Ushauri wa Bure kwa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa Bure kwa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by V.P, Nov 5, 2011.

 1. V

  V.P Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Viongozi na wapenzi wa Chadema. Nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu mwelekeo wa siasa nchini na nimejaribu sana kufanya utafiti usio rasmi. Nilitaka kufahamu watu wanaounga mkono CCM wanafanya hivyo kwa misingi gani na wanaounga mkono Chadema wanasukumwa na nini na pia kutaka kufahamu wanaopinga wanapinga kwa nini.

  Nilichogundua ni kwamba wanaoipenda CCM wanafanya hivyo kwa sababu ya mazoea na pia kwa sababu ya kukwamisha Chadema, ni wachache mno wanaounga mkono CCM wanafanya hivyo kwa ajili ya sera ama utendaji.

  Kwa upande wa Chadema, watu wengi wanaounga mkono Chadema wanaona chama hiki ni chama cha kumkomboa Mtanzania kutokana na dhuluma na ufisadi wa CCM, ni chama kinachowapa wananchi matumaini. Halikadhalika nimegundua kwamba waislamu wenzangu wengi wanakiona Chadema si tu kama chama cha kikristu bali pia ni cha kibaguzi na ni hatari kubwa sana kwa Waislamu. Mtazamo huu haupo miongoni mwa watanzania wenye elimu ya wastani ama pato la wastani bali hata wasomi wenye title ya udaktari wana mtazamo huohuo na watu wenye uwezo. Kwa kweli mimi nimekipenda sana chama hiki kutokana na sera zake na pia msimamo wake thabiti dhidi ya dhuluma katika jamii na pia nawapenda sana waislamu wenzagu na ningependa kuona Chadema kinakubalika kama chama cha waislamu vilevile.

  Huenda watu wakanibeza na kudai naleta hoja za kidini lakini napenda kuwakumbusha Chadema kwamba bila ya Islamic vote Chadema haiwezi kufurukuta katika uchaguzi ujao. Pia ninaona Chadema inafanya makosa mengi kuhalalisha lack of confidence from Muslims, mfano sijawasikia hata mukitoa mkono wa Ramadhan ama Eid lakini uhuru wa South Sudan mulitoa pongezi kwa haraka sana. Mambo kama hayo yananipa mimi na waislamu tunaowaunga mkono shida sana kuwashawishi wenzetu kwamba Chadema ni mkombozi wa wote na Chadema haina ubaguzi.

  Ninachoshauri sasa Chadema ijenge mkakati maalumu wenye lengo la kupata support ya Waislamu, ikibidi hata mulete mjadala kati ya Chadema na waislamu ili waislamu wafahamu msimamo wenu juu ya mambo muhimu kwa waislamu. Chadema haiwezi kupata kura za waislamu kutokana na sera tu ama kampeni za uchaguzi, acceptance must begin now. Waumini wenzangu wanaomba mpaka dua musiingie madarakani. Haya yote yanaweza kubadilika na mukawa munaombewa dua muingie madarakani kama mutafanya kazi nzuri ya kukubalika. Hata nchi zilizoendelea swala la dini ni nyeti na ndio maana dini za viongozi huwa zinajadiliwa, tafadhalini sana musi underestimate ushauri wangu.Ninawashauri Chadema kwa kuwa nina imani nacho na pia ningependa kuona ndugu zangu na waumini wenzangu wa Kiislamu wanajiunga na Chadema kwa wingi.

  Asanteni
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  habari za visiwani mkuu
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  VP
  Na wewe unaweza kuwa balozi wetu miongoni mwa Waislamu wenzako kwa kuwasaidia kuwaelewesha kwamba Chadema si chama cha kidiini na kuwakumbushia madhila ambayo CCM imetuletea sote Watanzania.
   
