Ushauri unahitajika: Familia tumekwama

Inawezekana mimba ikawa ya kaka yako, kuna wanawake wengine vizazi vyao viko karibu, bia inategemea na aina ya staili aliyoitumiwa/aliyopewa na mchepuko mpaka hizo mbegu chache kufanya urutubisho
 
Nimejikuta nawaza kwa mfano siku moja mke wa Kaka yenu angeamka tu akasema Mimi ni mjamzito reaction ya familia yenu ingekuaje? Mngemsikiliza na kuamini kuwa labda ni muujiza umetokea? Mngempa benefit of doubt Kama mlivyompa mchepuko? Mngemshauri Kaka alee tu mimba mke wake akijifungua watapima DNA umesema hapo juu kwamba ukoo unataka mtoto angekua ni mke wake ndo kapata mimba kwenye situation hiyo mngefumba tu macho as long as ukoo umepata mtoto?. Anyways nashauri ndugu msiingilie waacheni wenyewe wafanye maamuzi.
Na ndo wanavunja ndoa za watu bila aibu et tunakuwa na vikao mxeew!
 
Kosa Wanaume tunalofanya ni kwamba, baadhi yetu tukiwa kwa michepuko tunaongea sana hadi siri za ndani, sasa jamaa alivyobwege katangaza kwa mchepuko kuwa Wife hashiki mimba, kumbe yeye ndio mwenye tatizo, atarudije kwa mchepuko amwambie ukweli
Na ndo maana umemkomalia?yaani kuna wanaume suruali hivi kama we ni mwanaume ushajua huwezi zaa hivi unakosaje kutumia maarifa na mkeo mpaka familia nzima inajua tatizo lako?
 
Lakini hapa inaonekana huyo ulompa uhusika kama kaka yako ni wewe mwenyewe!

Ninachojiuliza kulikuwa na ulazima gani jambo dogo kama hilo mpaka ukoo mzima ujue??

Huna mbegu za kiume ukoo mzima unajua, umebambikiwa mimba na mchepuko ukoo mzima unajua na hadi uzi umeanzisha
Hakuna mwanaume hapa
 
Nilichogundua mnataka Kaka yenu akubal tunkuhudumia ili ionekane hyo mimba yake apate mtoto

Lakn ukweli jamaa Hana uwezo wa kutungisha mimba

Sasa achukuliwe huyo mjamzito mke wa Kaka yako na Kaka yako n wazaz wa pande mbili muende hospitali mtakayo kubaliana huyo Kaka akapime wote mkiwa Kama mashahid ili kutoa SINTOFAHAMU hii

Maisha magumu kwa sasa ukipata boya wa kumshikilia usimuache ndyo alichotumia huyo mchepukp
Inawezekana kuna wakati mbegu zinakuwepo. Mungu wa ajabu. Kama vile mwanamke anapopata mimba baada ya miaka mingi ya kuhangaika. Yaani linatoka yai lisilokuwa na dosari na kutungishwa.
 
Heshima kwenu wakuu. Usipite bila kushauri.

Kuna issue ya kimahusiano inaleta utata kwenye familia.

Tuna kaka yetu mkubwa ameo mwaka wa Saba sasa na hawajabahatika na mkewe kupata mtoto. Familia imewahi wasidia sana kujua nini chanzo cha tatizo mara kadhaa na taarifa rasmi za kitabibu tunayoijua kama familia ndugu yetu ana tatizo la kutokua na mbegu za kiume yaani azoospermia . Hali
Kama kaka yenu hawezi kumhudumia mjamzito, kwanini ninyi kama familia msilibebe hilo jukumu, mpaka mtoto atakapozaliwa ndio mpate uthibitisho kama ni mtoto wenu au la?
 
Tulishakubaliana mtoto ni wa jamii kwa hiyo alee tu kiroho safi.
Tena ameshaambiwa hana uwezo wa kupiga mimba halafu anakataa mtoto wa bure? Au amepanga kwenda kuwa mtawa?

Asubiri siku huyo mkewe watakapompiga ujauzito ndio atajua dunia haina huruma
 
Heshima kwenu wakuu. Usipite bila kushauri.

Kuna issue ya kimahusiano inaleta utata kwenye familia.

Tuna kaka yetu mkubwa ameo mwaka wa Saba sasa na hawajabahatika na mkewe kupata mtoto. Familia imewahi wasidia sana kujua nini chanzo cha
Amsaidie tu kulea mimba maana hata kama mtoto akiwa sio wake (baada ya vipimo vya DNA)then itakua kama sadaka tu !!kuliko kuacha halafu ikathibitika ni yake!!
 
Heshima kwenu wakuu. Usipite bila kushauri.

Kuna issue ya kimahusiano inaleta utata kwenye familia.

Tuna kaka yetu mkubwa ameo mwaka wa Saba sasa na hawajabahatika na mkewe kupata mtoto. Familia imewahi wasidia sana kujua nini chanzo cha
Mkuu ushauri wangu ni huu: Hiyo inawezekana ikawa ni damu yenu au isiwe yenu. Cha kufanya, kaka ako aendelee kuhudumia hiyo mimba ila kwa siri. Kivipi?

Kama upo mkoa mmoja na kaka ako awe anakupatia ww kiasi cha pesa cha kuihudumia hiyo mimba. Hasa iwe hand to hand au akutumie kwa wakala ili kuepusha shemeji yako kumtrace kaka yako kwenye simu yake kwa kuangalia miamala yake.

Mhudumieni uyo mama K(kwasababu ana wahitaji zaidi nyinyi) na Mungu atawabariki iwe ni damu yenu au isiwe ni damu yenu. Kila la kheri!!!
 
