Ushauri unahitajika haraka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri unahitajika haraka

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Zneba, Aug 19, 2011.

 1. Zneba

  Zneba Senior Member

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wana jf,kuna rafiki yangu wa karibu sana amepata tatizo hili hapa na anaomba mumsaidie ushauri.naomba ambae hayuko serious asichangie kabisa.

  Rafiki yangu ana boyfriend ambae wanapendana sana tu, tatizo hawa watu kwanza wana dini tofauti mwanaume ni mkristo na msichana ni muslim shida imekuja mwanaume amewambia ndugu zake kuwa anataka kumuoa huyo binti kwa ndoa ya bomani ndugu wamekataa kabisa wanataka amuoe msichana wake wa mwanzo ambae ni mkristo km yy, ila jamaa anasema huyo msichana hakuwa anampenda tangu mwanzo ila ndo ndugu wanamtaka huyo.

  Na tatizo lingine alilogundua huyu rafiki yangu jamaa amepunguza mawasiliano nae wala hamtembeli tena akidai emechanganyikiwa hajui nini cha kufanya. Sasa bint anauliza, VIPI AAMUE YY KUMUACHA JAMAA TU MANA ANAMUONA KAMA HANA MSIMAMO COZ HATA KAMA KUNA HILO TATIZO KWA NINI ABADILIKE?

  MSHAURINI AU ASUBIRI TU MANA JAMAA AMEMUAMBIA ANAENDA KUONGEA NA NDUGU ZAKE KAMA WATARIDHIKA JUU YA HILO.
   
 2. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni wewe usimsingizie rafiki yako
   
 3. Zneba

  Zneba Senior Member

  #3
  Aug 19, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni rafiki yangu kweli coz ningejitaja hakuna shida coz hakuna anayenijua.
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kama matatizo yameanza wakiwa bado hawajaingia kwenye ndoa na wakijaingia itakua je? Kilichopo asifikirie kwa sasa tu wafikirie na baadae itakua je wakiwa kwenye ndoa afu achukue uamuzi thabiti ambao hataujutia baadae
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Imani huwa si issue sana kama mmependana.
   
 6. Zneba

  Zneba Senior Member

  #6
  Aug 19, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ila ndugu ndo huwa issue au nifafanulie hapo ulimakafu
   
 7. Zneba

  Zneba Senior Member

  #7
  Aug 19, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  anayetakiwa kufikiria zaidi hapa ni nani mwanmke au mwanaume sijakupata vizur
   
 8. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mabadiliko yanasababishwa na mengi ... inawezekana yeye rafikiyo anaona mabadiliko ya mwenzake kuliko ya kwake ...kwanza katika kipindi hiki ambapo kuna mgogoro huyo rafikiyo anatakiwa awe na mwenzi wake karibu sana na anatakiwa amshauri au washauriane nini kinatakiwa na kwa wakati gani, pia ni vyema wakawekana wazi kikwazi kiko kwa nani hasa sidhani kama ndugu wote ni kikwazo .

  Je upande wa rafiki yako wanaridhia juu ya huyo bwana maana nimeona iko upande mmoja tu. na kwa nini afikiria kumwacha jamaa ilihali ndo safari inataka kuanza ??? je wao wamekubaliana kusimama kwa dini gani baaada ya ndoa??? watoto watafuata dini ya nani???
   
 9. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  kwa upande wangu mm ninaona hata iwe vipi tatzo litabaki pale pale mana hata ndugu ya jamaa wakikubali bado ndoa yao itaendelea kuwa na tatzo kwny upande wa dini hvyo basi nivizur mmoja wapo akakubali kuingia kwny din nyngne kuliko ndoa kuwa vuguvugu na kama itashndikana nivizur kila mmoja achukuwe taimu yake mana wakiwa kwny ndoa matatzo yatakuwa makubwa mara nne ya sasa na hvyo jamaa anaongozwa na ndugu na kuwasikiriza ajiadhar sana huyo rafiki yako
   
 10. Zneba

  Zneba Senior Member

  #10
  Aug 19, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aliyebadilika siyo rafiki yangu ni mwanaume ndo amebadilika baada yakuwaeleza ndugu zake,na mwanamke hana tatizo yko tayari kumpa sapoti yoyote kwa kipindi hiki na upo sahihi kabisa ila anashangaa jamaa amebadilika kwenye hiki kipindi cha matatizo,kuhusu upande wa mwanamke bado hawajaeleza wazazi wake akasikia wanasemaje ila baadhi ya ngugu zake aliwaeleza na hawana tatizo na hiyo imani na kuhusu watoto wataifata imani ya baba hilo lilikuwa lipo wazi na pia halikuwa na shida kihivyo.anafikiria kumuacha coz anahisi jamaa km ana fikiria hivyo kwanini sasa abadilike
   
