Ushauri wa bure kwa CHADEMA (tafadhali zingatia sana) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa bure kwa CHADEMA (tafadhali zingatia sana)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by commited, Jul 3, 2012.

 1. commited

  commited JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  ​Habari za usiku ndugu zangu! Natumaini kwa uweza wa Muumba wote mko salama, ninaushauri wa baadhi ya mambo kwa Chama kikuu cha UPINZANI(CHADEMA) Hasa kwa kile kinachoendelea bungeni. Najua viongozi, kama Mbowe, Zito, Mnyika, Lissu, Dkt K. Mkumbo mtapita huku na wengineo wengine zingatieni haya ili wananchi waweze kuwatofautisha nyinyi na Wakina Lusinde (CCM)

  1. Nimesikitishwa sana, tangu bunge hili limeanza wabunge wa CDM, wameshindwa kuelewa mikakati ambayo CCM, wameiweka. CCM wamejipanga kuhakikisha CDM haijadili tena kwa kina na kwa busara mada mbalimbali zinazo wagusa moja kwa moja wananchi.

  Na hilo CCM wanalifanya mahususi ili wananchi wapoteze imani na CCM waone mbona nao wako sawa tu kimawazo, na kimatendo tu kama CCM, Kwa sababu woote hawawatetei wananchi.. bali ni vijembe na vituko ndivyo wanavyoweza. CCM kupitia Spika pamoja na makada wake kama wakina Stella Manyanya, Chemba, Wasira,Lukuvi na hata baadhi ya Wabunge wa vyama vya CUF, NCCR au UDP, wamekuwa wakiwashambulia CDM waziwazi tena kwa shutuma zisizo na tija.

  Badala ya kueleza mikakati na hatua za kutatua matatizo ya wananchi kama vile kuhakikisha serikali inaboresha huduma za jamii, inatatua kero zamuda mrefu zinazo wakabiri wananchi, kupanda kwa mfumuko wa bei, kutekeleza kwa vitendo upunguzaji wa matumizi ya serikali, ili fedha zitakazopatikana zisaidie kuboresha miundombinu, pamoja na huduma za kijamii na nk, CCM imejipanga kuwatoa katika mstari CHADEMA, ili nao waingie katika malumbano tu.

  CCM na hao niliowataja wanafanya makusudi kukishambulia CDM, kwani wanajua wazi kwa sasa CDM, ndiye Mpinzani wake na wanamikakati mingi ya kukiangamiza kabla ya 2015(Ntaieleza siku nyingine). Wanachokifanya CCD na et al.. Ni kuwatupia CDM vijembe, na kebehi, ili CDM( WABUNGE) WAKASIRIKE, na hivyo kuhamaki na kutoka katika kujadili hoja na hivyo kuishia kuendeshwa na spika kwa kuomba miongozo, na utaratibu.

  Ninachowashauri jikiteni kujenga HOJA, hasa zile zenye maslahi kwa wananchi ili wananchi waweze kuwatofautisha nyinyi na Vyama vingine hasa CCM, Onyesheni Busara na hekima wakati mwingine kaeni kimya tu, angalieni mbele daima, acheni wakina Lusinde na wengineo waendeleze yao, ila nyinyi fanyeni muwezalo kuhakikisha mnazidi kujenga imani kwa wananchi kwa kuwasemea matatizo yao kila hoja inapokuja mezani. Msishindane na Tuhuma shindaneni kwa hoja, wananchi watawaamini sana, kwamba hata siku mkipewa nchi hamtaiuza au kufanya mambo kwa jazba kama serikali iliyopo inavyofanya. Muheshiwa Mbowe waeleze wabunge wako haya....

  2. CHADEMA, jihadharini sana na lugha kali, na za kuudhi muwapo majukwaani au mahali popote pale kwani zaweza kuwapelekea, kuonekana kama ni watu mnaotumia mabavu zaidi badala ya hoja na elimu. JITAHIDINI SANA wananchi wanataka kusikia sera zenu ni zipi, mtawasaidiaje ili rasilimali zilizopo ziwasaidie kutatua changamoto za maisha pamoja na kuwasaidia wao kumudu gharama za maisha zinazopanda kila wakati ambazo tayari JK zimeshamshinda na hana uwezo tena wa kukabiliana nazo tena

  3. Top layer ya Chadema na Wanachama woote naomba Msali sana KUMUOMBA MUNGU KWA DHATI awaepushe na kila aina ya hila zinazopangwa kwa ustadi mkubwa na maadui zenu, kupitia miongoni mwenu. Ili Mwisho wa siku msiweze tena kuzungumza lugha moja, hii miaka mitatu ijayo inaweza kuwa ndio mwisho wenu wa kuvuma, na kukubalika kwa chama katika jamii.

