Ushauri wa bure: Dkt. Mashinji hamia CCM

Team JPM

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
1,074
1,608
Ukatibu mkuu wa chama ni nafasi nyeti na ya juu sana katika uongozi wa chama, kwa nafasi hiyo, katibu mkuu huzifahamu siri nyingi na nyeti za chama, mwenyekiti pamoja na viongozi wengine.

Kuenguliwa kwenye uongozi katika chama katika umri ambao bado una nguvu, nia na uwezo wa kuendelea kukitumikia chama na Taifa, sio salama.

Kwa siasa zetu zenye figisu na hila nyingi, Mh. Mnyika na Mbowe hawawezi kuwa huru na Amani ikiwa msiri wao (Mashinji) bado yupo hai na hajarizishwa na mambo kadhaa ktk chama.

Sio rahisi chadema iruhusu Mashinji apate ubunge au nafasi nyingine ya uongozi kwa kuhofia kwamba anayajua mengi kuhusu chama, uongozi na viongozi wake.

Kwa mantiki hii, Namshauri DKT Mashinji ahamie CCM ili kujikinga dhidi ya maadui ambao walikuwa marafiki.

DKT Mashinji asisubirie kuhujumiwa na Chadema ndipo ahame, atumie fursa hii. Waswahili wanasema 'Udongo uwahi, ungali maji'. Karibu C.C.M DKT MASHINJI.
 
Mashinji alipwaa,kuanzia1 sokis,nepi mpaka kofia,Ukimuuliza hata mwanao katibu mkuu wa chadema anaitwa nani?hawezi kukujibu,hata wewe mleta mada ghafula tungekuuliza hilo swali usingeqeza weza kulijibu mpaka ungeiia kwenye mtandao.
 
Kujua siri za cdm ni km kujaribu kuvaa kiatu sawa na mtu wakati mguu wake unakua as days pass on
 
I smell something fishy....mnampango wa kummdhuru nn mbona unaongea tungo tata? Asipohamia ccm mumdhuru halafu mseme chadema wamefanya hivyo.
 
Uzi dhaifu Sana unaoenda kutufungia mwaka wa watu wa hovyo kabisa 2019.

Mtu kutoteuliwa kuendelea kuongoza Chama Ni Dhambi?

Daah hizi Ni akili za kijinga kabisaa. Mwanaume msimamo kuhama hakusaidii zaidi ya kuonekana dhaifu tu.
Yani mkuu unataka Wanawake Kama Wema sepetu wafanye kiki za kuhama chama na Mwanaume kama Mashinji nae afanye hivyohivyo kweli!!

Ushauri wangu: Dr Mashinji Kama kweli PhD yako siyo ya kuungaunga Fanya kubaki hukohuko uliko no matter how it takes.

Remember: Revenge does not change the past.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja, CCM ndio mpango mzima kwa 2020.

P
Je CCM ndio mpango mzima au Magufuli ndio mpango mzima?
 
Je CCM ndio mpango mzima au Magufuli ndio mpango mzima?
Hili swali hata mimi niliwahi kuuliza humu
P
 
Naunga mkono hoja, CCM ndio mpango mzima kwa 2020.

P
Huwa na kufananisha na mwandishi mmoja wa Makala za Siasa,Kila akitaka kunukuu and nukuu Kitabu chake😀😀...nawe katabia kako hiki,Kila kitu lazima uturejeshe kwa Maandiko yako...uandishi huu unaniboa Mimi ,Ni dalili za ubnafsi na ushamba wa kisomi!Sisi tulio ishia Darasa la Saba tunapenda kujifunza kutoka Kona mbalimbali...bila Shaka huu hizi Ni dalili za kupenda au kushabikia udikteta!
 
Back
Top Bottom