USHAURI: Usijiloge ukaomba mkopo wa bodi ya mkopo

USHAURI: Usijiloge ukaomba mkopo wa bodi ya mkopo

15% ya basic salary na hapo hujaweka nyengeza zao za deni... mfano unatakiwa kulipa 10mil unakuta unadaiwa 12mil.
Kwenye mshahara wako unabakiwa na kiasi gani baada ya makato ya Loan Board Mkuu? Tafuta vyanzo vingine vya mapato, usitegemee mshahara tu utaleta mada nyingi sana hapa zaq malalamiko.
 
Brother Upepo wa Pesa nakuheshimu sana kwa mada zako ila kwa hili umekosea sana.
Maisha ya chuo bila mkopo ni magumu sana tena sana haswa ukitoka kwenye familiia zetu hizii za kitanzania.
 
Once ukiingia ktk government system makato hayakwepeki tunachokuja kutofautiana ni kiasi kinachokatwa na serikali but kukaa kutegemea mshahara wako kama chanzo chako cha mapata ni ujinga na umaskini unaanzia apo...

Ushauri wangu fursa kama hzo za mikopo zikija zitumie vizur kwa kuwekeza japo wanafunz wengi wa vyuo pesa ya mkopo wanafanyia sana starehe...wanakuja kustuka kama walifanya makosa wakiwa mtaani au maofisini so nakuanza kupanic kama huyo apo bro mleta Uzi huu..
 
Brother Upepo wa Pesa nakuheshimu sana kwa mada zako ila kwa hili umekosea sana.
Maisha ya chuo bila mkopo ni magumu sana tena sana haswa ukitoka kwenye familiia zetu hizii za kitanzania.
Yaan mtoa mada anafananisha kupewa mshahara ambao ni pungufu labda laki moja, na kutopewa kabisa boom na ada, + meals and accomodation
 
Babaa ilo deni haliishi kamwe!!

Kila mwaka kuna riba yaongezeko la thamani.

Ndio maaana kinachoonekana kwenye salary slip ya mdeni na kile kilichiko kwenye system ya loan bord ni Vitu viwili tofauti!

So ukikatwa kwenye salary slip likaisha unapewa mwaka mmoja wa mapumziko then ngoma inaanza tena!!

So hilo deni ni for life.

Kama mtu unao uwezo wakujilipia jilipie, huu ni msalaba hata yesu hawezi kukuokoa!!!
So mwenye mkopo atapata 450000 na asiye na mkopo atapata 553000.

Unahisi hiyo difference ni significant kiasi kwamba mtu asote miaka 3 chuo akijilipia ada 1m + , akijilipia gharama za field, na gharama za kuishi, wakati akitoka familia za maisha ya chini au maisha ya kati?

Pia, kwa tofauti hiyo, maisha ya hao wawili hayatakuwa na significant difference kubwa.
 
Acha kuwatisha wenzako hakuna pesa tamu kama pesa za loan board
Nikikumbuka siku niliyoingiziwa katika account yangu laki 9 za field sisahau
 
Sasa na hili ni swali unataka nikujibu kweli?
kiufupi wapo wazazi wenye uwezo mkubwa tu wa kuwalipia vijana wao ada bila wasiwasi wowote ambapo nao pia uhapambana kuhakikisha kijana anapata mkopo, na pia wapo ambao mbali tu ya mkopo wao ata ile nauli ya kumpa kijana aende chuo alichopata ni issue, kijana hyu ukimwambia asiombe mkopo ni sawa na kumwambia aache chuo, so ushauri wako nadhan ungejikita kwa wale wenye uwezo wa kujilipia.
 
Unatakiwa kuwa makini sana na ushauri unaompa mtu aliyetoka six na anaenda chuo, bila kumpa coution; kwa sababu wengi hawayajui maisha ya chuo, so unaweza kumuambia asiombe na yeye akakuelewa, kumbe hajajua gharama halisi za maisha atakapokuwa chuo + gharama za ada ambazo mara nyingi ni zaidi ya millioni moja.

