siku hizi kuna usemi kuwa kakumbuka shuka huku kumekucha. Ni usemi ufananao na majuto mjukuu. Mwanasiasa makini ni Yule anaesoma alama za nyakati na kuwa na dira ya kumfikisha kwenye mafanikio. Mwanasiasa hodari lazima awe anabadilika kutokana na mazingira yaliyopo. Tatizo la vyama vyetu vya siasa na wanasiasa, hawapendi kusikia upande wa kukosolewa! Wanachotaka kusikia ni sifa! Ukawsifu wanafurahi. Natoa nasaha zifuatazo kwa vyama vya siasa Khasa ccm, chadema na cuf huku nikieleza mapungufu / kasoro za kila chama.
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
chama cha ccm ni chama kikongwe. kina makada wazoefu wa siasa za kila aina. siasa baridi, siasa safi na siasa chafu. kina mabingwa wa propaganda. pana uwezekano, kina mamluki katika KILA chama cha siasa. Ccm kina sifa kuu moja: kimeunganisha watanzania kutoka ktk kila kanda, dini, rangi na kabila. hali hii imetokana na kuwa chama pekee kwa miaka mingi hadi mwaka 1992. huwezi kusema ni cha wakristo au waislamu. wote ni chama chao. Kina kasoro nyingi ambazo zinatokana na KUKOSEKANA UWAJIBIKAJI NA UTAWALA BORA. kinasuasua ktk kuwaadhibu wanachama wake wanaotajwa ktk kashfa mbalimbali za rushwa. kukumbatia wala rushwa ni ishara ya kwamba rushwa ipo na imeshamiri. hali hii inatusababishia maendeleo duni. Baadhi ya wapinzani wanasema maana ya ccm ni chukua chako mapema. Kauli hii inatokana na wizi wa mali ya umma wakupindukia wa viongozi wa serikali. Sera ya KULINDANA inaharibu utendaji wa ccm na serikali yake. Ccm wana mtaji wa watanzania wengi ambao ama hawajafikiwa na vyama vya upinzani (hufikiwa siku moja tu ya kampeni ktk miaka mitano) au wana mapenzi ya kupindukia kwa ccm. Hali hii inawasaidia sana ccm
ccm wana hali ngumu kuhusu mgombea urais 2015 lkn wana sifa moja. wanaweza kwenda dodoma (kizota) wakiwa na tofauti kubwa. la ajabu wanatoka wakiwa kitu kimoja na wagombea wanapeana mikono. sijui huwa wanafanyaje!!!!!!!!!!!!! Sasa hivi kuna makundi ya wagombea lkn atapitishwa mmoja na wote watakaa kimya!
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
chama cha chadema ni chama ambacho kimefanya vizuri sana ktk uchaguzi wa mwaka 2010. idadi ya wabunge wake imeongezeka sana na ndiyo chama kikuu cha upinzani. kina viongozi jasiri ambao ni wabunifu na hawana uwoga ktk kueleza na kutetea ukweli.
Chadema kina kasoro kadhaa zifuatazo:-
a). viongozi wake wakuu wana ushindani wa kisiasa, sifa na umaarufu. hili ni tatizo kuu chdm. kushindana huku kumewafanya waogopane na kuoneana wivu. wanaweza kuonekana wana safu moja lkn ukiangalia kwa jicho la kiuchambuzi utagundua kuwa slaa, mbowe, zitto, lissu, msigwa, mnyika nk...... wana matabaka ya ndani kwa ndani.
b). chama chochote lazima kianzie ktk eneo mojawapo ktk nchi yetu. chdm kilianzishwa na mtanzania kutoka kasikazini. bila shaka mizizi yake ilianza kuimarika kaskazini. ccm wakatumiya mwanya huu kukipaka matope kuwa ni chama cha kikanda na kikabila hadi wakatafsiri chadema kuwa ni chagga development manifesto (ilani au mradi wa kuwaendeleza wachagga). hali hii imefanya watanzania wengine waogope kujiunga na chama cha chdm.
