Ushauri unahitajika: Ana mtaji wa laki tatu, afanyie biashara gani?

nyantuzu

Member
Oct 1, 2014
87
23
Habari wanajamvi,

Kuna dada mmoja yupo kijijini anadai kadunduliza wee kafanikiwa kupata kiasi cha laki tatu (300,000). Anataka kwenda Dar akatafute biashara afanye ila hadi sasa hajajua ni biashara gani (biashara halali), na huko Dar hana ndugu hivyo itabidi apange chumba kwenye hiyo hiyo hela alionayo.

Anasema kijijini maisha magumu hivyo anahofia kuila hiyo hela alonayo sasa anataka aizungushe kwenye biashara.

Anaomba ushauri aina ya biashara ya kufanya kulingana na hela alinayo, na ni wapi kwa Dar es Salaam vyumba vya kupanga vinapatikana kwa bei rahisi?

Nawasilisha kwa niaba.

Kwa pamoja tumshauri dada yetu!
 
Huo ni mtaji mkubwa kama isingekua kodi ya chumba inatoka hapo, hata hivyo anaweza fanya hivi;

Anavyotoka huko kijijini abebe godoro na vyombo vyake vichache vya kuanzia maisha mjini ili hiyo lk3 isitumike kununulia hivyo vitu.

Atafute chumba cha 30,000/= kwa mwezi, mara nyingi wanataka miez 6 @30,000, hivyo atalipa 180,000/=, akifanikiwa kupata chumba akawa na kwake kisaikolojia kashawini maisha.

Asubuhi sana aende Buguruni kununua matunda kama ndiz, machungwa, maembe bila kusahau mihogo vinginevyo huuzi, na kuyauza kwa kuyatembeza vijiweni, vituo vya taxi, bajaji, wanakojenga, wanakoosha magari, na sehemu nyingine zote zenye mikusanyiko ya watu, sijui gharama halisi lkn siamini kama unaweza kutumia zaidi ya elf hamsini kununulia bidhaa.

Au anunue Maziwa fresh asubuhi sana pale ubungo na kuyauza Kwa kutembeza kama Matunda hapo juu.

Najua lazima kuna gharama nyingine zitaibuka tu, lazma uzipotezee vinginevyo wafa wasila na kumbuka dunia haina mjomba alishakufa miaka mingi hata sikumbuki lini!

Gudbai
 
Atulie tu huko huko nakama hujawahi hata kufika dar bado kwakwe nichangamoto asije angukia mikononi mwa matapeli
 
Back
Top Bottom