USHAURI WA BURE KWA CCM- Fr. Privatus Karugendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHAURI WA BURE KWA CCM- Fr. Privatus Karugendo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, May 15, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  SIKUTAKA kuimba wimbo mpya wa “Bongo” wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kujivua gamba. Ninaamini kwamba wimbo huu hauna tija kwa taifa letu. Watanzania wanahitaji maji, umeme, chakula, dawa, barabara, elimu na afya bora; kilio chao ni utawala bora na viongozi wao kuwajibika; wanataka waone maisha yanakuwa nafuu; bei ya sukari inatelemka, nauli linakuwa nafuu na vyakula vinapatikana kwa bei nzuri.

  Miaka hamsini baada ya uhuru Tanzania haina kitu chochote cha uhakika: hatuna umeme wa uhakika, hatuna maji ya uhakika, hatuna chakula cha uhakika, hatuna elimu ya uhakika na kule vijijini hakuna nyumba za uhakika. Hakuna malazi ya uhakika na hakuna vyoo; tumeshuhudia mara nyingi mashirika ya misaada kutoka nje ya nchi yakijenga vyoo vijijini! Porojo za kuvuana magamba haziwezi kutusaidia hata siku moja. Hivyo niliamua kutojiingiza katika nisiloliamini.

  Leo nimeamua kujiingiza katika mjadala huu usiokuwa na tija baada ya kuona CCM wanazunguka nchi nzima wakieneza uongo. Badala ya kukaa chini kutengeneza mkakati wa kuliokoa taifa letu, wanazunguka wakiimba wimbo wa kuvuana magamba wakati watuhumiwa wote wa ufisadi wanaendelea kustarehe na kufaidi jasho la Watanzania. Badala ya kutuelezea watafanya nini ili bei ya sukari iteremke, watafanya nini ili mgawo wa umeme umalizike, wanaanza kutuimbia wimbo wa Dk. Slaa na Mbowe ni mafisadi, eti wana mpango wa kuvuna fedha kutoka CHADEMA.
  Sina nia ya kuwatetea Dk. Slaa na Mbowe, sifa zao kwenye jamii ya Watanzania ni mtetezi tosha, ingawa hata nikiwatetea si dhambi! Naogopa kuhukumiwa na historia kwa kukaa kimya wakati mambo yanaharibika.

  CCM, wanatuambia kwamba Slaa na Mbowe, ni mafisadi. Hili linatusaidia vipi sisi wananchi kuboresha maisha yetu? Hili linasaidia vipi bei ya sukari kutelemka. Linasaidia vipi mafisadi walichota fedha zetu na kuziwekeza nje ya nchi kuzirudisha? Hili litasaidia vipi rais wetu kuwawajibisha viongozi wanaoshindwa kazi zao? Anawajua vizuri kwamba hawafanyi kazi, badala ya kuwawajibisha anawaimbia taarabu?

  Kama Slaa, angekuwa fisadi, basi tungeelezwa wakati wa uchaguzi mkuu. CCM ilijitahidi kwa nguvu zote hadi kufuatilia kanisani alikokuwa akifanya kazi, lakini haikufanikiwa. Ndipo wakaanza kufuatilia maisha yake binafsi. Huyu tunamfahamu, ni mzalendo, mchapakazi na mtu makini. Sasa wanatwambia kwamba ufisadi wake, anawalazimisha CHADEMA wamlipe mshahara milioni saba.
  Hata wakimlipa milioni hamsini, sisi wananchi inatuhusu nini? Hizo fedha za CHADEMA, zinachotwa benki gani? Kwani CHADEMA wanaongeza bei ya sukari ili wamlipe mshahara Dk. Slaa? CHADEMA wanatoa misamaha ya kodi?

