Ushauri: Unamtambulishaje mama wa kambo?

Ushauri: Unamtambulishaje mama wa kambo?

Kama mahusiano si mazuri, naanza na Mama yangu, nitakuwa nimemtonya baba kwamba nikimtambulisha asimame na mkewe. Kama mahusiano ni mazuri, nitasema nina bahati ya kuwa na mama 2 au 3, na kuwatambulisha kwa kuanzia na mama yangu.
Hapa unamdhalilisha mzee ndg yangu. Kwanini uiambie hadhara waziwazi kuwa unao mama wawili? Si utauonyesha umma kuwa dingi ni mchepukaji?
 
Hapo kwanza nita acha Ku assume,
Halafu utambulisho wangu utaaza kama ifuatavyo.
SALAMU,,,ndugu wageni wahalikwa ,mabibi na mabwana__
Asalaaam alekhum,
Kristo,
Bwana YESU asifiwe,
Kwa maajina ,(bwana harusi unataja majina yako)
Unatoa ukaribisho na kuendelea ,
Ningependa kutambulisha ndugu zangu ambao ni,kwanza
Baba yangu mzazi na mama yangu mzazi kwa pamoja wasimame wapunge mkono,,
Pacha wangu (kama unaye) asimame apunge mkono.

Unaendelea_mama zangu wadogo wote walipo wasimame wapunge mkono,
Baba wadogo, wasimame wapunge mkono,
Dada zangu wasimame wapunge mkono
Kaka zangu wasimame wapunge mkono,


Unamaliza wote kwa staili hiyo,
Angalizo ,,babu na bibi zako na shangazi Mkubwa watabulishe kipekee siyo kima fungu.

Huyo mama wakambo kama hakusimama na kupunga mkono ulipo watambulisha mama wodogo zako ukumbini hapo,asikulaumu.


Over&out
Ndugu yangu Juniour Lecturer huyu mama wa kambo akigoma kisimama kwenye kundi la mama wadogo?
 
Hapo kwanza nita acha Ku assume,
Halafu utambulisho wangu utaaza kama ifuatavyo.
SALAMU,,,ndugu wageni wahalikwa ,mabibi na mabwana__
Asalaaam alekhum,
Kristo,
Bwana YESU asifiwe,
Kwa maajina ,(bwana harusi unataja majina yako)
Unatoa ukaribisho na kuendelea ,
Ningependa kutambulisha ndugu zangu ambao ni,kwanza
Baba yangu mzazi na mama yangu mzazi kwa pamoja wasimame wapunge mkono,,
Pacha wangu (kama unaye) asimame apunge mkono.

Unaendelea_mama zangu wadogo wote walipo wasimame wapunge mkono,
Baba wadogo, wasimame wapunge mkono,
Dada zangu wasimame wapunge mkono
Kaka zangu wasimame wapunge mkono,


Unamaliza wote kwa staili hiyo,
Angalizo ,,babu na bibi zako na shangazi Mkubwa watabulishe kipekee siyo kima fungu.

Huyo mama wakambo kama hakusimama na kupunga mkono ulipo watambulisha mama wodogo zako ukumbini hapo,asikulaumu.


Over&out
Ndugu yangu Junior Lecturer huyu mama wa kambo akigoma kusimama kwenye kundi la mama wadogo?
 
Mbona easy tu, we sema "namtambulisha mke wake baba"

Hapo utakuwa umemaliza kazi
 
Mama mkubwa kama mama yako ndio alipindua shilingi ya baba yako, kama yeye ndio alipindua sent ya mshua wako basi mwite Mama Mdogo
 
Kinachoongeza mapenzi baina ya mtoto na mzazi ni malezi.....na wala si kubeba mimba peke yake.....na kuzaa...kwani hata paka anazaa na anawala hao hao wanawe....
Wapo wazazi waliowatupa watoto wao na walezi wakashika majukumu....na hatimaye mtoto hataki hata kumuona mzazi wake.....

Kuna watu wanavumilia mzigo wa miezi tisa tumboni lakini mwisho wa siku anamtupa mtoto chooni.....

Ninachowausia wakina mama ni kuwa wajue kuwa maisha ni safari ndefu sana....na hakuna ajuaye la kesho.....onyesha upendo kwa huyo kiumbe uliyekabidhiwa jukumu la kumlea kwani huwezi jua la mbele.....anaweza kuwa msaada mkubwa sana kwako kuliko hata wanao wa kuwazaa.....

Tusipende kulipa mabaya kwani kila pitio unalopitia linakuwa kama funzo kwako.....kuelekea ngazi fulani nzuri ya maisha yako.....

Kuna watu wakati wapo na mama zao walikuwa kupika wala kufua lakini kwa mikiki mikiki ya mama kambo hatimaye wanajua kupika na kufua....

Pirika pirika za mama wa kambo zinaweza kukupa ari ya kuongeza bidii kwenye masomo ili uje ujitegemee.....mikiki mikiki ya mama wa kambo zinaweza kukufanya ufanye bidii kwenye maisha na hatimaye kufanikiwa....

Watu wengi wenye mafanikio wamepitia changamoto nyingi sana....kwa hiyo ni wajibu wako kutumia changamoto hizo kama ngazi....ya wewe kufikia mafanikio yako.....

Hapo utagundua kuwa ukiwa na mtazamo chanya mama wa kambo utaampenda kwani kwa changamoto zake kwenye malezi yake ndio zimekufanya wewe kufikia hapo ulipofikia leo kimafanikio.......

Kwa hiyo hata kwenye utambulisho unaweza ukamuita kama shujaa wako....ili nafsi yake imsute.....
 
Wale ni mama zako wote, haina haja ya kusema mama mzazi na mlezi, kwani kama alikulea huwa nyumbani unamwita mama wa kambo, mlezi au mama?? We sema tu nawatambulisha wazazi wangu baba na mama zangu.
 
Wewe unampotosha... Ni lazima kiburudisho cha babako ambacho ni currently ukipe nafasi stahiki. Namna hii: naomba kutambua uwepo wa baba mzazi, mama Mzazi na mama mlezi, wote kwa pamoja wasimame.
vipi kama hakuwahi kukulea?mfano baba alizaa na mama then hawakuoana, baba alioa mke mwingine,na wewe ulilelewa na shangazi?.
 
Back
Top Bottom