Ushauri wa bure kwa DC wa Kisarawe mrembo Jokate

Ushauri wa bure kwa DC wa Kisarawe mrembo Jokate

Sasa basi nikija kwenye hoja ya kile ninachomshauri Dc Jokate hii oparesheni yake awe nayo makini sana haijawahi kumuacha kiongozi yoyote salama kwa sababu yatokanayo ndani ya hizo oparesheni ujaa uonevu na dhulma dhidi ya wafugaji na askari wanaoshiriki zoezi hili wanaipenda sana hii oparesheni kwa sababu ya posho na dhulma zinazoambatana na hizi oparesheni.
KABISA KABISA !!!!!!!!!
 
Statement yako haijaeleweka ila najua mtu kama umeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakataaje hiyo nafasi na ukiikataa ni kama umemdharau
Na unaweza ukaemda na maji, ( you can go and water).
 
Mshahara wa dc ni around 4.8 to 5M

Kwa mtizamo wangu nilikuwa najua kwa jina alilo nalo jokate, anauwezo mkybwa kuingiza hiyo ela na zaidi.

Kumbe hamna kitu.
Kiukweli hawa Star wana fake maisha kinoma.

Mjini kuna mengi sana
Haufiki 4M
 
KWANZA MA OPERATION MENGI YANAKUWA YA KUPIGA PESA NA UGANDAMIZAJI MKUBWA SANA KWA WANANCHI!!!!
LAZIMA MA DC NA MA RC WAWE MAKINI SANA .
 
Sahvi kila anayeteuliwa anatafuta public attention tu....mwisho we zinawaponza tu

Ova
 
Mdogo au mkubwa?
3.5m, hivyo kama unategemea ukiwa mkuu wa wilaya utajirike forget about that. In short nafasi za utumishi wa umma si za kufurahia kama huna wito maana utaishia kuwa mla rushwa na dhambi kibao. Yaani mpaka mawaziri hawana mishahara minono, yaani Charles Kimei anawazidi mawaziri mpaka rais kwa mbali sana mishahara, yaani vijana wengi ma CEO hapa mujini wanalamba 24-30 milion kama utani na unakuta wametulia tu na hapo bado bonus kila baada ya mwaka au miaka kazaa mil 200 plus. Hivyo kijana kuwa na ndoto zako za kutengeneza hela na siyo kusubiri uteuzi utakufa masikini!
 
Operesheni jokate itafukua tu makaburi hii na matokeo yake yapo ya aina mbili kuna kupandishwa cheo au kutumbuliwa
 
3.5m, hivyo kama unategemea ukiwa mkuu wa wilaya utajirike forget about that. In short nafasi za utumishi wa umma si za kufurahia kama huna wito maana utaishia kuwa mla rushwa na dhambi kibao. Yaani mpaka mawaziri hawana mishahara minono, yaani Charles Kimei anawazidi mawaziri mpaka rais kwa mbali sana mishahara, yaani vijana wengi ma CEO hapa mujini wanalamba 24-30 milion kama utani na unakuta wametulia tu na hapo bado bonus kila baada ya mwaka au miaka kazaa mil 200 plus. Hivyo kijana kuwa na ndoto zako za kutengeneza hela na siyo kusubiri uteuzi utakufa masikini!
Good!!
Nafasi za serikalini ni umasikini mtupu.

Kuna broh wangu ni marketing meneja wa breweries moja hapa nchini, ana miaka 30 nw lkn analamba 13M. Acha hizo bonus.

Kiufupi, bongo ukitaka utoke, pambana ukapige MBA yako UK/ US, piga kazi huko km 5yrs ukija bongo we ni CEO wa kampuni kubwa.

Hizi nafasi za kisiasa ni stress na kudumaa tu
 
Kwa bahati nzuri mimi nayaelewa vizuri mazingira ya wilaya kisarawe ambayo kwa upande wa kaskazini inaungana na wilaya ya Kibaha vijijini.

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo, tuachane na past za Jokate tumuangalie Jokate wa leo na kwa nia njia tunaowatakia mema vijana tunapaswa kumpa ushauri kwa sababu kuu moja tu.

Sababu kuu ni kwamba huu siyo uteuzi wa Jokate tu bali ni sampling ya vijana na warembo je wanapaswa kuaminiwa? Atakapovurunda Jokate atawaponza vijana wengi na warembo kutoaminiwa kupewa madaraka haya ya kupatia uzoefu wa kwenda juu.

Mzee Jakaya Kikwete aliwaamini vijana wa rika langu langu lakini walimuangusha mpaka akaamuwa kurudi kuteuwa wazee kama Profesa Muhongo, na vijana waliomuangusha ni Laurence Masha, Ezekiel Maige, William Ngeleja nikiwataja hao kwa uchache.