 4. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red ndipo ulipo boronga. Kwamba CDM haiwezi kukwea hadi madarakani bila kura za Waislamu! Kwa hiyo leo hii CCM ipo madarakani kwa sababu ya kura za Waislamu. Kasome vizuri Statistics za Tanzania ndugu yangu..
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe kuhusu kuwa na mijadala na watu mbalimbali vikiwepo vikundi vya dini. Ila kitu kimoja ambacho sikipendi kabisa ni hii tabia ya viongozi na hasa rais anatoa chakula kwa watoto yatima au wazee n.k wakati wa sikukuu za dini au kitaifa na kuita 'zawadi'! Chakula ni zawadi?

  Najua kuwa huu ni utaratibu wa siku nyingi lakini kwa nini karne hii watu hawataki kufikiri wanaongoza nchi kwa ku-copy & paste? Rais anawapa chakula watoto yatima au wazee wasiojiweza wakati wa shule je baada ya sherehe watakula wapi? Nani mwenye jukumu la kuwapa chakula wazee wasio jiweza au watoto yatima? Na inakuwaje unaita chakula zawadi?

  Mfano kalamu ni inaweza kuwa zaidi, na unaweza kuishi bila kupata zawadi hiyo (kalamu) lakini huwezi kuishi bila chakula! Sasa inakuwaje rais wa nchi akumbuke kuwapa chakula maskini hawa wakati wa sherehe baada ya hapo anapotea! Haya ni makidai ya makumpuni binafsi, nilitegemea serikali iweke sera/mpango wa kuhakikisha kuwa hawa wazee wasiojiweza wanapata chakula muda wote wa mwaka na sio kuwafanya kama maonesho wakati wa sherehe wakimata mbuzi eti na unga - eti zawadi?
   
 6. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,277
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ushauri Mzuri sana.
  OMBI LANGU KWAKO:
  Na wewe kwa kuanzia jaribu kuwaeleza waislam watano mema ya Chadema, Kisha hao watano uwatume wakaeleze wema huo kwa wa watu watano kila mmoja, na wao vivyo hivyo. Na imani kwa style hii tutakuwa sisi wapenzi wa chadema tumeweza kutangaza chama chetu na mema yake. Sio kura tu hata Dua zinahitajika.

  Sote bila kujali tofauti zetu za imani, jinsia, umri, kabila nk, ni Watanzania na Tanzania ni yetu sote. Eneza Habari
   
 7. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #7
  Nov 5, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  Hizo thread kuhusu uislamu sichangii tenaaaa! Jana nilikula Ban kwa ajili ya kukosoa mambo ya kuuona uislamu ni dini bora kuliko nyingine zote duniani.
   
 8. V

  V.P Member

  #8
  Nov 5, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Demographics ziko wazi na zinaonesha kwamba chama chochote ambacho kitasusiwa na Waislamu ama Waristu hakiwezi kutwaa dola. Siri moja kubwa ya CCM kushinda ni kuvutia dini zote.
   
 9. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Na mimi nishawahi kuwaza kama mleta mada. Natamani CCM watoke madarakani kwa kushindwa kwa kishindo ili wasipate mwanya wa kuchakachua na ndipo suala la kutegemea kura za waislamu linapojitokeza. Lakini baada ya kuwaza sana hasa katika kufikiria ni mkakati gani chadema wanaweza kuutumia kupenya kwenye ngome za waislamu nikagundua pengine si muhimu sana kwa Chadema kuhofia jambo hili la kufanya jitihada za makusudi kuvutia kura za waislam au kutamani sana kwenda ikulu. Kama watanzania walio wengi (wakiwemo waislamu) hawataipigia kura chadema eti kwa sababu fulani fulani za kidini au kikabila badala ya kuangalia hoja na sera basi huo hautakuwa udhaifu wa Chadema bali wa wapiga kura wenyewe. Na kinachoifanya Tanzania iendelee kuwa na umaskini, ujinga na maradhi, ni kwa sababu wapiga kura wengi ni maskini, wajinga na wagonjwa kiasi cha kushindwa kuchagua chama sahihi. Sasa hapa tusitegemee miujiza. Mpaka pale watu watakapoanza kupambanua kwamba dini zetu hazitusaidii kupambana na ufisadi, ujinga wala maradhi, na makabila yetu hayatusaidii, na kwamba tusitumie vigezo hivi katika kuchagua chama au mgombea.....basi hapo ndipo tutakapokwamuka kama watz, waislam, wakristo, pamoja na makabila yetu.
   