  Eti Mbowe, anatafuta utajiri CHADEMA? Labda vijana wadogo wasiofahamu historia ya familia ya Mbowe. Huyu si masikini wa kutafuta utajiri kwenye chama; na wala hakuingia kwenye chama kutafuta utajiri kama wanavyofanya wengine. Kabla ya kuropoka, ni vyema vijana wa CCM wakafanya utafiti. Inawezekana yakawepo matatizo ya kiutendaji ndani ya CHADEMA. Inawezekana Slaa na Mbowe wakawa na udhaifu fulani kwenye uongozi wao ndani ya chama; hili linawezekana maana wao ni binadamu kama sote tulivyo. Hakuna binadamu aliye mkamilifu. Lakini kusema kwamba hawa ni mafisadi na kwamba wanatafuta utajiri kwenye chama chao ni upuuzi ambao tukikaa kimya bila kuweka mambo sawa tutahukumiwa na historia.
  Kutaka kumkomoa Slaa, kwa vile yeye ndiye bingwa wa kuibua hoja za mafisadi ni “utoto”, maana yeye anafanya hivyo kwa ushahidi. Mengi aliyoyaibua ni ukweli ambao na CCM imeungama hadi kufikia hatua ya kuvuana magamba. Fedha za EPA zilichotwa kweli, CCM inawafahamu Kagoda na inafahamu walichota fedha hizo kuzipeleka wapi. Tusiambiwe Slaa ni fisadi, bila ushahidi wa ufisadi wake.

  Slaa amechota fedha za umma wapi? Je, kule Karatu, alikokuwa mbunge zaidi ya miaka 15 anatuhumiwa kuchota fedha za umma? CHADEMA ni chama cha upinzani. Ni wazi lengo lake ni kushika dola. Hivyo daima kitajitahidi kuangalia kasoro ambazo zinachelewesha maendeleo na kuwaeleza wananchi.

  Kasoro kubwa ya serikali ya CCM ni kushindwa kulinda rasilimali za taifa letu; ni kuwaachia watu wakachota fedha za umma bila kuchukua hatua zozote zile; na ugonjwa sugu wa kulindana. Maandamano ya CHADEMA na mikutano yao ni kulenga kuwaelewesha wananchi yale ambayo CCM limeshindwa kuyatekeleza. Hivyo utakuwa ni ujinga na kutofikiri CCM nayo kujibu hoja hizo kwa maandamano na mikutano.


  Tulitegemea CCM ambacho ni chama kikongwe, kina wazee wenye busara na hekima kingejibu hoja za CHADEMA kwa matendo: Mafisadi wote wafukuzwe kwenye chama na kufikishwa mbele ya sheria. Fedha zetu walizoiba wazirudishe, ikishindikana basi mali zao zitaifishwe. Mikataba mibovu ishughulikiwe, misamaha ya kodi ifutiliwe mbali. Mawaziri wanaoshindwa kazi wafutiliwe mbali. Unafuu wa maisha uonekane; mfumuko wa bei utafutiwe jibu.

  Kama nilivyoanza makala hii ni kwamba wananchi wanataka unafuu wa maisha; wanataka kuona umeme unawaka, wanataka bei ya sukari itelemke, wanataka nauli itelemke, wanataka watoto wao wasome elimu ya juu bila matatizo ya kutopata mikopo na mengine kama hayo. CCM, wakitaka kufanikiwa katika harakati zao za kukijenga chama na kukipatia sura mpya; wakae chini na kutengeneza mikakati ya kushughulikia kero za wananchi. Bila matendo na kuendelea kutuimbia taarabu wanachochea hasira za wananchi.

  Fedha wanazozitumia kuzunguka nchi nzima ni za wananchi. CCM kama chama, hakina fedha zake kama vilivyo vyama hivi vya upinzani. Hiki kilikuwa chama kimoja cha siasa; utajiri wake wote umetokana na serikali; umetokana na kodi za wananchi wote wa Tanzania.

  Mali zote walizokuwa nazo chini ya serikali ya chama kimoja, baada ya kuingia mfumo wa vyama vingi walikimbia nazo: Viwanja vya michezo, majumba, magari na mengine mengi. Anayepinga asimame na kuonyesha mali za CCM kama chama cha siasa. CCM ni chama kinachoongoza serikali yetu, iwe kwa kuchakachua au kwa kuchaguliwa, ndiyo ukweli kwamba kikatiba ndicho chama kinachotawala.