 11. Zneba

  Zneba Senior Member

  #11
  Aug 19, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo nalo neno na yy alichogundua ni jamaa anawasikiliza sana ndugu zake ndo mana amepata hofu juu ya muendelo wa uhusiano huu
   
 12. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  tatizo rafikiyo alipoambiwa kwamba ndugu wa mwanaume hawataki ni lazima ilimshtua na ameshajenga uoga ... unasema kabadilika mwanaume kwa vile umesikiliza upande mmoja .. kaa na rafiki yako umwambia awe karibu na jama asisubiri hadi jamaa amtembelee
   
 13. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mapenzi ya kweli hayana dini, kabila, rangi, sura, mali wala umri… Dini siyo issue!

  Huwezi kuomba kibali cha kumwoa yule unayempenda ila unaweza kutoa taarifa kwa ndugu; jamaa; marafiki. Kumbuka hakuna demokrasia kwenye maisha ya watu wanaopendana. Maisha ni ya wawili. Mwanaume ameonyesha kutojiamini na ni dalili mbaya za maisha ya baadaye. Nyumba inaweza kutawaliwa na ukoo mzima..

  Kwa nini achanganyikiwe badala ya kumshukuru Mungu kwa kumkwepesha na bomu? Huyo jamaa yake wanafaa kwa kufanya mazoezi ya mapenzi tu lakini HAFAI kwa jukumu la kumpa moyo na maisha yake.

  Kumbe jibu zuri la suluhu analo..Kama alikuwa anataka support hapa JF..mwambie yuko sahihi kupiga chini huyo jamaa.. Hamna kitu hapo!
   
 14. Zneba

  Zneba Senior Member

  #14
  Aug 19, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yani tulizo asante kwa ushauri wako ameupata hata mi kwa mtazamo wangu nimeona jamaa atamsumbua huko mbele familia nzima itatoa maamuzi kama hapo tu ameshindwa kutoa maamuzi na kubadilika juu ni wazi kabisa mbleni ni hatari kubwa,thanx
   
 15. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #15
  Aug 19, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180


  Asilimia zaidi ya 50% ya ahadi wanazopeana wapenzi ni za uongo. Nadiriki kusema kuwa huyu rafiki yako kadanganywa...

  Kinachoonekana hapa huyu jamaa alikuwa na huyu dada ki-mapenzi zaidi lakini linapokuja suala la kuoa, inabidi awe siriaz, na ndicha anachofanya. Kusema kuwa ndugu wanamkataa, hata mimi ndicho ningesema kama nataka kumuacha mtu ambaye sina sababu ya kueleweka kwake. Indication kubwa ya uongo huo ni huyo jamaa kupunguza mawasiliano kwa kisingizio eti 'amechanganyikiwa'.... Naamini huyo dada atakuwa na umri mdogo au uzoefu mdogo sana katika mapenz, otherwise angeshamshtukia jamaa.

  Kwa hiyo huyo dada ajue tu kuwa kama ataendelea kuwa na huyo jamaa, kikomo chao ni jamaa atapooa mtu wa dini yake, ama kwa sababu ya dini au kwa sababu anampenda huyo mwingine zaidi, maana pia inawezekana hampendi tena huyo rafiki yako, anatafuta kisingizio. Zipo threads kadhaa humu za namna ambavyo watu wana-act pale wapenzi wao wa dini tofauti wanapokataliwa na ndugu. Zipitie, utaona kuwa anavyofanya shem wako, sivyo ianvyokuwaga real, hapa natafuta kisingizio tu...
   
 16. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mwambie aingie huku tumshauri yeye moja kwa moja...!
   
 17. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  kama huyo jamaa yako hayo serious we mteme tu bhana, atakuja kuwa kikwazo bureee, inaonekana hawezi maisha, ie He cant afford challenges in life.
   
 18. Kottler Masoko

  Kottler Masoko Senior Member

  #18
  Aug 19, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Temana tu, maana hata mkioana familia yenu hasa watoto watayumba sana, mtaishi kwa kuogopana badala ya kuheshimiana. Fikirieni mbali zaidi na nyayo zenu. Usiwasikilize wanaokudanganya kwamba dini haina nafasi ktk ndoa, Maadili Mazuri ya dini ktk Familia ndiyo yanayoongoza nyumba.
   
 19. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wazee wa ukoo walikuwa wasiwasi na ndugu yetu kuoa dini ingine, lakini jamaa aliendelea na msimamo wake,ajabu ile umekuwandoa ya mfano kwa kila familia, wanaishi kwa amani na upendo karibu kuliko wote wanandoa wa lika lao kwenye ukoo, kwa hiyo kama huyo jamaa atakubali hili limshike wala hakufai achana nae tu kabla hujaumia moyo
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Wait and see.....
   
Loading...