 10. m

  mtolewa Senior Member

  #10
  Nov 5, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mkuu mengi uliyosema ni ya kweli hasa la mdahalo na waislam ingawa wengine wanaweza kuhoji kwani waislam hawaoni,hawasomi wala kusikia mambo mazuri ya chadema kwenye sera,katiba na utendaji wao wa kila siku mpaka waandaliwe mdahalo maalum? ukweli ni kwamba waislam wengi kwa makusudi wamepotoshwa sana kuhusu mambo mbalimbali sio ya siasa tu bali hata ya uongozi wa serikali.mfano kwa utafiti wangu usio rasmi nimegundua kuwa waislam wengi bado wanaamini kuwa wanafunzi wa kikiristo pamoja na shule zao huwa wanapendelewa ktk mitihani huku wao wakionewa!
  kwa mawazo uliyotoa unajipambanua kama mtu aliyeelimika na ni kwa muktadha huo naungana na wa jf wengine kuwasihi vijana wa kislam wanaoelewa mambo na wenye nia njema kuwaelimisha waislam wenzenu ukweli ulivyo kuhusu mambo mbalimbali ingawa najua mtakutana na vikwazo vingi sana kwani baadhi ya wapotoshaji wa makusudi ni viongozi wenu wa kidini. Inshallah Munyazimungu awafanyie TOWFIQ MPATE KUWAELIMISHA NA KUWASHAWISHI WAISLAM WENGINE WAWE WANAKUBALI MAMBO BAADA YA KUYAFANYIA UTAFITI NA KUYAHAKIKI BADALA YA KUMEZA KILA KITU WANANCHOAMBIWA KWA HISIA TU.
   
 11. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Ushauri wakozuri Ila suala la kutoa chakula kwenye sherehe za kioslamu siyo kweli,
  CCM imekuwa ikiwatumia Waislamu Kama Tools ya kupata kura kila mwaka ilianza kuitumia sera za Udini kwa CUF na sasa wanatumia fimbo hiyo hiyo kuwapiga Chadema na Fimbo ya Udini CCM inatumia Udini ili kuwamaliza wapinzani wake Udini Mfano juzi juzi huko igunga iliibua habari za Hijab ili ifuse hisia za waislamu na waislamu waliposhikwa walishikamana na kusema hawaipigii kura Chadema wakati kuna wabunge Lucy Owenya alipigwa ngwala na askari wa kiume na alidhalilishwa pia kule Rukwabunge wa CUF aliwekwa selo moja na wanaume pia alidhalilishwa lakini hakukuwa na Tamko la labda kwa kuwa si waislamu.
  Waislamu amkeni CCM inawatumia tu kama......Amkeni tuungane tuwatoe hawa watu wamewaonea kipindi kirefu sana mara Wanaweka Mahakama ya Kadhi kwenye Ilani ya chama chao kumbe wanawapiga changa la macho Enyi ndugu Waislamu kataeni kutoa matamko ya kuwafurahisha CCM.
   
 12. T

  TrueVoter JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 875
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 80
  Haina haja kuseek special audience na watu ambao wameamua wao kwa akili zao kukataa ukweli! dini zote ni sawa mbele ya vyama vya siasa labda ccm ambako wanataka hizo tofauti, ndio maana wakaja na mambo ya zamu kwa nafasi ya urais au uongozi wowote, mambo ya kipumbavu kabisa!!!
  kama CHADEMA ni chama kinachojali maendeleo ya watanzania haina haja kubembeleza watu wakubali kitu kiko wazi hata watoto wa shule za msingi wanajua!! asietaka kuona hilo mwache! wala si kweli kwamba waislamu wana vote ya kufanya chama kishinde uchaguzi au kisishinde!
   
