Ushauri: Unamtambulishaje mama wa kambo?

Ushauri: Unamtambulishaje mama wa kambo?

Hii ni rahisi,utata ni pale mama alikuzaa na mme mwingine,then akaolewa na mme mwingine na sasa baba mzazi na baba wa kambo wote wapo ukumbini.Tena huyo aliyeolewa na mama yako awe hajawahi kukulea.
 
Hapo kwanza nita acha Ku assume,
Halafu utambulisho wangu utaaza kama ifuatavyo.
SALAMU,,,ndugu wageni wahalikwa ,mabibi na mabwana__
Asalaaam alekhum,
Kristo,
Bwana YESU asifiwe,
Kwa maajina ,(bwana harusi unataja majina yako)
Unatoa ukaribisho na kuendelea ,
Ningependa kutambulisha ndugu zangu ambao ni,kwanza
Baba yangu mzazi na mama yangu mzazi kwa pamoja wasimame wapunge mkono,,
Pacha wangu (kama unaye) asimame apunge mkono.

Unaendelea_mama zangu wadogo wote walipo wasimame wapunge mkono,
Baba wadogo, wasimame wapunge mkono,
Dada zangu wasimame wapunge mkono
Kaka zangu wasimame wapunge mkono,


Unamaliza wote kwa staili hiyo,
Angalizo ,,babu na bibi zako na shangazi Mkubwa watabulishe kipekee siyo kima fungu.

Huyo mama wakambo kama hakusimama na kupunga mkono ulipo watambulisha mama wodogo zako ukumbini hapo,asikulaumu.


Over&out

Kwani hiyo ni ndoa ya mkeka au ya kushtukizwa? Kama ni harusi iliyopangwa haya yatakuwa yamekwishazungumzwa kabla ya siku husika na maamuzi muafaka yamefikiwa.
 
Kwani mama wa kambo humtambulisha vipi mtoto wake wa kambo akionana na watu? Kama akisema huyu mtoto wangu wa kambo nae mtambulishe kama mama wa kambo lakini ikiwa anasema huyu mtoto wangu. Basi na wewe useme huyu ni mama yangu mke wa baba yangu. Ikifika kwa mama mzazi ndio useme huyu mama yangu mzazi.
Mkuu hapo mume wa huyo mamayako kama naye yupo hapo ukumbini utasemaje?
 
mama angu wa kambo namuita ma mkubwa, ikitokea utambulisho itakua hivo hivo mama angu mkubwa
 
vipi kama hakuwahi kukulea?mfano baba alizaa na mama then hawakuoana, baba alioa mke mwingine,na wewe ulilelewa na shangazi?.
Mkuu, malezi ni dhana pana muno,.. Ukipata mama wa kambo anayekubali kuja ukumbini kwenye show yako, huyo kakuleaaaa... Kwa sababu hata kukutunzia babako ili aweze kukusaidia ni malezi pia.
 
Mama wa kambo huwa tunasema ni ''MAMA MLEZI''
 
Back
Top Bottom