwatu kabisa! Nawaombeni mshaurini Mzee wenu atulie.

Mwaka 2010, Dr. Gharib Bila alitinga Dodoma akiwa na uhakika wa kushinda ugombea wa Zanzibar. Ni Bilal tu ndiye aliyekuwa akitakiwa na Wazanzibari kwa udi na uvumba.Kama si yeye basi angekuwa Ndugu Shamsi Vuai Nahodha. Wote. Bilal na Nahodha wakakatwa. Akawekwa Dr. Shein. Bilal alionesha ukomavu na kujiamini. Akalamba ugombea mwenza na kuwa Makamu wa Rais.

Mwambieni Lowassa atulie hivyohivyo. Asithubutu kufuata njia ya Ndugu Agustino Mrema. Ile ya 1995. Atapotezwa na kupotea. Atajuta kuifahamu CCM. Makabrasha yake yatafukuliwa na salama hatasalia. Abaki kimya na kukubali matokeo. Ashiriki kampeni na kukipatia ushindi chama chetu. Mlioamini kuwa Lowassa angepita ima wageni ndani ya CCM au 'bendera fuata upepo'. CCM ina wenyewe.Lowassa si mmoja wapo.

Akifungua mdomo,yatafunguliwa makabrasha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Last edited by a moderator:
Pasco The President kiloriti, MUSSA ALLAN na wengneo, mfikishieni ujumbe huu Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Najua mnampenda ingawa Wajumbe wa CC hawakumpenda. Najua mnamkubali lakini CC haikumkubali. Najua mmeumizwa na yaliyotokea lakini wapo walioshangilia hadi kukesha kwa jambo hilo hilo. Hata mimi sasa,roho yangu kwatu kabisa! Nawaombeni mshaurini Mzee wenu atulie.Mwaka 2010, Dr. Gharib Bila alitinga Dodoma akiwa na uhakika wa kushinda ugombea wa Zanzibar. Ni Bilal tu ndiye aliyekuwa akitakiwa na Wazanzibari kwa udi na uvumba.Kama si yeye basi angekuwa Ndugu Shamsi Vuai Nahodha. Wote. Bilal na Nahodha wakakatwa. Akawekwa Dr. Shein. Bilal alionesha ukomavu na kujiamini. Akalamba ugombea mwenza na kuwa Makamu wa Rais.Mwambieni Lowassa atulie hivyohivyo. Asithubutu kufuata njia ya Ndugu Agustino Mrema. Ile ya 1995. Atapotezwa na kupotea. Atajuta kuifahamu CCM. Makabrasha yake yatafukuliwa na salama hatasalia. Abaki kimya na kukubali matokeo. Ashiriki kampeni na kukipatia ushindi chama chetu. Mlioamini kuwa Lowassa angepita ima wageni ndani ya CCM au 'bendera fuata upepo'. CCM ina wenyewe.Lowassa si mmoja wapo.Akifungua mdomo,yatafunguliwa makabrasha!Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Ushauri mwanana.Tena wamwambie yale mafuriko yamezimwa na mikono!!!
 
VUTA-NKUVUTE katika ubora wake kwani kasema anahama? Nazan anataka kushukuru kwa alipofikia
 
Last edited by a moderator:
Pasco The President kiloriti, MUSSA ALLAN na wengneo, mfikishieni ujumbe huu Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Najua mnampenda ingawa Wajumbe wa CC hawakumpenda. Najua mnamkubali lakini CC haikumkubali. Najua mmeumizwa na yaliyotokea lakini wapo walioshangilia hadi kukesha kwa jambo hilo hilo. Hata mimi sasa,roho yangu kwatu kabisa! Nawaombeni mshaurini Mzee wenu atulie.

Mwaka 2010, Dr. Gharib Bila alitinga Dodoma akiwa na uhakika wa kushinda ugombea wa Zanzibar. Ni Bilal tu ndiye aliyekuwa akitakiwa na Wazanzibari kwa udi na uvumba.Kama si yeye basi angekuwa Ndugu Shamsi Vuai Nahodha. Wote. Bilal na Nahodha wakakatwa. Akawekwa Dr. Shein. Bilal alionesha ukomavu na kujiamini. Akalamba ugombea mwenza na kuwa Makamu wa Rais.

Mwambieni Lowassa atulie hivyohivyo. Asithubutu kufuata njia ya Ndugu Agustino Mrema. Ile ya 1995. Atapotezwa na kupotea. Atajuta kuifahamu CCM. Makabrasha yake yatafukuliwa na salama hatasalia. Abaki kimya na kukubali matokeo. Ashiriki kampeni na kukipatia ushindi chama chetu. Mlioamini kuwa Lowassa angepita ima wageni ndani ya CCM au 'bendera fuata upepo'. CCM ina wenyewe.Lowassa si mmoja wapo.

Akifungua mdomo,yatafunguliwa makabrasha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

wewe ni nani mpaka hutaki atumie haki yake ya kikatiba kuamia chama kingine kama anaona hakutendewa haki. ni unafiki wa hali ya juu kuwaambia watu wachukue form halafu mnaminya haki zao huku wakijua wazi wanakubalika lowassa atakuwa mjinga sana kama atakubali kubaki ndani ya chama cha manafiki eti kwa ajili ya tumbo lake tu wkt nia yake ni kupigania haki za watanzania. wewe vuta nikuvute tunajua huko ccm kwa ajii ya tumbo endelea huko lakini tuache sisi wenye uchungu na nchi tukafanye maamuzi magumu wewe endelea na yako ya kujaza tumbo
 
Vita vya marafiki wawili, silent and smiling killer adhihirisha kuwa ni prolific strategist than Edo. Cha msingi kaka Pasco ni Mhe Edo kuendeleza utiifu kwa mwenyekiti na Chama ktk kudumisha fikra za mwenyekiti. Nje ya CCM Mhe Edo atashindwa maradufu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom