Dr Matola PhD
Platinum Member
- Oct 18, 2010
- 61,892
- 110,060
Kwa bahati nzuri mimi nayaelewa vizuri mazingira ya wilaya kisarawe ambayo kwa upande wa kaskazini inaungana na wilaya ya Kibaha vijijini.
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo, tuachane na past za Jokate tumuangalie Jokate wa leo na kwa nia njia tunaowatakia mema vijana tunapaswa kumpa ushauri kwa sababu kuu moja tu.
Sababu kuu ni kwamba huu siyo uteuzi wa Jokate tu bali ni sampling ya vijana na warembo je wanapaswa kuaminiwa? Atakapovurunda Jokate atawaponza vijana wengi na warembo kutoaminiwa kupewa madaraka haya ya kupatia uzoefu wa kwenda juu.
Mzee Jakaya Kikwete aliwaamini vijana wa rika langu langu lakini walimuangusha mpaka akaamuwa kurudi kuteuwa wazee kama Profesa Muhongo, na vijana waliomuangusha ni Laurence Masha, Ezekiel Maige, William Ngeleja nikiwataja hao kwa uchache.
Sasa basi nikija kwenye hoja ya kile ninachomshauri Dc Jokate hii oparesheni yake awe nayo makini sana haijawahi kumuacha kiongozi yoyote salama kwa sababu yatokanayo ndani ya hizo oparesheni ujaa uonevu na dhulma dhidi ya wafugaji na askari wanaoshiriki zoezi hili wanaipenda sana hii oparesheni kwa sababu ya posho na dhulma zinazoambatana na hizi oparesheni.
Mimi ni muwekezaji upande wa kibaha vijijini kwahiyo oparesheni hiyo ya Jokate naijuwa vyema na madhara yake na siamini kwa ugeni wake ati yeye ndio amebuni hiyo oparesheni, ukweli ni kwamba kuna wajanja wanaonufaika na hizi oparesheni kwahiyo nina uhakika wa 100% Jokate anaingizwa kwenye dili za watu bila kujijuwa huku akidhani anapata kick kumbe anashibisha matumbo ya wajanja na kwa percent kubwa wafugaji siyo wa kuwapa ambush bali kuongea nao na kuwapa mapori ya kulisha mifugo yao, sipendi pia jeuri ya wafugaji kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima lakini ukweli ni kwamba swala hili liko juu ya uwezo wa Dc Jokate ni swala linalohitaji mjadala wa kitaifa
Balozi Kagasheki alipoteza uwaziri kwa oparesheni Tokomeza sasa na hii oparesheni Jokate ajiangalie.
Nimetumia uungwana wa Kitanzania kumpa ushauri wa bure mrembo huyu najuwa hakuna alijuwalo juu ya hili zaidi ya dili za watu.