Ushauri unahitajika, mambo yamenifika shingoni

pole mkuu .. kama unaona anaweza rekebishika msamehe ila mmh me sipendi ujinga kwenye pesa aisee
 
Habari wanajamii mm ni mme wa mke mmoja na watoto watatu nimeoa mwaka 2000 hali ya maisha haikuwa nzuri kimapato nilijifunza mgambo mwaka 2000 mwaka 2004 nikaanza kazi ya ulinzi kampuni moja 2005 nikahamia nyingine tatizo langu mke wangu amekuwa na matumizi mabaya sana ,tumejenga nyumba1 kinachofanya nilete hii threed ni kwamba wakati nafanya kazi nilikuwa naweka ppf na ilipofika mwaka jana nilichukuwa fao langu la kujitoa kama 3milion nikapeleka kwa mke wangu tuzifanyie biashara ya kukopesha nilimpa 2milion kulingana na utaratibu wa kazi tunaishi mikoa tofauti tulihamia mkoa mwingine sasa mwaka 2015 nikarudishwa mkoani kwetu wife na watoto wakabaki mkoa ule ambako nilikuwa awali nilikuwa karibu sana nao kwa matumizi ya msingi yote kuanzia mavazi chakula na mahitaji mengine ya nyumbani na shuleni tulipokopesha hizo 2milion nikamwambia malejesho apeleke bank lakini kinyume chake akawa anasema hajalipwa nilipofuatilia wateja wamelipa wote na hela ametumia zote nilipo fuatilia zaidi nikakuta amekopa madeni kwa watu binafs finca brack kiasi cha madeni yote siyo chini ya milioni moja na riba inaendelea na alipokuwa anakopa alikuwa anasema hana mme kwamba tulishatengana alijaribu kujiua ikashindikana sasa yupo nyumbani na hali yetu siyo nzuri siku nyingine tunakosa hata chakula na matumizi mengine amekuwa mharibifu wa fedha matumizi yake siyo mazuri vyombo vya ndani kama kochi ameuza na vilivyopo ndani ameweka lehani wenye mikopo walipotaka kushika niliweka pingamizi mambo ni mengi nimedonoa kiasi naombeni ushauri jamani naishi maisha magumu kazi ya kulala njee nimechoka(ulinzi)
:rolleyes::rolleyes: Huu uandishi ni wa Aina yake. Yaana nmeona alama ya Mkato moja Tuu.
 
Aisee!

Uandishi gani sasa huo?

Hakuna koma, hakuna nukta, haijulikani sentensi imeanzia wapi na imeishia wapi....

Tuna majanga mengi mno nchi hii!

Mkuu Nyani Ngabu punguza munkari mkuu wa kazi, nimeona for the past two weeks humu jf mabandiko yako yanaashiria hauko sawa mkuu, kwa sisi marafiki zako tunao kujua humu JF tunajua tu haupo sawa punguza munkari.
 
Aiseeee..! Huyo mwanamke hakufai na kwa maelezo yako inaonyesha yy ndie mwenye sauti.
2M kala bado kaenda kuchukua na mkopo haitoshi kauza na thamani za ndani ww upo upo tu. .! Pole sana ila mzizi wa matatizo ni ww mwenyewe.
 
Kweli tunatofautiana! Na muda wa kuingia humu umeupata.....hii kwangu ilikuwa kesi tayari,nashukuru mungu sio mimi.
 
Habari wanajamii mm ni mme wa mke mmoja na watoto watatu nimeoa mwaka 2000 hali ya maisha haikuwa nzuri kimapato nilijifunza mgambo mwaka 2000 mwaka 2004 nikaanza kazi ya ulinzi kampuni moja 2005 nikahamia nyingine tatizo langu mke wangu amekuwa na matumizi mabaya sana ,tumejenga nyumba1 kinachofanya nilete hii threed ni kwamba wakati nafanya kazi nilikuwa naweka ppf na ilipofika mwaka jana nilichukuwa fao langu la kujitoa kama 3milion nikapeleka kwa mke wangu tuzifanyie biashara ya kukopesha nilimpa 2milion kulingana na utaratibu wa kazi tunaishi mikoa tofauti tulihamia mkoa mwingine sasa mwaka 2015 nikarudishwa mkoani kwetu wife na watoto wakabaki mkoa ule ambako nilikuwa awali nilikuwa karibu sana nao kwa matumizi ya msingi yote kuanzia mavazi chakula na mahitaji mengine ya nyumbani na shuleni tulipokopesha hizo 2milion nikamwambia malejesho apeleke bank lakini kinyume chake akawa anasema hajalipwa nilipofuatilia wateja wamelipa wote na hela ametumia zote nilipo fuatilia zaidi nikakuta amekopa madeni kwa watu binafs finca brack kiasi cha madeni yote siyo chini ya milioni moja na riba inaendelea na alipokuwa anakopa alikuwa anasema hana mme kwamba tulishatengana alijaribu kujiua ikashindikana sasa yupo nyumbani na hali yetu siyo nzuri siku nyingine tunakosa hata chakula na matumizi mengine amekuwa mharibifu wa fedha matumizi yake siyo mazuri vyombo vya ndani kama kochi ameuza na vilivyopo ndani ameweka lehani wenye mikopo walipotaka kushika niliweka pingamizi mambo ni mengi nimedonoa kiasi naombeni ushauri jamani naishi maisha magumu kazi ya kulala njee nimechoka(ulinzi)
Binafsi nakushauri usithubutu kumwacha, jaribu kuwashirikisha ndugu Wa pande zote mbili niimani yangu mambo yatakaa saw a. Kikubwa usiache kupiga magoti kwa BWANA kuomba awape kibali cha amani na furaha katika ndoa yenu,Mungu ni mwema na mwaminifu hatokuacha katika hili lengo la shetani ni kuona ndoa yenu imevunjika . Kwa imani ya kikristo uwezi kumuacha mke kwa sababu yoyote ile isipokuwa kwa habari ya uasherati ( math 19:7-9). Ubarikiwe
Hakika mke mwema hutoka kwa bwana
Jipange upya huku ukiweka mipaka ya matumizi

MPE talaka
 
Pole.

Ila ulijua mkeo mfujaji (ndio udhaifu wake kwa nini ulimpa?????)

Maji yamekwisha mwagika.

Kikubwa hapa ni kupamban kiume.

Mkeo sio wa kumpa hela hata ya bajeti (kama maelezonyako ni yanukweli).

Wewe ni mlinzi.
Unaporudi asubuhi ukishapumzika tafuta kitu kingine cha kukuingizia pesa.

Unapoishi.kama.mazingira yanaruhusu mkeo afunge ubuyu mpike chapati uzeni mkaa nk (chini ya usimamizi wako wa hali ya juu katika pesa)

Jitahidi pia chakula mnunue kingi hata kama uwezo mdogo. Rejareja inaumiza.

Mnappishi kama mna kijieneo pandeni nyanya mahindi mbogamboga kwa ajili ya chakula na kuuza iki lpate senti...tena uzuri hamlipi kodi ya nyumba nyie
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom