Nimeishi naye miaka 7, kapata mwanamke mwingine kaniacha kwa kudai nina mikosi!

The tolerance 1

JF-Expert Member
Sep 10, 2022
404
512
Habari zenu wandugu.

Niende moja kwa moja kwenye mada, jamani jambo hili linaniumiza sana kila nikifikiria nashindwa kuamini. Mimi ni ke, nimeishi na mwanaume takribani miaka saba, tumeishi kama mke na mume na kila kitu kilikuwa kimeshafanyika kuanzia utambulisho wa pande zote na posa, ilibaki tu tarehe ya kufunga ndoa. Katika kipindi chote hicho tulifanikiwa kupata watoto wawili Mungu alitujalia.

Lakini pia tulifanikiwa kununua kiwanja na kuanza kujenga, na pia tulifanikiwa kununua kigari kidogo angalau cha kutembelea, japo hayo yote alikuwa akifanya mwenzangu halafu anakuja tu kunipa taarifa. Wakati tunaanza maisha hatukuwa na chochote, tulianza na kulala chini tena kwenye chumba cha giza takribani miezi mitatu ya mwanzoni, hata kula yenyewe ilikuwa ya tabu lakini tulivumiliana huku tukimuomba Mungu kuwa ipo siku atatjalia na sisi.

Nifupishe kidogo hadithi hii, kuna kipindi mwenzangu aliniambia anataka apange chumba kingine tofauti na nyumbani kwa kuwa alipokuwa anafanyia kazi ni mbali na nyumbani, hivyoo wakati mwingine anakosa wateja kwa kuchelewa. Tulikubaliana kuwa akapange tu kwasababu ni jambo la muda mfupi tu, hakuna shida.

Basi tulikubaliana akaenda kupanga lakini nikimuuliza mbona wakati wa kurudi haji na nguo nyumbani nifue, anasema anafua tu mwenyewe, wakati alikuwa anaimbia muda ni mchache na wateja ni wengi. Kwahiyo alisema anafua mwenyewe, alikuwa analala huko siku tatu au nne au week ndiyo anakuja nyumbani, anasalimia tu na kesho yake anaondoka tena, ila kwa kuwa nilimwamini sikuwa na tabu.

Basi ilipita takribani miezi sita fikiria sijui mume wangu analala wapi, kuna siku nakamwambia kwa upendo tu baba T naomba kwenda kupaona unapolala ili hata likitokea la kutokea nipate cha kusema kwa wazazi wako, maana wanajua nipo na wewe, na hawajui unalala sehemu nyingine tofauti na hapa nyumbani.

Heee,, ilikuwa ni ugomvi mkubwa! Yaani alikataa katukatu kunipeleka, nilikaa kimya kwa muda wa mwezi tena nikamuuliza, alikataa tena kunipeleka nikamwambia basi sitakuuliza tena. Siku ziliendelea kusogea nikawa sina amani na yeye tena. Ilifika wakati pia nikimkumbusha kuhusu kufunga ndoa anakuwa mkali sana, ndipo nikawa na wasiwasi kuna jambo linaendelea ambalo mimi silijui.

Nilikaa chini nikalia machozi nikamwambia Mungu kama kuna kitu kinaendelea aniambie. Baada kama ya wiki mbili hivi nilifanikiwa kuishika simu yake maana siku zote nilikuwa siishiki, ina 'password' na akimaliza kutumia anazima.

Aliniambia nimletee baada ya kusikia inaita, ikatokea bahati mbaya nikashika sehemu ya Whatsapp, lo! Ilikuwa ni huzuni, kumbe mwenzangu alikuwa ameshaoa mwanamke mwingine na wameshazaa mtoto mmoja tayari! Nilivyomuuliza aliniambia niamue kubaki tuwe wawili au niondoke, lakini yeye hawezi kumuacha yule mwanamke na kashamtambulisha kwao na mama yake pia anamjua.

Niliumia sana sana maana sikutegemea kwa miaka yote hiyo angenigeuka namna hiyo. Baada kama ya wiki mbili hivi aliondoka kabisa nyumbani na watoto na kwenda kuishi na yule mwanamke. Kilichonifanya nije huku ni kwamba ananiambia ameniacha kwa sababu nina mikosi, nimeishi naye lakini hakupata pesa.

