Ushauri wa bure kwa chadema

Mkombozi

JF-Expert Member
Feb 19, 2008
806
426
Nawasifu sana CDM kwa kutoa elimu ya uraiya kupitia maandamano ya kanda ya ziwa.Ila kikubwa ninachowashauri wasisahau kugawa kadi za uanachama wa chadema.Huu ni wakati wa kupata wanachama wengi sana.Ni muhimu sana kuanza kuongeza base ya uanachama na kua nao wa kutosha.Wakifanya hivyo itasaidia sana kwenye chaguzi zijazo pia.Kingine wangeenda na Tshirts,kanga,kofia au magwanda ya chadema,wengi wanayahitaji.Hata kama hawana hela waende nayo wawauzie kwa bei nafuu.
 
Mkombozi hilo wazo ni kweli nakuunga mkono wakifanya hivyo, hawajamaa wa jembena nyundo watashika adabu manake naona na wenyewe wameanza kupasha misuli.
 
mbona mwanza walikuja pia na tshirt, skafu, na kofia za kununua pia kuna watu walirudisha kadi za ccm wakapewa za chadema.
 
..ushauri wangu ni kwamba hotuba zao zilenge matatizo ya eneo husika.

..kama wako Geita wawaelimishe wananchi kuhusu ufisadi unasababisha wasifaidike na dhahabu iliyoko ktk eneo lao.

..wananchi lazima waweze kuunganisha madhila wanayoyapata na sera mbovu na ufisadi wa CCM.
 
Mkuu: Kauli za ccm wakati wa kampeni, ukipima na sasa hali ya nchi ilivyo utabaini ccm wako taabani, ccm imeipeleka nchi kwenye kaburi, kwa sasa Tz haiheshimiki kimataifa kwa nyanja zote kutokana na nchi kuendeshwa ovyoovyo na ccm, tumekichoka, mi imefikia hata nikio ofc zao najisikia kichefuchefu, tuamke jamani wakati ni huu wa mabadiliko.
 
Nawasifu sana CDM kwa kutoa elimu ya uraiya kupitia maandamano ya kanda ya ziwa.Ila kikubwa ninachowashauri wasisahau kugawa kadi za uanachama wa chadema.Huu ni wakati wa kupata wanachama wengi sana.Ni muhimu sana kuanza kuongeza base ya uanachama na kua nao wa kutosha.Wakifanya hivyo itasaidia sana kwenye chaguzi zijazo pia.Kingine wangeenda na Tshirts,kanga,kofia au magwanda ya chadema,wengi wanayahitaji.Hata kama hawana hela waende nayo wawauzie kwa bei nafuu.


Pia naomba Kamati Kuu ya CDM iangalie uwezekano wa kuanzisha TV station yao. Zilizopo zinaitumikia CCM hazikutaka kuonyesha maandamano ya Mwanza kwa kina.
 
Pia CDM wangefanya utaratibu angalau kwa nusu saa kwenye kila mkutano waoneshe kwa wananchi ile hotuba muhimu ya Baba wa Taifa aliyoitoa mwaka 1995. Ni hotuba nzuri mno na, kwa kweli naweza kusema, ilitabiri mambo yote ambayo yanatokea leo. Nina uhakika maelfu ya watanzania, hasa kizazi kipya na wale wa maeneo ya vijijini hawaikumbuki au baadhi yetu tumeisahau. Na hawa jamaa hutumia udhaifu huu wa watanzania wa kusahau wakijua baada ya muda mambo muhimu yatapita.

CDM lazima watumie mbinu zote sahihi kupambana na yule adui; kwa kweli nchi iko vitani hivyo mbinu zote lazima zitumike. Namshukuru mwanaJF mmoja alituwekea kipande cha hiyo hotuba humu jamvini jana (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/113302-nyerere-huyu-mzee-kiboko.html). Big-up LoyalTzCitizen‎.
 
Pia ningependa kukishauri chama,watumie suala la tofauti kubwa ya mishahara kama karata ya TURUFU,hili la baadhi ya wafanyakazi kulipwa MAMILIONI wakati wengine wakipata kilaki lina KERA SANA na kunasiku litazua BALAA NCHI HII,.CHOCHONDE CDM LISHUGHULIKIENI HILI MTAKUWA mmeisaidia sana jamii, kuhusu mishahara ya WABUNGE,kiukweli ni MIKUBWA,wabunge we2 jinasueni kwenye mtego huu,toeni percent flani kwa maendeleo ya majimbo yenu!
 
Back
Top Bottom