Ushauri unahitajika

Ushauri unahitajika

atlas copco

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
8,552
Reaction score
9,809
Habari za jumatatu wadau na imani weekend ilienda poa sana

Kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu kuna dada nipo nae kwenye mahusiano na ninadhani nilishaleta uzi hapa unamzungumzia huyo mwenzangu, huyo dada ni single mama ila nilitokea kumwelewa sana. Kwa kweli tuna mipango mingi ya maisha na hivi karibuni nahitaji kwenda kwao kujitambulisha ili nijibebee mazima ila kuna sintofahamu imejitokeza .

Kilishosababisha nihitaji ushauri wenu wadau, jana nilibahatika kushika simu yake bila yeye kujua, baada ya kuipekua niligundua mwenzangu sio mwaminifu kuna namba kama mbili hivi tofauti ambazo ukisoma text zake zina ukakasi tena sio kidogo, kwakweli baada ya pale mood yote ilikata nikabaki nimkodolea macho tu, ila kabla hajaondoka nilimweleza japo sikumwambia straight, nilimwambia hao wanaume uliokuwa nao wanakudanganya so kuwa makini so kama bado unaona hujamalizana na ulimwengu just unieleze kuliko kupotezeana na muda na magonjwa, baada ya pale alibaki ameduwaa tuu na kukataa hana mahusiano yeyote zaidi yangu

Hebu nishaurini wadau niendelee na harakati za kwenda kwao au nicancel hio michakato?,nipo njia panda.

Nb:dunia ya sasa hivi naelewa hamna mwanamke/mwanaume wa pekee yako ila ninachohofia je atakapokuwa ndani ataendeleza hii tabia?!....

Samahanini kwa uandishi mbaya nahitaji ushauri masihara tuweke pembeni

Niwatakie j3 njema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila mtu anakaujinga flani huwa anakafanya kwa lengo la kujifurahisha au kupoteza muda in a very secret way. Mwingine kuchati na wanaume au wanawake ndio funny yake ila hawezi kutembea nao. Ili kujiridhisha nilazima uweke mitego yako vizuri kwamba kwanini anafanya hivyo na kwa lengo gani. Ukijiridhisha kuwa hajatulia basi unapiga chini. Ukitaka nikukamatie nijulishe..
 
Naomba mkweli kwako, ukimuoa utakuwa umefanya kosa kubwa katika maisha yako, kumbuka kwamba tabia unazo zigundua kwa mwenza wako pasipo yeye kukuambia wakati wa uchumba HIVYO NDIVYO ALIVYO. Na ukijidanganya kwamba atakuja kubadilika hiyo ni utashi wako, pia tarajia kupata migogoro na hicho ulicho kiona kwenye sim yake hakitokaa kifutike kirahisi kwenye akili yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nadhan fikria hivi...single mother ila anamtu alozaa nae na uyo mtu ananamba mbili wanawasiliana kumjadili mtoto wao na wewe hutaweza kuja zuia kamwe!
 
Kila mtu anakaujinga flani huwa anakafanya kwa lengo la kujifurahisha au kupoteza muda in a very secret way. Mwingine kuchati na wanaume au wanawake ndio funny yake ila hawezi kutembea nao. Ili kujiridhisha nilazima uweke mitego yako vizuri kwamba kwanini anafanya hivyo na kwa lengo gani. Ukijiridhisha kuwa hajatulia basi unapiga chini. Ukitaka nikukamatie nijulishe..
Okay nimekupa ngoja niendelee kuweka mitego yangu,asantee kwa ushauri ila nitakufuata private unitengenezee mitego

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Single maza pasua kichwa sana. Aliewaroga kafa. Umezwalishwa na kutelekezqa unapata mtu wa kukistiri bado unawashwa huko chini kutulia hutaki. Ni laana au nn tatizo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hii dunia wanawake ni changamoto aisee,japo na ss hatujalia lakin wenzetu wanataka nin ukiwa na pesa utasalitiwa ukiwa ndio shida kabisa ss sijui hata tufanyaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna kitu kinauma kama ugundue mwenzio anakusaliti na huna namna ya kumfanya aache zaidi ya atake mwenyewe
Kweli mkuu sikufichi baada ya kuona hizo text nilimwangalia nikabaki namtafakari tuu,mpaka muda huu sitaki kulichukulia hili jambo kwa hasira,ushauri wako bado nauhitaji mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
@Ushimen,Kuhusu huyo jamaa nina uwezo wa kumdhibiti ila na mpaka ss nimeanza kumtengenezea mazingira huyo mshikaji,ss jamaa yangu nikisema nitafute mwingine unaweza kujikuta umeruka mkojo ukakanyaga mavi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nadhan fikria hivi...single mother ila anamtu alozaa nae na uyo mtu ananamba mbili wanawasiliana kumjadili mtoto wao na wewe hutaweza kuja zuia kamwe!
Kuhusu mzazi mwenzake huyo hana tatizo sababu mtt atabaki kwa bimkubwa wake wakat tunaendelea kujipanga,so kama ni mawasiliano baba mtt atakuwa anawasiliana na bibi yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli mkuu sikufichi baada ya kuona hizo text nilimwangalia nikabaki namtafakari tuu,mpaka muda huu sitaki kulichukulia hili jambo kwa hasira,ushauri wako bado nauhitaji mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
mweleze bas kua huwezi kumfos aache anachokifanya na hukipendi ila mpe option kama anaona hawezi heri muachane mapema kabla hamjaoana kuachana mkiwa hamjaona ni kiasi cha maamuzi tu kama mmoja wenu akiamua, waweza pia kumpa muda akiendelea kujitafakari,
 
Okay na asantee kwa ushauri mkuu,soon nitakupa mrejesho,ila kabla hatujaachana nilimweleza kabisa kuna mtu anakudanganya kama ni uongo niambie nasema uongo,alikaa kimya tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom