Ushauri: Ununuaji wa magari

CIF2,000 USD3,240,700 TZS
Import Duty500 USD810,175 TZS
Dumping Fee500 USD810,175 TZS
Excise Duty150 USD243,053 TZS
VAT567 USD918,738 TZS
Total Taxes1,717 USD2,782,141 TZS
Port Charges150 USD243,053 TZS
L/Shipping Line75 USD121,526 TZS
Total Cost
3,942 USD6,387,420 TZS

Hiyo ndo estimate cost kama umenunua leo 30/6/2011.Bado Bima na usumbufu wa jamaa wa TRA..
mkuu! thanks kwa info. hivi taasisi gani ambazo zina pata nafuu ya hizi kodi zote?
 
Wana JF,

Kuna ndugu wa karibu ambaye anataka kununua gari lililotumika toka Uingereza na kulipeleka Tanzania. Kaniomba ushauri kuhusu namna ya kufanya au kama ninamfahamu dealer yeyote anayejihusisha na biashara hii. Bahati mbaya sijawahi agiza gari toka Uingereza na sijui dealer yeyote aliyepo Tanzania.

Nilishawahi kuambiwa kwamba magari mengi yauzwayo toka Uingereza huwa hayawi na ubora sawa na picha za kwenye mtandao, yaani yanaweza yakawa machakavu zaidi ya yalivyooneshwa na pia ati ni ghali kununua gari Uingereza ukilinganisha na kununua Japan.

Sijajua kama hivi vitu ni kweli, ila viliniogopesha toka mwanzo. Sasa tupeane ushauri kutokana na uzoefu wa watu walioagiza magari yao Uingereza, na pia kama kuna dealers wowote wanaojihusisha na uuzaji wa magari toka Uingereza (na hata Ulaya kwa jumla) naomba tufahamishane.
 
Una mtu unayemwamini UK? Kama yupo chagua gari kwenye mtandao wa autotraders UK ila uwe na tumia post code ya UK ya huyo mtu, then mtume huyo mtu akalikague kabla hujatum, a pesa, kuna makampuni ya wa Tanzania UK wanasafirisha magari na vifaa vingine
 
Wana JF,

Kuna ndugu wa karibu ambaye anataka kununua gari lililotumika toka Uingereza na kulipeleka Tanzania. Kaniomba ushauri kuhusu namna ya kufanya au kama ninamfahamu dealer yeyote anayejihusisha na biashara hii. Bahati mbaya sijawahi agiza gari toka Uingereza na sijui dealer yeyote aliyepo Tanzania.

Sijajua kama hivi vitu ni kweli, ila viliniogopesha toka mwanzo. Sasa tupeane ushauri kutokana na uzoefu wa watu walioagiza magari yao Uingereza, na pia kama kuna dealers wowote wanaojihusisha na uuzaji wa magari toka Uingereza (na hata Ulaya kwa jumla) naomba tufahamishane.
Angalia WWW.AUTOTRADER.CO.UK kuna aina ya kila gari.Ungekuwa huko UK ningekushauri pia utembelee auctions

Nilishawahi kuambiwa kwamba magari mengi yauzwayo toka Uingereza huwa hayawi na ubora sawa na picha za kwenye mtandao, yaani yanaweza yakawa machakavu zaidi ya yalivyooneshwa.
Si Uingereza tu, Hili tatizo lipo kila nchi kwa sababu madhumuni ni kuuza gari, wataweka picha za sehemu itakayo kuvutia.

However Mwaka wa gari, mileage, picha na wengine wanaweka maelezo gari ilikuwa inatumika kwenye mazingira ya aina gani vita kusaidia kukupa hali halisi ya gari

na pia ati ni ghali kununua gari Uingereza ukilinganisha na kununua Japan.
Inategemea na aina ya gari.Kwa mafano,Scania na Jaguar ni rahisi UK kuliko Japan lakini ukinunua Land Cruiser kutoka UK kuna uwezekano kwa asilimia kubwa utakuwa umeingia choo cha kike
 
Una mtu unayemwamini UK? Kama yupo chagua gari kwenye mtandao wa autotraders UK ila uwe na tumia post code ya UK ya huyo mtu, then mtume huyo mtu akalikague kabla hujatum, a pesa, kuna makampuni ya wa Tanzania UK wanasafirisha magari na vifaa vingine
Yeah, nina vijana Milton Keynes na London.
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Angalia WWW.AUTOTRADER.CO.UK kuna aina ya kila gari. Ungekuwa huko UK ningekushauri pia utembelee auctions

Si Uingereza tu, Hili tatizo lipo kila nchi kwa sababu madhumuni ni kuuza gari, wataweka picha za sehemu itakayo kuvutia.

However Mwaka wa gari, mileage, picha na wengine wanaweka maelezo gari ilikuwa inatumika kwenye mazingira ya aina gani vita kusaidia kukupa hali halisi ya gari

Inategemea na aina ya gari. Kwa mfano, Scania na Jaguary ni rahisi UK kuliko Japan lakini ukinunua Land Cruiser kutoka UK kuna uwezekano kwa asilimia kubwa utakuwa umeingia choo cha kike

Asante sana mkuu, umenipa elimu ya kutosha
 
Hayo magari ya UK, vipi kuhusu spare zake? Hapa bongo zinapatikana? Mfano, BMW au Volkswagen Polo, hapa bongo spare zake zipo za kutosha jamani. Mwenye fununu anisaidie kwasababu mimi mwenyewe nilikuwa nataka Volkswagen polo toka UK au Japan. Msaada please!
 