Yaani bro wako alishindwa kumuhudumia huyo Dada kimya kimya Hadi issue ikajulikana na wife wake!!?.

Kwa ushauri wangu aendelee kumuhudumia huyo Dada kwa Siri pasipo mkewe kujua. Akishajifungua waende kupima DNA kuthibitisha Kama mtoto ni wake kweli.
you said it all, miracles happens in mysterious way

hahahahha
 
Mkuu ushauri wangu ni huu: Hiyo inawezekana ikawa ni damu yenu au isiwe yenu. Cha kufanya, kaka ako aendelee kuhudumia hiyo mimba ila kwa siri. Kivipi? Kama upo mkoa mmoja na kaka ako awe anakupatia ww kiasi cha pesa cha kuihudumia hiyo mimba. Hasa iwe hand to hand au akutumie kwa wakala ili kuepusha shemeji yako kumtrace kaka yako kwenye simu yake kwa kuangalia miamala yake.

Mhudumieni uyo mama K(kwasababu ana wahitaji zaidi nyinyi) na Mungu atawabariki iwe ni damu yenu au isiwe ni damu yenu. Kila la kheri!!!

Yani unaamini huo Uko wote hawajui cha kufanya mpaka unashauri?
 
Mshaambiwa hana mbegu za kiume anadhani huyo mtoto wake?

Aache kujichosha

Kwanza ashukuru mkewe hajamletea mtoto wa nje halafu bado anajishaua!!!!
 
Wawe na kitabu cha matumizi kwa ajili ya kurekodi gharama amabazo kaka yako anagharamia hiyo mimba, kisha waandikishane kuwa baada ya kujifungua DNA ikigoma kaka yako alipwe matumizi yote aliyotoa.
 
Huwa anakwenda kupima wakati amekwisha zimwaga zote na hormone zimeparaganyika, wakati yupo safi na manii zake zina mbegu kama zote ndio anakutana na mchepuko...ikumbukwe yai la mchepuko au house girl huwa yanapaa kuzikimbilia mbegu za muwe wa mtu mjue!

Hivyo hata zikiwa kidogo tu mimba hiyo! Jamaa aendelee tu kuitunza mimba ya mtoto wake wa nje! Pia wife aache mapozi, achangamke ili na mayai yake yasisubiri mpaka vimbegu vya mumewe viogelee vifike, ajiongeza kwa kufukuzia mbegu hizo kidogo na dhaifu ili abebe mimba! Vipimo siyo siku zote ni 100% uhakika!

Heshima kwenu wakuu. Usipite bila kushauri.

Kuna issue ya kimahusiano inaleta utata kwenye familia.

Tuna kaka yetu mkubwa ameo mwaka wa Saba sasa na hawajabahatika na mkewe kupata mtoto. Familia imewahi wasidia sana kujua nini chanzo cha tatizo mara kadhaa na taarifa rasmi za kitabibu tunayoijua kama familia ndugu yetu ana tatizo la kutokua na mbegu za kiume yaani azoospermia . Hali hii aina uhusiano na kufanya mapenzi na kulizishana bali ni kwamba mwanaume anakua hana mbegu za kiume kwenye manii yake.

Sasa hivi karibuni imeripotiwa case kuwa amempa mdada ujauzito. Brother amekili kuwa amewahi kutembea bila kinga na huyo dada ila hana uhakika kama dada alikua hana jamaa mwingine. Dada huyo amekua akifuatwa na family member akiulizwa kuwa ujauzito ni wa nani ili kuhepusha mgogoro unaoendelea kwenye familia. Mara zote dada amekua akisema hakua na mtu mwingine kipindi icho wanakutana, na ana uhakika kuwa ujauzito ni wa brother.

Mwanzoni brother inaonekana alikua anampa msaada wa kujikimu dada huyo ila baada ya tafaruku kubwa linaloendelea home kasitisha saport ,kwani mkewe amedai yuko tayari kuachika kama kaka etu ataendelea kuwasiliana na huyo dada na kumsaidia. Fujo na kelele kila siku home aziishi na kuitwa familia kutatua mgogoro.

Dada huyo aliyepewa ujauzito alikua amepanga na anafanya shughuri zake ndogo ndogo . Ila ujauzito umekua ukimsumbua ,kutapika kama kote na kila week hospitali, hali iliopelekea kushindwa kujihudumia na amerudi kwa wazazi wake.

Mama wa huyo dada kaleta mashitaka home akitaka kaka yetu aendelee kumsapot huyo dada hadi atakapojifungu ili watatue mgogoro kwa kipimo cha DNA.

Wife wa brother kusikia pendekezo hilo kagoma katu katu kuwa ana uhakika mmewe anabambikiwa mimba na kuwa dada huyo anataka mtu wa kumlelea ujauzito. Kifupi ahamini mmewe kamtungisha mimba dada huyo.

Juzi tu wamerudi hospitali na bado jibu ni lile lile kua kaka hana mbegu za kiume.

Sasa wakuu katika mkasa kama huu

Busara ni nini ?

Kuikana mimba hadi mtoto azaliwe huku unajua kuwa yule dada anateseka na familia yake imekomaa hawana uwezo wa kumtunza mtoto wao ?

Au kaka amsapoti mdada huyo hadi ujauzito ukamilike na kipimo cha DNA kifanyike.

Familia imekwama nini kifanyike kwani vikao haviishi home kila siku

Wakuu ushauri wenu ni upi kwenye kisa kama hiki?
 
Back
Top Bottom