Ushauri unahitajika kunusuru roho ya mtu!

Ushauri unahitajika kunusuru roho ya mtu!

Hun

Senior Member
Joined
Oct 11, 2012
Posts
110
Reaction score
106
Ni mahusiano ya miaka saba, na mtoto wa miaka 5, hawajaoana

Mwanzoni wa mahusiano ndugu za mwanaume hawakumtaka mwanamke kwa kuwa ana imani tofauti, lakini mwanaume aling'ang'ana

wamejenga nyumba mbili pamoja moja ipo Dar moja Kijijini kwa mwanaume. mwanaume anaishi kwenye nyumba ya Dar, mwanamke anaishi kwa wazazi wake.

Tangu 2010 mahusiano yamekuwa ni machungu kwa mwanamke mana alikuwa akipaa lugha za kejeli, matusi, vipigo na kutojaliwa. wameacha zaidi ya mara tano na kurudiana.

Kuna kipindi mwanamke aliambiwa hakupendwa, aliumia akalia lakini bado alimsamehe. wakaendelea.

katika siku saba za wiki watafurahi kwa siku moja au nusu siku the rest ni maumivu kwa mwanamke.

sometime mwanamke alikuwa akimuambia kuwa atachoka,lakini kidume atasema "utaenda wapi wewe", "mie siachwi".na maneno kedekede ya kejeli. akiombwa waongee anasema "wimbo wa taifa"

sasa mwanamke kachoka amemuacha huyu kijana tangu mwaka jana May lakini kidume kilijua ndo yaleyale atarudi tu.mpaka navyoandika hapa mwanamke kashikilia msimamo wake.

kuna usemi unasemwa 'what goes around come around'. ndo yanayomkumba mwanaume sasa.kapita kwa ndugu wote, rafiki wote,anamfwata nyumbani na kazini, bi dada hamtaki.kafikia hatua ya kulia kama mtoto aliyepigwa,bi dada wapii.sasa kafikia hatua mbaya ya kusema atajiua. je anaweza kujiua kweli au mkwala, je amtafutie watu wa kuongea nae au nini afanye?ni maswali anajiuliza bi dada hapati jibu. ndo nimeamua kuleta jamvini, mana Hapo bi dada kaogopa, hajui afanyeje,mana hataki kurudi mana anasema aliteseka sana, na amepata anayemthamini na kumpenda kwa dhati.

Anahitaji ushauri wenu wa busara wajameni.
 
How many chances again alizopewa huyo mwanaume????
 
Aachane naye wanao jiua hawatangazi, wangekuwa wanatangaza wangeokolewa, wengi wao tunakuta mizoga tu.
 
Kujiua hawezi kujiua.

1. Kama bidada anahisi moyo umekufa ganzi kabisa na hana haja kumsamehe basi akaze tu

2. Kama ana nafasi kidogo moyoni kwake, basi amsamehe jamaa, ila amwambie wafunge ndoa kabisa na waishi pamoja
 
  • Thanks
Reactions: Hun
Asilegeze kamba, akimsamehe tu imekula kwake atajuta.Kama anataka kujiua bi dada amtafutie dawa au kamba ya kujinyongea.
 
second chance apewe bwana! maisha ni haya haya mi ningerudi nione kama kuna jipya,kama hakuna napiga chini tena ,kwani nini?
 
Aachane naye wanao jiua hawatangazi, wangekuwa wanatangaza wangeokolewa, wengi wao tunakuta mizoga tu.

Aaah we...mimi kuna cousin bro wangu ndio ulikuwa mkwara wake huo for years, kitu kidogo tu 'ntajiua mimi'. Alijiua kweli mwaka juzi!
 
Aaah we...mimi kuna cousin bro wangu ndio ulikuwa mkwara wake huo for years, kitu kidogo tu 'ntajiua mimi'. Alijiua kweli mwaka juzi!

Mh na nyie mkwara wa muda mrefu, kwanini hamkumpeleka kumpima akili?
 
And she thinks he is worthy another eeh?

hahaha Kaunga wanichekesha....akimuona analia anaona huruma ila mpaka sasa bado amekaza kamba.katoka kunipigia leo kaenda job kwake kampigia magoti na kulia kama mtoto
 
Kujiua hawezi kujiua.

1. Kama bidada anahisi moyo umekufa ganzi kabisa na hana haja kumsamehe basi akaze tu

2. Kama ana nafasi kidogo moyoni kwake, basi amsamehe jamaa, ila amwambie wafunge ndoa kabisa na waishi pamoja

according to bidada anasema moyo umekufa ganzi kabisa sasa hivi ana mapenzi nae tena, na ameshamove on
 
kujiua sio solution ya matatizo, either aondoke au avumilie, aache utoto
 
hahaha Kaunga wanichekesha....akimuona analia anaona huruma ila mpaka sasa bado amekaza kamba.katoka kunipigia leo kaenda job kwake kampigia magoti na kulia kama mtoto

Ever heard of psychopath? Kukuabuse, Kulia kutishia kujiua, kuku stalk ipo ndani ya DNA yao. Hivyo maisha yake chaguo lake, kama hizo crocodile tears zinamdanganya ampe chance ya 6, 7 hadi 27
 
  • Thanks
Reactions: Hun
gfsonwin njoo toa ushauri huku. binti anatishia nyau.

kujiua sio solution ya matatizo, either aondoke au avumilie, aache utoto

Blaine hujaipata vizuri story ...mwanaume ndo anatishia nyau kuwa atajiua bidada asipomrudia
 
according to bidada anasema moyo umekufa ganzi kabisa sasa hivi ana mapenzi nae tena, na ameshamove on

Kama hivyo ndivyo basi tena, haina haja basi, amwambie wazi kuwa haiwezekani na nakuhakikishia jamaa hawezi kujiua.

Sorry niulize, bidada kashapata pumziko lingine la moyo nini?
 
Blaine hujaipata vizuri story ...mwanaume ndo anatishia nyau kuwa atajiua bidada asipomrudia
ooops!! my bad. mwanaume kujiua for a woman, that's even more stuuuppppidd. mwambie tutakuja kumfariji mjane
 
  • Thanks
Reactions: Hun
Back
Top Bottom