c). ccm wamepakaza kuwa chdm ni chama cha wakristo. wakawa wanatoa mfano wa viongozi wake wakuu. wakasema dk. kabourou alipokua katibu mkuu, alipigwa vita kwa kuwa ni muislamu. kutodhihirika kwa majina ya kiislamu ya bob makani na zitto kabwe, kulifanya watu waamini kuwa viongozi wote wa chdm ni wakristo. chdm hawakujitahidi kuweka wazi kuwa bob makani, zitto kabwe na mzee arfi ni waislamu. japo mzee arfi anajulikana lkn amekua hapewi nafasi ktk majukwaa ya chdm licha ya kuwa ni makamu mwenyekiti. Propaganda za kuwa chdm ni chama cha wakristo, zimewafanya waislamu waliowengi waogope kujiunga chdm. CHDM WATAFAKARI NAMNA YA KUTOKOMEZA MADAI HAYA!
d). chdm kimeridhika kwa kuwa na mashabiki na siyo wanachama wakereketwa. kimesahau kuwa kasoro ya ccm ktk kura za maoni mwaka 2010, ndizo zilizochangia chdm kupata wabunge waliohama ccm. Vilevile baadhi ya wanaccm walikikomoa chama chao kwa kuipa chdm kura. Hii ilitokana na hasira za kura ya maoni ndani ya ccm. huu ndiyo ukweli kuhusu mwaka 2010. MFANO MDOGO NI KWAMBA IRINGA MJINI WALIMTAKA MWAKALEBELA. ALIPOPITISHWA MBAGA, WANACCM WOTE WAKAMPA KURA MSIGWA WA CHDM. HAWA BADO NI WANACCM HADI LEO NA WANAIPENDA CCM! pana uwezekano mkubwa kuwa iwapo ccm itacheza karata vizuri, itarudisha sehemu kubwa ya viti vyake katika uchaguzi wa mwaka 2015. ufunguzi wa matawi ya chdm unafanywa sn vyuoni na nje ya nchi kuliko vijijini. hii ni kasoro! CHADM inategemea mikutano ya hadhara ya siku moja kuliko uhaasishaji wa kila siku matawini.
e). kinyang'anyiro cha kumtafuta mwenyekiti wa chama na mgombea urais mwaka 2015 nalo ni tatizo chdm. mbowe, zitto, lissu na slaa wote nadhani wana nia ya kugombea urais (japo kuna utata kwenye umri wa zitto). slaa alifanya vizuri 2015 lkn wengine wanamuona kama mzee ambae huenda asiwe na mvuto 2015. Kashfa lukuki anazo undiwa wengine wanasema zinatoka ndani ya chdm! mbowe ana sifa lkn ile propaganda ya ccm kuwa chadema ina wenyewe, inamgharimu kwa kufanya wanachdm kutoka mikoa mingine wasimkubali.
f). lugha inayotumiwa na wanachama wa chdm kuwaelimisha wanachama wa vyama vingine ni kali sn. Inatumika jazba sn kuliko busara! Hili jambo linafanya ongezeko la wanachama chdm kusuasua. Vijana wasomi kutoka vyuo wanajazba na wanataka mabadiliko leo hii siyo kesho. Chdm kina jukumu la kuwaelimisha vijana wake kuhusu lugha ya kutumia kuwavutia wanachama. SILAHA KUBWA NI KUMUELIMISHA MTU SIYO KUMTUKANA!
Civic United Front (CUF)
chama cha wananchi cuf hakikufanya vizuri mwaka 2010 tofauti na chaguzi zilizotangulia. ni chama ambacho kina kasoro zifuatazo;
a). uongozi wa juu wa chama haubadiliki. japo prof lipumba na maalim seif wamejaribu kufafanua kuwa wao ni wapiganaji ambao wako vitani hivyo makamanda huwa hawabadilishwi kama nguo. Wakibadilishwa malengo yatapotea. kutobadili viongozi wa juu kumetumiwa na ccm pamoja na chdm kuisulubu cuf.
b). ccm ilianzisha propaganda kuwa cuf ni chama cha waislamu. kama ilivyo chdm, cuf nayo ilianzia sehemu mojawapo ya jamhuri yetu. wakazi wa eneo la visiwani wengiwao ni waislamu. cuf ikawa na wanachama wengi wa mwanzo wakiwa waislamu. hali hiyo ikatumiwa kisiasa na ccm kuwa cuf ni chama cha kidini na wakristo waliowengi jambo hilo limewatia hofu kujiunga cuf! wengi wanakiita chama cha wapemba na waislamu
c). licha ya profesa lipumba kuwa msomi lkn ameshindwa kuwavuta wasomi wenzake kujiunga na cuf. chdm kimefanikiwa kuwavuta wasomi wengi tu! kosa hili la lipumba limekiathiri sn chama.
