Iongeze kukusanya mapato yapi? Unataka wakusanye mpaka damu?.
Maana kila mwaka inavuka malengo ya ukusanyaji. Mfano kama mwaka huu malengo ni kukusanya elfu 20 wanavuka mpaka elfu 40.
Kila mwaka wanavuka malengo ndio ujue wananchi au mfanyabiashara hakwepi kodi,ila Vita yote uliyoizingumzia kati ya TRA na wafanyabiashara,kuna mambo mengi ambayo sina muda wa kuyaandika yote. Yanayombana mfanyabiashara.
Pia kuna swala la mazingira ya upangaji matokeo.
Swala la mashine. Kwanza ilitakiwa TRA wenyewe ndio wawe nazo hizo mashine wagawe bure kwa wafanyabiashara,ksbb wao ndio wenye uhitaji wa hizo mashine bila kumuonea mtu. Pia matengenezo yake iwe juu ya TRA.
Ukija kwenye swala la kutoa risit. Wewe ulieleta huu Uzi japo sijasoma wote lakini unaweza usiwe unaifahamu hata biashara ya kuuza nyanya tu. Ingia kwenye biashara kwa hapa Tanzania ndio utauona mziki wake. Ukitoa rist kwa

ujue unaenda kufunga biashara yako.. Huo ndio ukweli. Na semina zote tunazokaa na TRA wanaelezwa hili pia. Na ndio maana wananchi wengine hawadai risit kwa nguvu ksbb tunaishi nao wanajua madhira anayopitia mfanyabiashara wa Tanzania kwa upande wa kodi.
Kwa ujumla kodi za Tanzania nyingi ziko juu kuliko nchi zote zinazotuzunguka. Nafikiri hatuna wataalam wazuri kuhusiana na mambo ya kodi. Au ni makusudi ya maafisa.
Mfano mzuri wewe na rafikiako Mmalawi mmeagiza magari aina moja labda Toyota corolla kila mmoja la kwake. Kule mmenunua kwa kila mmoja milioni 4 labda. Gari zote mbili zikasafirishwa mpaka hapa bandarini Dar. Wa Malawi akalichukua gari lake akaenda kulipia upande wao wa Malawi milioni 2 kwa rate ya Tsh. Gari hilo hilo kwa hapa bongo unaweza kulipia kodi milioni 7,8 hadi 9. Kwa gari hilo hilo. Wakati yule Mmalawi kapitisha kwenye bandari yetu,sisi wenye bandari badala tunufaike nayo lakini matokeo yake ndio hivyo
Mfano mwingine kontena la vitenge kwa Zanzibar haizidi milioni 38 mpaka 40. Kenya hivyo hivyo. Zambia milioni 35. Kwa hapa bongo ni milioni mia 300. Wakati ni nchi za ukanda mmoja. Na sisi Watanzania ilipaswa tunufaike ksbb tuna bandari.
Mimi nafikiri uanze kuyazungumzia haya kwanza ili angalau tuwe sawa kwenye viwango vya kodi na nchi zingine.