Ushauri: Tumekuwa wachumba kwa miaka mitatu lakini sijawahi kufika nyumbani kwake. Hii inaweza kuathiri chochote?

Sijaelewa, hiyo ni ndoa au uchumba?. Isitoshe huoni kama hujiamini? Nini kinakuogopesha mpaka ubembelezwe kwa miaka Yote hiyo. Unajitengenezea kudharauliwa jitahidi uondoe hilo doa kabla mambo hayajakuwa magumu.
 
Pajue kwake bila yeye kujua halafu fanya ziara ya kushtukiza kama alivyokuwa anafanya hayati, utapata kujua kama kuna tatizo. Vizuri ziara iwe ijumaa usiku au jumamosi.
Zingatia kama una presha au mshtuko wa moyo usifanye hiyo ziara.
 
Unawezaje kusema unampenda mtu na unakataa kwenda kumuona anapoishi ilhali kakualika juu!!

so kila mkitaka kutana hadi akufuate?
 
Naomba mnisadie hili jambo.

Nimedumu na mpenzi wangu kipenzi kwa muda wa miaka mitatu mpaka sasa.

Tuna ndoto kubwa ya kuja kuwa wanandoa muda si mrefu, lakini katika miaka mitatu mimi "male" sijawahi kufika nyumbani kwake.

Yeye mara kwa mara huja nyumbani kwangu kunitembelea, sasa amekuwa akinilalamikia mara kwa mara kwa nini siendi kwake? Kiufupi mimi huwa sina tabia ya kwenda kwa mwanamke ndio msimamo wangu nilio jiwekea.

Naomba mnipe ushauri vijana wenzangu kwa huu msimamo wangu unaweza kuathiri chochote kwenye mahusiano yetu? Ahsanten

Kuna shida sehemu hakika!
Mchumba miaka mitatu aiseee?
Kwanini utaki kwenda? Waogopa nini? Unajua ana mwanaume unaogopa kumuacha maana wampenda sana maana mmedumu muda mrefu hivyo waogopa kumfumania?

Lazima kuna kitu hakiko sawa ndio maana anataka umwambie unaenda siku gani ili afix mapema kabla hujafika kwake...

Binafai sioni kama unamfaa maana sio kama wewe ni msaada kwake kwa chochote....sasa akipatwa na shida utamaaidiaje?

Mchumba wako halafu hutaki ujue anaishije kwake?

Nahisi kuna kitu hapa ujaweka wazi na ndio kinakufanya hadi leo hujamuoa na hutaki kwenda kwake.....

Kuna hakiko sawa na utaki kusema!
 
Back
Top Bottom