d). safari za mara kwa mara za lipumba na za muda mrefu nje ya nchi zinachangia kudumaza chama. Hafanyi uhamasishaji hadi kipindi cha kampeni. Jembe linalo saidia cuf ni Julius mtatiro. Akiwezeshwa kifadha, anaweza kuamsha hamasa za watu kujiunga cuf. Vilevile atafuta dhana ya cuf ni chama cha waislamu.
e). hakuna asiejua hali na mpasuko wa kisiasa ulivyokua visiwani kati ya ccm na cuf. ilifikia waamue kuungana ili kusitisha tofauti zinazo irudisha nyuma znz. ni jambo zuri lkn chdm wamelitumia kwa kuisulubu cuf. wanaiita ccm B. si kweli kuwa cuf ni ccm b lkn kisiasa chdm wanahaki ya kusema hivyo. cuf wanadai kuwa vile wamo serikalini, 2015 watachukua znz. hawatoibiwa kura tena. yetu macho!
vyama vya nccr, tlp, udp nk....... havifanyi vizuri sn. inasemekana kuwa ushindi wa nccr kigoma ni kutokana na mgombea wao urais wa 2010, mzee hshim rungwe kuwa mwenyeji wa kigoma. walimpa kura za "tusimuangushe mtoto wetu...". mrema kwishnei, cheyo yupoyupo........
KWELI CCM ITANG'OKA 2015?
jibu la haraka ni kuwaHAPANA. pana uwezekano mkubwa wa ccm kushinda. kwa nn nasema hivi?
1- ccm wanauzoefu wa kumpitisha mgombea na tofauti zao zikaisha. rasharasha huwepo lkn huwa chache sn!
2- vijijini bado wana imani kubwa na ccm na hata baadhi ya miji.
3- tofauti za safu ya juu ya chadema zinaweza kukipa zilzala (mtikisiko) kipindi cha uchaguzi wa mwenyekiti na mgombea urais. Hii itakua neema kwa ccm.
4- propaganda za ukanda na udini zimekua mwiba kooni mwa chadema. hakikubaliki sn kwa waislamu. anae bisha apitie matokeo ya uchaguzi wa 2010 ktk tovuti ya NEC. Ataona chdm ilivyofanya ktk maeneo yenye waislamu wengi nchini.
5- cuf imekuwa ikiiharibia chadema. uwepo wa cuf ni kihunzi kwa chadema. na hivi sasa uadui bungeni wa cuf na chdm ni mkubwa. Cuf itaendelea kupunguza kura za chdm.
6- ili ccm ifanye vizuri, pana uwezekano ikakubaliana kuwapa cuf znz ili wanacuf wa bara wote waipigie ccm. Mpango huu unaweza kuinufaisha ccm huku bara. Ktk siasa lolote linawezekana. WANASIASA NI WANAHARAMU SANA! (ashakum
!)
7- siyo siri uchaguzi wa 2010 ulitawaliwa na udini (anaekataa hili atakua na matatizo). ccm ilikua na mgombea muislamu. cuf ilikua na mgombea muislamu. chdm ilikua na mgombea mkristo. wakristo wengi walipeleka kura zao chdm. kura za waislamu wengi zilikwenda ccm na cuf. mwaka 2015, pana uwezekano mkubwa ccm watampitisha mkristo. hali hii itapunguza kura za chadema. maaskofu ambao walikuwa upande wa chdm, wakiona mgombea mkristo ccm, bila shaka watahama na wafuasi wao kwenda upande wa ccm.
Ikumbukwe kuwa ccm inajua KULA VIZURI na viongozi wa dini!
Bado hakujakucha! Shuka bado lina umuhimu kutokana na baridi iliyopo. Ili chama kifanye vizuri 2015, kizingatie ushauri wangu. kusema ccm inaweza shinda 2015, hayo ni maoni yangu binafsi! hata ccm inaweza kuangushwa vile ktk siasa lolote linawezekana!
nimeandika makala haya kwa kutanguliza uzalendo mbele!
Wakatabahu: wakuziba (mzee wa maneno yanayochoma nyoyo)