 13. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #13
  Nov 6, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama hili ndilo jibu baada ya kusoma Demographics za Tanzania basi naweza kusema bado hujazielewa. Kwamba CCM imeweza kuvutia dini zote hilo ni la Uongo. CCM chini ya Kikwete ndio waasisi wa udini ambao tunaujadili leo hii hapa ambao ulikuwa ni nadra sana kuusikia enzi za Mkapa, Mwinyi na Nyerere.

  Leo hii Wakristo wanaichukia CCM kutokana na kujijenga hisia (kwa sababu wanazozijua wao) vichwani mwao kwamba CCM hii ya JK ina pendelea Waislamu. Na waislamu nao wanaichukua CCM kwa sababu ya kuwahadaa katika ilani yake ya Uchaguzi wa 2005 kwamba watawasaidi waanzishe Ofisi ya Kadhi Mkuu kupitia mgongo wa serikali. Pia iliwaahidi kwamba itaiingiza Tanzania katika jumuia ya kiislamu OIC. So CCM haina mvuto kwa dini zote. Na 2010 CCM haikushinda kwa haki kwa kuwa walitumia loop holes za Tume ya Uchaguzi ambayo si huru. Ubovu wa katika Katiba yetu pia ulichangia CCM ipate huo ushindi wa wizi unaouita ni ushindi..
   
 14. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #14
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Tatizo sio kuwashawishi waislam ili wakipende CHADEMA, Tatizo ni kwamba hiki ni chama chenye sera za kidini na kikabila. Na hii imetokana na na kuwa na uchu mkali wa kuingia IKULU haraka haraka, hivyo kulitumia kanisa ili chati yao ipande kwa haraka sana. Hii inawagharimu sana

  Hata mbeya ambao walikishabikia na kupata wabunge kupitia chama hicho, wakagombana kwenye ugawaji wa viti maalum. Asilimia 80 ya viti maalum vilikwenda Moshi na Arusha. Sasa unatarajia kuwaeleza nini wananchi ikiwa katibu mkuu wa CHADEMA alishasema kama hawataki wahame CHAMA. Maana udikiteta uliopo hakuna hata majadiliano.

  Ikiwa mgombea wao wa Urais katika uchaguzi mkuu 2010 alipoulizwa kuhusu tuhuma za kuhusishwa chama chake na udini, alishindwa kujibu au kuwashawishi wananchi kuwa hizo shutuma ni za uongo. Sasa ndugu yangu unatarajia huyu mtoa hoja atawezaje kuwashawishi waislam kuwa CHADEMA NI POA, haina udini.

  Jisafisheni kwanza ndani ya CHAMA CHENU kabla waislam wanaowapenda hawajawapigia debe.
   
 15. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #15
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Kama hizi hoja ndio hoja za CHAMA, basi CHADEMA MSUBIRI MIAKA 50 KUINGIA IKULU au mkate tamaa kama Bwana Mapesa- Cheo na kichama chake cha kikabila kabila.

  Kweli nawasikitikia kwani wapenzi wengi wa CHADEMA wanalugha kama hizo za kejeli, na eti katika mkakati wao wa uchaguzi mkuuu 2015 wanataka kujikita vijijini ambako karibu 70 % hawana elimu tosha wanayoihitaji CHADEMA kwa wapiga kura. Tatizo lenu ni kwamba nyie mmejikita sana Moshi na Arusha ambako watu wengi wamekwenda shule. Lakini unachosahau ni kwamba asilimia kubwa ya watanzania wameishia darasa la saba au kidato cha nne failure. Hawa ndio watu utaowaongoza, hivyo ni muhimu katika kampeni kuwafikishia ujumbe wataoamini kuwa ni msaada kwao ikiwa utaingia madarakani. HAPA NDIPO CCM WANAPOWASHINDA. Ninahakika mkiingia madarakani mtaweka kikwazo cha kupiga kura ni kuwa na elimu ya kidato cha sita na kozi ya miaka miwili. Haa haaa haaaaa!

