Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,635
- 29,508
Kwema Wadau,
Kipindi hiki kila Mkoa tunasikia Serikali na Polisi wakikamata Pombe iliyoharamishwa na serikali ya Viroba. Kila mahali na kila siku habari ni hizi hizi. Kamata kamata hii inafuatia agizo la Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kutangaza kupiga marufuku Pombe hii kwa sababu za kiafya na za kimazingira. Agizo hili lilitolewa mnamo tarehe 17th February 2017 kwamba ifikapo tarehe 01st March 2017 (12 days notice) watazuia uuzwaji na usambazaji wa pombe hii.
Nimejaribu kuwaza kwa siku hizi 12 hawa waagizaji, watengenezaji na wauzaji wangefanya nini labda. Manake Hata Watengenezaji wa hivi Viroba wakisitisha uzalishaji, bado kwenye mzunguko viko viroba vingi sana vilivyonunuliwa kwa halali kabisa ambavyo kuisha kwa siku hizo 12 ilikua ni ngumu sana.
Nachojiuliza kama ni kua kama kwetu Tanzania viroba vimekua haramu, kwanini basi usifanywe utaratibu wa kuvipeleka Viroba hivyo nje ya nchi vikauzwe huko kurudisha angalau gharama (kupunguza hasara)?? Hivi kipi bora, wafanyabiashara wanyang'anywe viroba vikatupwe wale hasara 100% au voizwe nje ya nchi ambako huko sio haramu angalau wapunguze hasara??
Viroba hivi vikipelekwa nje vikauzwa huko kutakua na faida mbalimbali. Hizi faida ziko nyingi sana ila hapa nataja zile zinazhusiana na hili swala letu tu kama vile Kuiingizia nchi fedha za kigeni, kuimarisha "balance of trade" ya nchi, kutengeneza soko la bidhaa zetu, Kuitangaza nchi yetu, etc.
Kuna sheria zinatungwa lakini zisiwe mwiba kwa Wananchi kwani Wazalishaji na Wafanyabiashara hawa ni walipa kodi na hutegemea Biashara zao kuendesha maisha yao, kusifanyike mambo ya kukomoana kwa kisingizio cha sheria wakati sheria zimewekwa kwa ajili ya wananchi.
Ushauri wangu ni huu tu.