  Hivyo kila mtu anayejali uhai wa taifa letu hawezi kukaa kimya na kuwaachia hawa watawala wetu waendeleze porojo na kutuimbia taarabu wakati wananchi wanateseka kwa maisha magumu. Hatutaki kusikia ufisadi wa Slaa na Mbowe, maana hawa hawajashika dola, wakishika wakawa mafisadi tutawawajibisha, sasa hivi tunataka kusikia usafi wa viongozi wetu, tunataka kusikia mapacha watatu wako Segerea, tunataka kusikia maisha bora kwa kila Mtanzania.

  Ni ushauri wa bure na kwa nia njema kabisa!

  Tanzania daima
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  PHP:
  Hivyo kila mtu anayejali uhai wa taifa letu hawezi kukaa kimya na kuwaachia hawa watawala wetu waendeleze porojo na kutuimbia taarabu wakati wananchi wanateseka kwa maisha magumuHatutaki kusikia ufisadi wa Slaa na Mbowemaana hawa hawajashika dolawakishika wakawa mafisadi tutawawajibishasasa hivi tunataka kusikia usafi wa viongozi wetutunataka kusikia mapacha watatu wako Segereatunataka kusikia maisha bora kwa kila Mtanzania

  Hii imetulia
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  yafaa magazeti yote kesho yatoe kama press release from peoples of tanzania!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  HTML:
   
  Miaka hamsini baada ya uhuru Tanzania haina kitu chochote cha uhakika: hatuna umeme wa uhakika, hatuna maji ya uhakika, hatuna chakula cha uhakika, hatuna elimu ya uhakika na kule vijijini hakuna nyumba za uhakika. Hakuna malazi ya uhakika na hakuna vyoo; tumeshuhudia mara nyingi mashirika ya misaada kutoka nje ya nchi yakijenga vyoo vijijini! Porojo za kuvuana magamba haziwezi kutusaidia hata siku moja. Hivyo niliamua kutojiingiza katika nisiloliamini
  This is too much a truth, hadi inasababisha moyo kubadili mapigo!
  Mafisadi ndio wanaotamba na hela za serikali yetu!...na wengine wana damu ya kigeni!
  Any sniper out there?
   
 5. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kila mbuzi anakula kwa usawa wa kamba yake! Gap la walio nacho na wasio nacho linazidi kuongezeka!
  Mungu ibariki Tanzania.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  PHP:
  Mali zote walizokuwa nazo chini ya serikali ya chama kimojabaada ya kuingia mfumo wa vyama vingi walikimbia nazoViwanja vya michezomajumbamagari na mengine mengiAnayepinga asimame na kuonyesha mali za CCM kama chama cha siasaCCM ni chama kinachoongoza serikali yetuiwe kwa kuchakachua au kwa kuchaguliwandiyo ukweli kwamba kikatiba ndicho chama kinachotawala
   
  Ndipo ufisadi ulipoanza kupenyeza mizizi, leo hata hawajui wapi walikoanza kuvua gamba la unyerere, na hivi gamba wanalosema wanajivua hawalijui ni gamba gani.
   
 7. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,964
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Kweli imekaa vizuri, lakini nadhani CCM ni sikio la kufa .............................
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Huyo ndio Padre Privatus karugendo.

  Imetulia na nimeipenda sana na kama CCM wataifanyika kazi basi angalau maendeleo yataonekana na wakiipuuzia basi mauti ndio hukumu yao 2015.
   
 9. Guyton

  Guyton JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Imekaa vizuri.
  Napendekeza kabla ya uchaguzi kuwe na form ya maswali ya kuyajibu, marks anazopata mtu iwe ndo percentage ya kula yake, ila wakina Tambwe wapate zero, kula zao zisihesabiwe, labda itasaidia.
   
 10. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  go tanzanians go! ni nchi yetu. hatuna nchi nyingine duniani. ni wakati wetu kuirudisha tz kwetu na c kwa wachache na mafisadi
   
 11. luck

  luck JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2011
  Joined: Oct 3, 2009
  Messages: 768
  Likes Received: 283
  Trophy Points: 80
  yafaa tujiulize, nyoka akijivua gamba ndio anabadilika nini?
   
Loading...