Mkyamise
JF-Expert Member
- Apr 14, 2014
- 526
- 677
Habari za leo waungwana? Naomba ushauri. Assume wewe ni mtoto wa kiume uliyezaliwa nje ya ndoa. Ikatokea ukafunga ndoa. Mkiwa kwenye sherehe ukumbini, MC akakutaka uwatambulishe ndugu zako. Hapo ukumbini yupo baba yako mzazi, mama yako mzazi, mama yako wa kambo na ndugu wengine. Sasa huyu mama wa kambo utamtambulisha kama nani? Kumbuka hutakiwi kumtambulisha kwa lugha au neno litakalomuudhi au kuleta ukakasi ili kidumisha mahusiano. Asanteni.