  Ikiwa kama tungekuwa na vyama vingi mwaka 1965 sijui CHADEMA Mngewaambia nini wananchi. POLENI! Kweli wenzetu hamjui siasa.
   
 16. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Kwa hili CCM wasubiri miaka michache kufikia 2015 jibu watalipata na Zawadi Ngoda na siasa zake za Udini jibu atalipata.
  Waislamu someni Alama za nyakati CCM inawatumia tu wala haina haja nanyi leteni hoja za kuungana na sikuleta hoja za Kidini maana hazitasaidia Watanzania.
   
 17. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #17
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Malaria sugu na udini. Hv huna thread zaidi ya huu udini?
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #18
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Jambo la kuangalia siyo chadema inafanya nini ili kitarajie nini, au ccm ifanye nini kipate nini. Kitu cha msingi ni kwamba watanzania tunataka tuwe katika mzunguko mzuri wa maisha ya kueleweka kwa rasilimali tulizonaza, bila kutegemea misaada isiyo ya lazima inayotudidimiza. Tunataka tufaidike na rasilimali zetu, uchumi imara, elimu kwa wote. Mambo haya yote yameshindikana kufanyika kwa muda wa miaka 50 ya uhuru chini ya utawaka wa serikali ya ccm. Pamoja na nchi hii kubarikiwa kuwa na mali asili nyingi ukilinganisha na nchi zinazotuzunguka, pesa zetu zimekuwa zikishuka thamani kila kukicha. Suala la kujadili uislamu au ukristo siyo ilani ya cha ccm wala chadema. Hivi sasa tunatakiwa tukombolewe kwenye haya mateso ya kimaisha na kiuchumi wa mtu moja moja. Ili kutekeleza hili tunatakiwa kuwasimamisha viongozi wenye uzalendo na nchi hii kutoka moyoni mwake, asiye mdini wala mkabila.
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mwandishi wa hii thread kaandika mambo mazuri sana lakini suala la udini cjui kama cdm wanasingiwa au la ila yafaa wakristo kwa waislam kuwa wamoja ktk kuikomboa TZ yetu kwani tusitegemee mgeni ajekuijenga bali wataibomoa kama wanavyofanya wachina kutuletea bidhaa bandia pamoja na serikali kuwaruhusu kujakufanya biashara ndogondogo ambazo wazawa tunaenza kuzifanya. Miezi kadhaa ya nyuma serikali ilituhadaa wanawaondoa nashangaa ndo wameongezeka kwa kasi nahisi chama kingine kikiingia madarakani wanaezakuwa thabiti ktk mambo madogomadogo kama haya yanayotutesa ndani ya nchi yetu.
   
 20. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #20
  Nov 6, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  mh nchi hii inamatatizo mengi sana kuliko,udini kuna katiba mbovu na hila za kuleta katiba mbovu zaidi! kuna magonjwa ya kawaida yanaua watz miaka 50 ya uhuru,kuna ukosefu wa huduma za jamii hata maji tu hakuna wakati 13% ya maji baridi yako TZ! KUNA raslimali zinaibiwa! kuna ukosefu wa utawala bora ukiukwaji wa misingi ya demokrasia ! hivi sisi waislamu tunawaza nini? mbona tusiwape CHADEMA support kwanza kwa mambo ya jumla tunajibagua HATUONI KAMA NI UBINAFSI MKUBWA ? na CDM imeandika wapi kwenye katiba yake kuwa haiwajali waislam mpaka tuweke hofu!? WAISLAM TUNAENDA WAPI?
   
Loading...