Wakati tunaishu naye tulifanikiwa kununua kiwanja chenye thamani takribani 12m, duka na gari, na wakati tunakutana hatukua na chochote. Hizi pesa zote tulizipata tukiwa pamoja. Sasa napatwa na butwaa, hii inaweza kuwa kweli?

Wenzangu mliyopitia hali kama hii mlifanyaje? Ushauri wenu jamani katika hili, limeniumiza sana hili, lakini pia nimekuwa single mama bila kutarajia kwa mtu ambaye nilimuamini kupita kiasi na ndiyo mwanaume wa kwanza kwangu na sikuwahi hata mara moja kumsaliti, japo alikuwa ananiweka katika mazingira magumu sana.

Naombeni ushauri wenu maana naumizwa na mengi.

Asanteni.
 
Duuh pole Sana! Ila muda bado upo! Na unaonekana na mwanamke mpambanaji Sana!! Sasa kisheria wewe huyo Ni mume wako na sheria inakuruhusu kugawana Mali! Usiache kitu kizembe!

Narudia afe kipa afe beki mgawane mali
 
Ni changamoto kwelly kwelly.. kama mambo yamefikia huko .. na ww unaona huwez ishi bora utaratibu wa vtu kugawanywa.. tu
 
Hapo hakuna Msalia mtume, mpeleke mahakamani kudadadeki, mgawane kila.kitu.

Na kama ikishindikana, nenda KAMLOGE ***** zake.
Yaan hata ukiweza kumuekea dawa.ya kuharisha kwenye chakula mwekee kbsa.

Bora uende kivita tu. Sidhan kama atakua na sababu ya msingi ya kukuacha.
Amemwaga mboga, we mwaga ugali na uvunje jiko
 
20220117_111814.jpg
20220209_064105.jpg
 
Habari zenu wandugu.
Niende Moja kwa Moja kwenye mada,jamani jambo hili linaniumiza sana kila nikifikiria nashindwa kuamini,mimi ni ke nimeishi na mwanaume takribani miaka Saba,tumeishi kama mke na mume na kila kitu kilikuwa kimeshafanyika kuanzia utambulisho wa pande zote na posa ilibaki TU tarehe ya kufunga ndoa.Katika kipindi chote hicho tulifanikiwa kupata watoto 2 Mungu alitujalia.

