Ushauri: Tumekuwa wachumba kwa miaka mitatu lakini sijawahi kufika nyumbani kwake. Hii inaweza kuathiri chochote?

Naomba mnisadie hili jambo.

Nimedumu na mpenzi wangu kipenzi kwa muda wa miaka mitatu mpaka sasa.

Tuna ndoto kubwa ya kuja kuwa wanandoa muda si mrefu, lakini katika miaka mitatu mimi "male" sijawahi kufika nyumbani kwake.

Yeye mara kwa mara huja nyumbani kwangu kunitembelea, sasa amekuwa akinilalamikia mara kwa mara kwa nini siendi kwake? Kiufupi mimi huwa sina tabia ya kwenda kwa mwanamke ndio msimamo wangu nilio jiwekea.

Naomba mnipe ushauri vijana wenzangu kwa huu msimamo wangu unaweza kuathiri chochote kwenye mahusiano yetu? Ahsanten
Muda wote huo hujawahi shtuka sasa leo mpaka kuja kujiuliza na hatimaye ukashindwa kupata majibu ukaamua kutuuliza na sisi huku maana yake shida tayari ipo mahali.
 
Kama yeye anakukaribisha na unakataa, siyo mbaya sana.

Ila ujue kuna confidence unajipotezea.

Hujawahi kwenda kwake for 3 good years, hujui anaishi na nani, hujui anaishije ishije.

Jiulize swali moja, akipata tatizo hapo nyumbani kwake unadhani atakupigia wewe ukalitatue wakati anajua hutaenda?

Kuna baadhi ya vitu ambavyo huwa vinakuwa fixed na wanaume kwenye nyumba, hivyo ungekuwa umepafanya pale kama kwako ungeweza kuwa msaada kwa hayo.

Kwa wewe kutoenda, jua kuna mwanaume anayefanya hizo kazi.
Naunga mkono.
 
Back
Top Bottom