  Kumbukeni maadui wenu wa kisiasa na serikali yao yenye makachero takribani 250,000, na Watumishi wake vya vyombo vya usalama na nyadhifa mbalimbali takribani ya 400,000 hawatakuwa tayari ajira zao ziingie mchanga kirahisi kama mnavyodhani. Mtangulizeni Mungu kwa kila Jambo.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Well said,wl work for it.viva cdm!
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kitu kimoja tu ningezee. Sitowashauri Chadema wakae kimya na kuzungumzia maslahi ya wananchi tu bali pambaneni nao bila matusi kwa sababu hulka ya Watanzania mtu akishindwa kujibu akikaa kimyaa huonekana dhaifu japokuwa kapuuza.

  Kwa hulka Ya Mtanzania majibu laini na yenye mantiki ndio yanatakiwa na sii kukubali kupigiliwa msalabani..

  Iwe ni njama yao au sio, tatizo ambalo vyama hivyo havikulitazama ni pale wanaposhambulia mtoa hoja pasipo majibu nadhani Watanzania wengi wamelitazama bunge la jana na wamejua jinsi gani wabunge wa CCM wasivyokuwa na akili...

  Ushahiwi wa Chadema umeweza kuonyesha sura kamili za baadhi ya watu walokuwa wakiaminiwa, walokuwa wakithaminiwa kumbe wamejaa pumba kichwani.

  Nafasi kama hii waitumie vuzuri tu bila matusi na nguoni wala kulikimbia Bunge..
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Chadema wana haki ya kujibu mashambulizi yanayoelekezwa kwao na kamwe loyal opposition haiwezi kuwafikisha kokote
  kwani you go to war with the army you have and not the army you want.

  Kwahiyo mashambulizi ya CCM na MAKUWADI ZAO inabidi yajibiwe kwa kadiri yanavyokuja kwani its chadema against the stubborn regime.

  nakuunga mkono mkono kuhusu tactics mbaya wanazotumia CCM za kuwasimamisha watu kama manyanya watukane huku wakiwalinda ni game wanacheze lakini chadema haiwezi kukaa kimya tutapambana kwenye uwanja wao mpaka kieleweke. Walikuja hapa arusha na majeshi yao yote lakini tukapambana na tukawashinda.

  ENOUGH is ENOUGH.
   
 5. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,753
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Ahsante.Imetulia sana!
   
 6. t

  true JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Message sent mkuu! Chadema daima.
   
 7. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Waambie vile vile waache kuwa antagonistic as a matter of principle kwa kila tatizo na badala yake wawe na constructive criticisms.
  Hili la madktari wanalolishabikia wanaonekana kuwa wanashabikia mauaji ya wagonjwa mahospitalini.
   
 8. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Asante kamanda nadhani umeona mbali sana God bless chadema
   
 9. f

  fcharles2000 Member

  #9
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeongea vizuri sana!
   
 10. m

  majebere JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Huu ushauri si ungeupeleka kwa mtei, unaleta hapa ili iweje?
   
 11. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Wewe pia hutofautiani na Manyanya hakuna sehemu yoyote ambapo Chadema wameshabikia mgomo na ndomana wamepigania sana lijadiliwe Bungeni na spika akalitolea nje kwakivuli cha mahakama.
   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  ndugu cdm wanachotaka ni swala hili la mgomo lijadiliwe bungeni kwani watu wanaendelea kufa.

  Hivi unajua kama wabunge wa ccm wanasema hakuna mgomo wakati madaktari bingwa walitangaza mgomo?
   
 13. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Safi sana
   
 14. Delegate

  Delegate JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 35
  jana tulisikishwa sana sana na kitendo cha mwenyekiti felsta alivyojitahidi kuongea kwa jazba na hasira wakati anaongea na Mnyika,kwa kweli hii ni mipango ya kuwanyamazisha chadema lakini sisi wananchi tumegundua hilo,kama ccm wanakuja na hilo ili sisi tuwaone chadema hawafai basi wamegonga ukuta,huwezi kutumia dakika 4 kumshambulia mbunge mmoja huku ukimnyima nafasi ya kuongea
   
 15. S

  Shambano Member

  #15
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  <BR><BR>unawashwa nini? huu ushauri ni kwa ajili ya baba mwanahasha, mkwele, dakitari binwga wa watoto wanaopata ziro fomu iv katika shule bora<BR>
   
 16. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,633
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  asante great thinker!
   
 17. commited

  commited JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu Majebere unatambua uhuru wa kutoa maoni, au unatatizo gani... Tumia busara tafadhali....
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  ningependa kusema kama ulivyosema lakini niongezee tu kuwa lugha kali waendelee kuzitumia ieleweke si matusi.....
   
 19. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Soma magazeti ya leo na ushahidi uliotolewa kwa mikutano katika hoteli ya Drsert Palm na Dear Mama huko Dodoma.
  You are behind the news mkuu!
   
 20. commited

  commited JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  daah mkuu Crashwise... hii huwezi ona kama innaweza kuleta madhara kwa baadhi ya rika la jamii yetu kuona kuwa CDM wanatumia mabavu... na siyo kujenga hoja
   
Loading...