Uchaguzi 2020 Ushauri: Tundu Lissu kubali adhabu ili kampeni zisivurugike

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
4,040
8,895
Ni kweli kuwa umeonewa kupewa adhabu. Hilo kila mtu analielewa. Hao wanaosimamia haki (Polisi na NEC) ni wateule wa mgombea mwenzio. Hapo tatizo lipo kwenye katiba yetu.

Umefanya kampeni na watanzania wote tumeshuhudia jinsi ulivyowakaba koo watawala. Sasa hivi wanatafuta kila mbinu ili wakumalize. Hiyo adhabu ya wiki moja haitaathiri chochote kwenye imani ya watanzania juu yako, ndio kwanza watazidi kukubali.

Ukifanya kampeni wiki hii utakuwa umewapa nafasi ya kukukamata na kukuongezea adhabu, KUWA SMART.

Pumzika wiki hii baada ya hapo uje upige msumari wa mwisho kwenye sanduku la maiti ya POMBE kwenye maisha yake ya kisiasa.

Magufuli atatangazwa ila umeshampa adabu kuwa watanzania sio wajinga. Umemvua nguo kanda ya ziwa hadi aibu yaani!.

Leo hii jiwe anapiga magoti?! Kiburi chote kimekwisha.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Ushauri wa hovyo kweli yaani ningekuwa Lissu kesho ningetoka na mahandamano makubwa na kundelea na kampeni mpaka kieleweke na ndio ungekuwa mwanzo wa mapinduzi katika nchi hii
Maandamano ayapate wapi bwana tusidanganyane hapa?
 
Ushauri wa hovyo kweli yaani ningekuwa Lissu kesho ningetoka na mahandamano makubwa na kundelea na kampeni mpaka kieleweke na ndio ungekuwa mwanzo wa mapinduzi katika nchi hii
Naunga mkono Bora iwe ivyo ili andolewe ijulikane moja basi
 
Ushauri wa hovyo kweli yaani ningekuwa Lissu kesho ningetoka na mahandamano makubwa na kundelea na kampeni mpaka kieleweke na ndio ungekuwa mwanzo wa mapinduzi katika nchi hii
Yale ya Dada enu Kule inst mlishauri maandamano yaliishia wapi?
 
Ushauri wa hovyo kweli yaani ningekuwa Lissu kesho ningetoka na mahandamano makubwa na kundelea na kampeni mpaka kieleweke na ndio ungekuwa mwanzo wa mapinduzi katika nchi hii
Toka na hayo maandamano polisi wakufanye kazi. watakuchapa wewe.
 
Ni kweli kuwa umeonewa kupewa adhabu. Hilo kila mtu analielewa. Hao wanaosimamia haki (Polisi na NEC) ni wateule wa mgombea mwenzio. Hapo tatizo lipo kwenye katiba yetu.

Umefanya kampeni na watanzania wote tumeshuhudia jinsi ulivyowakaba koo watawala. Sasa hivi wanatafuta kila mbinu ili wakumalize. Hiyo adhabu ya wiki moja haitaathiri chochote kwenye imani ya watanzania juu yako, ndio kwanza watazidi kukubali.

Ukifanya kampeni wiki hii utakuwa umewapa nafasi ya kukukamata na kukuongezea adhabu, KUWA SMART.

Pumzika wiki hii baada ya hapo uje upige msumari wa mwisho kwenye sanduku la maiti ya POMBE kwenye maisha yake ya kisiasa.

Magufuli atatangazwa ila umeshampa adabu kuwa watanzania sio wajinga. Umemvua nguo kanda ya ziwa hadi aibu yaani!.

Leo hii jiwe anapiga magoti?! Kiburi chote kimekwisha.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
Naanzia hapa kwanza, Tundu Lisu hajaonewa amepata kile alichostahili kukipata.
Pili, suala la kufanya kampeni kila mtu kafanya kampeni, ila uchambuzi wa kampeni ni kwamba Lissu wengi walioenda kwenye kampeni zake wameenda kumshangaa yeye kwa sababu ni msekule wa kisiasa.
Tatu, akifanya kampeni ndani ya siku ya adhabu yake atazidi kuvunja sheria na kanuni mbalimbali hivyo ataongezewa adhabu maana hakutakuwa na namna nyingine.
Na mwisho kabisa yani yeye Lisu hata apewe mwaka mzima kufanya kampeni hakuna atakachobadilisha kwa maana hana sera yeyote kazi yake ni kuomba michango na kutukana kwenye jukwaa.
Kaa utambue watanzania wote tayari wanamuelewa Magufuli na watampigia kura Magufuli ifikapo Oktoba.
 
Nimewahi kusema mara nyingi, shida ya hivi vyama ni mashabiki. Ndio nyie pia mlimwambia membe gombea uraisi tupo nyuma yako.
HAKUNA WA KUANDAMANA, na hili lissu analijua hivyo wala hawezi kushughulika nalo.
Kama kweli watu wamechishwa na kweli wana kiu cha maandamano wala wasingesubiri lissu awaambia, NEC walipotoa tu uamuzi basi watu wangeenda kujazana pale kushinikiza wabatilishe
Tatizo kubwa kuna watu wanafikiri wanaotakiwa kuandamana ni watu wengine, alafu wao wabaki na kazi ya kupost picha na video maamuzi

Back
Top Bottom