Advise from personal experience:

Ingia website za autotraders kama ambavyo wengi wameshauri hapo juu, angalia gari unayopenda, then uwe na mtu kule akalithibitishe then ulipie, dealers wengi wanataka pounds cash. Kuhusu kutuma kua kaka yake Dewji yuko London ndio kazi yake miaka mingi, sikumbuki website yake, anatuma magari Tanzania na ni mwaminifu sana.

Kuhusu spare zipo nyingi ingawa inategemea na aina ya gari, mfano Quanshai ni gari latest na zipo kule hapa Tanzania ukileta zitasumbua maana hakuna spare hadi uagizie nje.

Nadhani nitakuwa nimekusaidia sana.
 
Naomba kuuliza wadau, kama gari zinazouzwa yard, Dar zipo za kuaminika. Napata shida sana nikiwaza kuagiza gari (used) toka Japan au kwingineko kwa kuwa muda wa kusubiria ni mrefu sana. Naomba kama kuna mtu ana info ya mahali Dar, naweza kupata gari za kuaminika na bei reasonable.
 
Inategemea unanunua gari ya aina gani kama ni saloon za Japan nenda show room tu zipo nyingi so utapata unayotaka kwa bei nzuri na imara kama ni 4x4 au European car agiza tu mwanawane
 
Mimi siziamini sana show room za bongo. Naona bora mtu uagize tu gari. Utaepuka mengi
 
Inategemea, zipo show rooms reliable na fake. Just like yapo makampuni reliable na fake huko Japan. Vilevile inategemea uhitaji wako gari ya yard unaipata on the spot (intact bila kuibiwa redio etc) ya kuagiza ni kati ya wiki 6 mpaka miezi 3(utaibiwa redio etc). Nawaaminia YOKOHAMA Kimweri road Namanga) na JAZMAK (next to Shoppers) katika yards za Bongo.
 
Nami naomba niulize hapo hapo. Je ukinunua pale yard kuna faida nyingine zaidi ya kusave time, kutokuibiwa baadhi ya vifaa nk? Mfano vipi bei, kulinganisha na kuagiza moja kwa moja? Kuna tofauti kubwa sana?
 
Naomba kuuliza wadau, kama gari zinazouzwa yard, Dar zipo za kuaminika. Napata shida sana nikiwaza kuagiza gari (used) toka Japan au kwingineko kwa kuwa mda wa kusubiria ni mrefu sana. Naomba kama kuna mtu ana info ya mahali Dar, naweza kupata gari za kuaminika na bei reasonable.

Ipo yard moja naifahamu ina gurantee ya miez 6 na bei zao ni resonable sana. Mimi nilinunua Spacio old model mil 11.mpaka leo haijanisumbua.nilipofanya research ya yard ingine bei zilikuwa juu na hamna guarantee. Na nilipo calculate tofauti ya kuagiza na kununua nikakuta ni pesa ndogo sana. Hivyo inategemea wewe unataka nini.
 
Nami naomba niulize hapo hapo. Je ukinunua pale yard kuna faida nyingine zaidi ya kusave time, kutokuibiwa baadhi ya vifaa nk? Mfano vipi bei, kulinganisha na kuagiza moja kwa moja? Kuna tofauti kubwa sana?

Faida ipo. Tatizo kubwa la kuagiza mwenyewe ni ushuru mzito. Hawa jamaa kwa kuwa ni regular importers hupata namna ya kulipa ushuru nafuu. Vilevile suala la storage charges halipo kwa kuwa wao wakitoa gari melini straight kwenye yard. Ukiagiza mwenyewe linalala bandarini each day $50. Ukikwama ndio hivyo tena. Halafu gari la yard una uwezo wa kulikagua wewe mwenywe unlike la internet unonyeshwa a doctored picture. Ni muhimu uende na fundi wako mlikague na ulitest mpaka uridhike
 
Mwenyewe nataka niwauzie jamaa flani wana yard yao kimeo changu cha 1996. Karibu Dar es Salaam.
 
CAMARADERIE,

Mkuu siku hizi bondage warehouse ni nyingi sana yani gari ikifika tu unapigiwa simu siku hiyo ukaichukue . Manji anakula sana shavu hilo. Juzi tu nimeagizia gari imefika Dar imekaa wiki mbili kwenye foleni ya kushusha but siku ilyoshushwa the same day nilipigiwa simu. Nikawa nimepewa 3 days za kutoa na vinginevyo wataanza kucharge warehousing fee. Niliitoa siku hiyo hiyo pale Chang'ombe mkuu.
 
Suppose umepigiwa simu na huna hela? Kumbuka Manji et al hupata faida kutokana na hizo storage fees. Hakuna bure hapo. Yard haiwezi kukucharge storage hata kidogo
 
Hebu nenda pale sinza palestina (baada ya msikiti) kuna yard zipo gari kama 10 hivi nadhani ni bei ila usiludi kutuuliza mafundi wazuri wanapatikana wapi
 
Mkuu siku hizi bondage warehouse ni nyingi sana yani gari ikifika tu unapigiwa simu siku hiyo ukaichukue . Manji anakula sana shavu hilo. Juzi tu nimeagizia gari imefika Dar imekaa wiki mbili kwenye foleni ya kushusha but siku ilyoshushwa the same day nilipigiwa simu. Nikawa nimepewa 3 days za kutoa na vinginevyo wataanza kucharge warehousing fee. Niliitoa siku hiyo hiyo pale Chang'ombe mkuu.

Well said, mie mwenyewe kamkweche kangu (Noah) nilitoa hapo hapo Chang'ombe last week. SIku hizi wako kasi kidogo kuyatoa, tofauti na zamani.
 
Back
Top Bottom