Ushauri unahiyajika tafadhali.

Ushauri unahiyajika tafadhali.

kinachomfanya jamaa ajirudishe si ni mtoto?si anakuja kwa gia ya mtoto?anaweza pia kumpeleka mtoto kwa baba yake.aende mpaka kwake amkabidhi mtoto mbele ya mke wake,akimkataa amwambie wasisumbuane,manake anachokifanya huyo jamaa ni kujaribu kuvuruga ndoa ya xwake.lazima bdada awe na msimamo otherwise ndoa yake kwishney.lazima afanye maamuzi magumu,sometimez u just hav to say..."to hell with shit"

Asante kaka kwa ushauri wako, nitamfikishia naamini ataufanyia kazi.
 
Asichague kumfurahisha mtu mzima mwenye hatia na anayejua anavhofanya na kumtesa mtoto asiye na hatia na asiyejua lolote
 
Nashukuru mno dada mimi49 kwa ushauri wako.
 
Mmoja kati ya marafiki zangu amekutwa na maswaiba yanayomfanya awaze kumchukua Maamuzi ambayo mi nimeyaona kama yatamuumiza mwanae;
Ipo hivi,
Akiwa chuo(degree holder kwa sasa)
Aliwahi kuwa na boyfriend na kutokana na upeo wake kuwa kiduchu akabeba mimba, alilea mimba akazaa ila baada tu ya kubeba mimba ndipo alipogundua kua mwanaume aliyekuwa nae was animal, alimpiga several time na kuna kipindi alitaka kumuua mtoto akiwa tumboni kwa kumbinya sana na kusema anayaka kumuua, baada ya mtoto kuzaliwa kipigo kiliendelea kwa kuwa alikuwa anaweza kwenda kwa bidada alipokuwa anakaa(bdada alipanga nje ya hostel).
Ilifikia wakati bidada ikabidi ampeleke mtoto kijijini kwa mama yake ili aendelee na chuo bila yale mateso, pale ndipo kila mtu aliendelea na maisha yake kwa kuwa bdada alirudi hostel bt alibebwa na shost wake(mimi). Kijana hakuwahi kumpenda mtoto, hakuwa kugharamia chochote bdada alimlea mwanae kwa kutumia boom, baada ya kumaliza chuo akaenda kumchukua mtoto mwanaume akaanza tena kumfuatafuata kwa kisingizio kuwa anaenda kumuona mtoto, bdada akaona isiwe tabu akamrudisha mtoto kijijini na kumuambia kama kweli anampenda mwanae akamtembelee ila cha kuchekesha ana cm ya bibi wa mtoto hakuwah kabisaa kupiga kutuma hata centi hata kwenda kumuona, baada ya mwaka na nusu jamaa akafunga ndoa ya kanisani, at the time mawasiliano yalishakata kabisa, miaka miwili baada ya ile ndoa bidada akapata mume tena sio mume tu bali mume mwema nae akafunga ndoa kanisani, maisha ya ndoa yakaendelea fresh tatizo lilianza pale yule baba wa mtoto anamtumia bdada sms, bdada akaamua kuteketeza line kwa kuwa hakuwah kubadilisha ila b4 ndoa ya bdada alimwambia kijana anataka kumkabidhi mtoto for good badala yake kijana akayeyuka. Sasa ameanza tena usumbufu wa ajabu ajabu anamfuata mume wa bdada na kujitambulisha mara anamtumia mama yake(bibi wa mtoto) ajidai anamjulia hali mtoto.
Maamuzi ya bidada;
Anasema kwa kuwa anampenda sana mume wake na watoto na kwa kuwa mumewe ni mpole na hastahili kusumbuliwa wala kuumizwa anampeleka mtoto kwa bibi yake mzaa baba ijapo anajua atakuwa amemtelekeza na hawawezi kumsomesha shule kama Anayosoma wala kumpa maisha anayopewa sasa kwa kuwa baba yake hakuwahi kumpenda.

Naombeni ushauri kama kuna yeyote aliye na ushauri tofauti ya uamuzi anaoamua kuuchukua.

Note; mme wa bidada alimchukua mtoto in akampa jina na malezi mazuri sawa na wanae(amezaa na bdada watoto wawili sasa)
Mi nadhani bora suala hili walichukulie kisheria zaidi...ili wawe na custody ya mtoto 50/50 au mama awe na mtoto 100% mpaka atakapofikisha umri fulani....Kwasababu wakiendelea kulichukulia kiholela tu huyo mwanaume atampelekesha sana bidada....
 
Asichague kumfurahisha mtu mzima mwenye hatia na anayejua anavhofanya na kumtesa mtoto asiye na hatia na asiyejua lolote

Hapa shida sio kumfurahisha huyo jamaa ila shida ni kuhakikisha ndoa ya bidada haiterereki na sanasana mumewe haumizwi.
 
Mim naona aende ustawi wa jamii na kule atakutana na sheria ambazo zitamsaidia na itaamuliwa mtoto akae wapi ktk mikono salama,na pia huko aeleze kila kitu kuhusu mumewe anavyopata usumbufu watatoa ushaur mzur ambao utasaidia.
 
Mim naona aende ustawi wa jamii na kule atakutana na sheria ambazo zitamsaidia na itaamuliwa mtoto akae wapi ktk mikono salama,na pia huko aeleze kila kitu kuhusu mumewe anavyopata usumbufu watatoa ushaur mzur ambao utasaidia.

Nashukuru mno dada yangu. Nitamfikishia ili ajaribu kuufanyia kazi.
 
Back
Top Bottom