Sasa basi nikija kwenye hoja ya kile ninachomshauri Dc Jokate hii oparesheni yake awe nayo makini sana haijawahi kumuacha kiongozi yoyote salama kwa sababu yatokanayo ndani ya hizo oparesheni ujaa uonevu na dhulma dhidi ya wafugaji na askari wanaoshiriki zoezi hili wanaipenda sana hii oparesheni kwa sababu ya posho na dhulma zinazoambatana na hizi oparesheni.

Mimi ni muwekezaji upande wa kibaha vijijini kwahiyo oparesheni hiyo ya Jokate naijuwa vyema na madhara yake na siamini kwa ugeni wake ati yeye ndio amebuni hiyo oparesheni, ukweli ni kwamba kuna wajanja wanaonufaika na hizi oparesheni kwahiyo nina uhakika wa 100% Jokate anaingizwa kwenye dili za watu bila kujijuwa huku akidhani anapata kick kumbe anashibisha matumbo ya wajanja na kwa percent kubwa wafugaji siyo wa kuwapa ambush bali kuongea nao na kuwapa mapori ya kulisha mifugo yao, sipendi pia jeuri ya wafugaji kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima lakini ukweli ni kwamba swala hili liko juu ya uwezo wa Dc Jokate ni swala linalohitaji mjadala wa kitaifa

Balozi Kagasheki alipoteza uwaziri kwa oparesheni Tokomeza sasa na hii oparesheni Jokate ajiangalie.

Nimetumia uungwana wa Kitanzania kumpa ushauri wa bure mrembo huyu najuwa hakuna alijuwalo juu ya hili zaidi ya dili za watu.

View attachment 830144
Inawezekana upeo ni mdogo bado lakini tunavyo mjadili huyu dada bila sababu za misingi kwasababu tu ya uzuri wake au umashuhuri wake ni namna ya ubaguzi. Inawezekana hujui hilo bado lakini unachangia kubagua wanawake zetu , dada zetu na kuwafanya tuwaone kama ni vitu zadi wakati ni watu. Sasa mtu ameamua kufanya kazi kwenye jamii ambayo ni cheo kidogo hivi tena wilayani je tunatoa message gani kwa watoto wetu wa kike.
 
Akili zako hazikutoshi unahitaji booster. Soma upya thread jinga wewe.
 
Mshahara wake,mavazi yake,wachawi kibao JF,uchawi ungekuwa unafanya kazi tayari Jokate angekuwa keshapigwa kipapaii.
 
Nashangaa hiyo picha kweli DC mzima anakaa hapo mlangoni kama utingo? Sasa anampigia saluti nani? Saluti huwainapigwa mtu akiwa amekaa? Tatizo ni kuwa kila mteuliwa huwa anafuta kiki ya kuanzia kumfurahisha mkubwa wao. Hii ni kiki mbaya aliyoichagua. Jingine naona toka Mwiguli alipobuni skafu ya rangi za bendera ya taifa akina lugora wakaamua kuigeuza kuwa mifuko ya suti na huyu binti naye kaziweka mabegani. Kazi ipo!
 
Anapenda Sana public attention!
Ushauri hauwezi kimsaidia Kwa jeuri ya mamlaka anayodhani ameipata hapo Kisarawe....
Anasema mwenyewe ana sifa nying za Ku qualify hiyo nafasi hata akianza kuorodhesha hatamaliza leo....
Wachimba chumvi tumuache mtoto wa watu ainjoi kazi ya jamhuri.

It's about time!
Qualifications gani za kutumia zaidi ya siku moja? Basi atakuwa anaqualifications zaidi ya Mungu. Kweli time is a good teacher. Time'll tell!
 
Statement yako haijaeleweka ila najua mtu kama umeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakataaje hiyo nafasi na ukiikataa ni kama umemdharau
Siyo kazima kukubali teuzi na kabla ya kutangaza lazima awe consulted. Mbona kuna mdada mmoja aliomba asiteuliwe tena kwenye hiyo nafasi kwakuwa anashighuli zake nyingi abataka kuzisimamia
 
Watu kibao wameteuliwa na kujiuzulu, tena awamu hii. Km ni mfuatiliaji kuna dc aliteuliwa huko mbozi hata wilayani hakufika, akashukuru kwa uteuzi na kujiuzulu.

Mimi kama nina biashara zangu zinanipa zaidi ya 10M kwa mwezi kwanini nikasumbuane na wahuni huko?
Halafu baadaye uje utumbuliwe hadharani na kuaibishwa. Sasa huyu hata muda wa kuolewa ataupataje? Watamfuata huko kweli? Muda ukipita sana atakuwa artical of no commercial value kama dada Ubaya Spade aka Hama Hama Jazz Band
 
Mbona ulichopost hakihusiani na mada?
Mada haizungumzi mshahara wa DC
Kinahusiana mkuu. Ana maana kwa sifa na uwezo wa huyo binti anaweza kupata zaidi ya 4m kwa mwezi kwa shughuli zake hapa town kuliko hiyo nafasi ambayo inaweza kumletea matatizo makubwa kutokana na kuvamia operation bila kutulia kwanza na kuwa mwangalifu.
 
Back
Top Bottom