Lkn pia tulifanikiwa kunukua kiwanja na kuanza kujenga,na pia tulifanikiwa kununua kigari kidogo angalau Cha kutembelea japo hayo yote alikuwa akifanya mwenzangu then anakuja TU kunipa taarifa.
Wakati tunaanza maisha hatukuwa na chochote tulianza na kulala chini tena kwenye chumba Cha Giza takribani miezi mitatu ya mwanzoni,hata kula yenyewe ilikuwa ya tabu lkn tulivumiliana huku tukimuomba Mungu kuwa ipo siku atatjalia na sisi.
Nifupishe kidogo hadithi hii,kuna kipindi mwenzangu aliniambia anataka apange chumba kingine tofauti na nyumbani kwa kuwa alipokuwa anafanyia kazi ni mbali na nyumbani hivyoo wakati mwingine anakosa wateja kwa kuchelewa,tulikubaliana kuwa akapange TU kwa sababu ni ishu ya mda mfupi TU hakuna shida.
Basi tulikubaliana akaenda kupanga lakini nikimuuliza mbona wakati wa kurudi haji na nguo nyumbani nifue anasema anafua TU mwenyewe,wakati alikuwa anaimbia muda ni mchache na wateja ni wengi.So alisema anafua mwenyewe.alikuwa analaoa huko siku tatu au nne au week ndo anakuja nyumbani anasalimia TU na kesho yake anaondoka tena.ila kwa kuwa nilimwamini sikuwa na tabu.
Basi ilipita takribani miezi SITA imagine sijui mume wangu analala wapi,kuna siku nakamwambia kwa upendo TU baba T naomba kwenda kupaona unapolala ili hata likitokea LA kutokea nipate Cha kusema kwa wazazi wako maana wanajua nipo na wewe,na hawajui unalala sehemu nyingine tofauti na hapa nyumbani,he ilikuwa ni ugomvi mkubwa yani alikataa katikatu kunipeleka,nilikaa kimya kwa muda wa mwezi tena nikamuuliza alikataa tena kunipeleka nikamwambia basi sitakuuliza tena.
Siku ziliendelea kusogea nikawa Sina amani na yy tena,ilifika wakati pia nikimkumbusha kuhusu kufunga ndoa anakuwa mkali sana ndipo nikawa na wasiwasi kuna jambo linaendelea ambalo mi sioijui.
Nilikaa chini nikalia machozi nikamwambia Mungu kama kuna kitu kinaendelea aniambie.Baada kama ya wiki mbili hivi nilifanikiwa kuishika simu yake maana siku zote nilikuwa siishiki Ina password na akimaliza kutumia anazima, aliniambia nimletee baada ya kusikia inaita,ikatokea bahati mbaya nikashika sehemu ya Whatsapp lo!! Ilikuwa ni huzuni kumbe mwenzangu alikuwa ameshaoa mwanamke mwingine na wameshazaa mtoto mmoja tayari.
Nilivyomuuliza aliniambia niamue kubaki tuwe wawili au niondoke,lkn eye hawezi kumuacha yule mwanamke na kashamtambulisha kwao na mama yake pia anamjua.Niliumia sana sana maana sikutegemea kwa miaka yote hiyo angenigeuka namna hiyo. Baada kama ya wiki mbili hivi aliondoka kabisa nyumbani na watoto na kwenda kuishi na yule mwanamke.
Kilichonifanya nija huku ni kwamba ananiambia ameniacha kwa sababu Nina mikosi nimeishi naye lkn hakipata pesa wakati tunaishu naye tulifanikiwa kununua kiwanja chenye thamani takribani 12m,duka na gari,na wakati tunakutana htukua na chochote,hizi pesa zote tulizipata tukiwa pamoja,Sasa napatwa na butwaa hii inaweza kuwa kweli? Wenzangu mliopitia Hali kama hii mlifanyaje? Ushauri wenu jamani katika hili limeniumiza sana hili,lkn pia nimekuwa single ma bila kutarajia kwa mtu ambaye nilimwamini kupita kiasi na ndio mwanaume wa kwanza kwangu na sikuwahi hata mara Moja kumcheat japo alikuwa ananiweka katika mazingira magumu sana.
Naombeni ushauri wenu maana naumizwa na mengi.
Asanteni
Nimesikitika.
Watu wengi kesi kama hizi ingekuwa upande wa mwanaume ndo analalamika wangesema kwani ulimkuta bikra!
Wengine husema kaor mwanamke bikra!
Kuna mwingine mpaka alishauri watu kutembelea mahafari ya shule za wasichana kidato Cha sita kutafuta bikra!

Sasa wewe ingawa ni story ya upande mmoja, umekuja na nadharia tofauti. Ni mwaminifu, alikukuta ukiwa bikra, ume hustle naye, hujawai kucheat lakini amekuacha!

Ngoja tusubiri wanamajumui tuone mawazo yao.

Pole sana.
Halafu sisi wengine mbona hatupati wanawake kama nyinyi? Au miti bado inaendelea kuota pasipo wajenzi hadi miaka hii
 
Kesi ngumu sana hii mkuu.
Wewe kwa sasa una mishe gani?
Na kwa nini umeruhusu huyo kichaa aondoke na watoto?
 
Dah sisi wanaume kuna mda tunazngua aisee,, kuna jamaa yangu alifanya huu upimbi ana mke na mtoto alafu kmya kmya kampangia chumba mwanamke mwngne alafu anamletea dharau mkwewe.

Yule mkewe alikua ananilalamikia sana,, shemeji nisaidie huyu mwenzio saiv ananifanyia mambo mabaya, akija nyumban ananitukana tu na ananitishia kuniacha.. jamaa nikiongea anakataa.

Nilimwambia yule shemej yangu dada amua unavoona kuhusu huyu pimbi nimeshindwa kumbadilisha.

Dem alifanya maamuzi magum akasepa alafu jamaa na yeye akaja kupata msala wa hela za watu na madeni kibao.. jamaa akaanza kumtafuta tena yule mwanamke lkn demu alikataa mpka leo kaolewa na mtu mwingne.. jamaa yangu karma nilikuambia ukajifanya mbishi
 
Back
Top Bottom