Pia wengine wanaweza kuwa na mtu wa kuwasaidia leo; lakin hakuna aijuaye kesho yake, pengine anayekupa msaada akaacha kukupa kwa sababu kama kifo, kufirisika au kukosana.

Nilipokuwa chuo niliyaona maisha ya watu wengi wasiyo na mkopo yalivyokuwa magumu, hasa kwa wale ambao wazazi wao si matajiri na wale ambao sehemu walizozitegema mwanzo kupewa pesa, zimeharibika. Hichi kitu kiliathiri sana performance zao kwenye masomo.

Hivyo basi mtu atakayefuata ushauri wako ahakikishe yafuatayo:
1. Anavyanzo vya uhakika cha pesa

2. Apige gharama halisi za chuo pamoja na gharama za maisha ambazo ndiyo tatizo kubwa kwa wanachuo
Kweli mkuu
 
Wanafunzi wengi wanapoa apply chuo jambo la kwanza wanaanza kuuliza kozi hii nitapata mkopo asilimia mia?

Kwa ushauri wangu, wewe kama ni mwanafunzi unajiandaa kuanza chuo kaa mbali kabisa na mkopo wa loan board!!

Unaweza ukawa unafurahi kupata laki sita au laki nne za mkopo kila semester ila majuto yake utakuja kuyaona ukisha maliza chuo!!

Bora usome kwa msoto miaka mitatu/minne/mitano chuo kuliko kuja kuishi kwa msoto uki maliza chuo!!

Najua unayeanza chuo WENDA usinielewe namaanisha nini ila utakuja kunielewa/kunishukuru uki maliza chuo na kuanza kazi!!

Narudia tena ... Kaa mbali na mkopo wa loan board!!
Serious ? Msomi una rise mada kama hii ? Watu hawana uwezo wa kujilipia unategemea watasomaj, wasisome kwasab makato ni makubw or ?
 
Ni kweli kbs mambo ya loan board ni hasara baada ya kumaliza chuo hasa kwa wa course za science lkn ni jambo la mtu kuangalia Kama uwezo upo hta Kama co wa kuridhisha Sanaaaa kheri ukapambana usipate hilo janga kuzipata hizo Hela raha lkn hakuna Hela ya bure.... Tatizo mtu anaingia chuo alafu anabadilika kwasababu ya kutaka kufanana na flani tatizo hili
Wanafunzi wengi wanapoa apply chuo jambo la kwanza wanaanza kuuliza kozi hii nitapata mkopo asilimia mia?

Kwa ushauri wangu, wewe kama ni mwanafunzi unajiandaa kuanza chuo kaa mbali kabisa na mkopo wa loan board!!

Unaweza ukawa unafurahi kupata laki sita au laki nne za mkopo kila semester ila majuto yake utakuja kuyaona ukisha maliza chuo!!

Bora usome kwa msoto miaka mitatu/minne/mitano chuo kuliko kuja kuishi kwa msoto uki maliza chuo!!

Najua unayeanza chuo WENDA usinielewe namaanisha nini ila utakuja kunielewa/kunishukuru uki maliza chuo na kuanza kazi!!

Narudia tena ... Kaa mbali na mkopo wa loan board!!
 
Ushauri ni mzuri ila naona umefeli jinsi ya kuufikisha! Huwezi kuwaambia vijana wasiombe mkopo eti wasome kwa msoto. Hivi huko kusoma kwa msoto hutakiwi kulipa ada?hutakiwi kulipa kodi ya pango?hutakiwi kula? Ni bora ungewapa angalizo kwamba mtu kama anajua wazazi wake wana uwezo wa kumsomesha ni bora asiombe,sio kuwaambia tu wote waache kuomba!
Mimi nimekuwa mnufaika wa bodi ya mikopo na ndo imeniwezesha kumaliza masomo yangu na hadi kupata kazi. Hadi Leo ninashukuru Mungu vinginevyo ndoto zangu zingeishia kidato cha sita tu. Familia zetu wengi hazina uwezo wa kulipia gharama za masomo ya elimu ya juu.
 
Back
Top Bottom