Ushauri - TOYOTA RAV4

Korosho

Senior Member
Nov 30, 2007
132
29
Ndugu wana JF,

Kwa wale wote ambao wamewahi kumiliki au wanamiliki Toyota RAV4 hizi tafadhali naomba uzoefu wenu kuhusu unywaji wa mafuta, uhimili wa gari katika barabara zetu za bongo, upatikanaji wa spea, na gharama za matunzo kwa ujumla.

1. Toyota RAV4 (1995 -1999, 3S-FE 2.0L engine, 4WD)

2. Toyota RAV4 (2000 - 2003, 1ZZ-FE 1.8L engine, 2WD)

Natanguliza shukrani zangu.
 
rav 4 ni moja ya magari yaliyouzika sana hapa tz na africa kutoka kampuni ya toyota. yana spea nyingi ajabu. ni very smooth na hayana shobo ilimradi serice tu....... nunua mzeee. ninamiliki ya 1998 rav 4 junior
 
Shukrani Mkuu, lakini vipi kuhusu unywaji wa mafuta? Je ni gari ambayo mtu wa kipato cha kawaida anaweza kuimudu ?
 
Ni gari nzuri sana Na ni ngumu......ili mradi usiinyime mahitaji yake.....kama service....mafuta....nk
 
Shukrani Mkuu, lakini vipi kuhusu unywaji wa mafuta? Je ni gari ambayo mtu wa kipato cha kawaida anaweza kuimudu ?

Inakula mafuta vizuri kutegemea na matumizi yako......bora tu iwe katika hali nzuri.....si unajua gari ikiwa mbovu ndio inabugia mafuta........
 
Shukrani sana Preta. Twende kwenye specifics, inatumia lita ngapi kwa kilometa? Gari ndogo kwa mfano zenye injini 1.5L zinakwenda kilomita 10,11,12, nyingine mpaka 16,17 kwa lita. Hizi RAV4 zikoje ?

Samahani kwa maswali mengi, ni katika hali ya kutaka kujua...ili niweze kujipanga.
 
Nimenunua 2008, mpaka leo naifurahia kwa kila kitu spea, mafuta, imetulia yeah... ni gari hutakaa ujute kuimiliki go and take it!
 
RAV4 Nyingi ni cc1998 (2000) kuanzia km7 kwa isiyo na service(mbovu) mpaka km13 kwa lita
 
Nimenunua 2008, mpaka leo naifurahia kwa kila kitu spea, mafuta, imetulia yeah... ni gari hutakaa ujute kuimiliki go and take it!

Shukrani Elia. Matumizi ya mafuta kwa wiki yakoje ? Spea bei zake zikoje ? Na vipi kuhusu re-sale value kama ukitaka kuiuza? Maana unaweza kuwa na gari halafu inakuwa kimeo kuiuza.
 
Ndugu wana JF,

Kwa wale wote ambao wamewahi kumiliki au wanamiliki Toyota RAV4 hizi tafadhali naomba uzoefu wenu kuhusu unywaji wa mafuta, uhimili wa gari katika barabara zetu za bongo, upatikanaji wa spea, na gharama za matunzo kwa ujumla.

1. Toyota RAV4 (1995 -1999, 3S-FE 2.0L engine, 4WD)

2. Toyota RAV4 (2000 - 2003, 1ZZ-FE 1.8L engine, 2WD)

Natanguliza shukrani zangu.

Nina experience na Rav 4 1ZZ vvTi 1.8L 2002, full kiyoyozi inaenda 11km per litre (nimetumia kwa mwaka na nusu, I know what am saying)! Full Tank nafika Moshi Marangu nikienda mdogo mdogo 100 - 130km/hr!
 
Shukrani sana Mkuu. Barabara zetu za vumbi na matope wakati wa masika inapiga vizuri ? Spea pati zake vipi zinapatikana na bei ikoje ?
 
Mkuu Riwa kuna tofauti kubwa sana kati ya matumizi ya mjini (folen na mengine) na kusafiri masafa....
Mimi nilikua na escudo, matumizi ndani ya jiji la dar ilikua km 7 hadi 8 kwa lita, ila siku nilipoenda nayo moshi, fuel consumption ilipanda hadi km 12 kwa lita!
Sasa hiyo 11km/l ni matumizi yapi hasa.....nadhani interest kubwa ya Korosho itakua kwa mjini (worst scenario).

Nina experience na Rav 4 1ZZ vvTi 1.8L 2002, full kiyoyozi inaenda 11km per litre (nimetumia kwa mwaka na nusu, I know what am saying)! Full Tank nafika Moshi Marangu nikienda mdogo mdogo 100 - 130km/hr!
 
Last edited by a moderator:
Shukrani Elia. Matumizi ya mafuta kwa wiki yakoje ? Spea bei zake zikoje ? Na vipi kuhusu re-sale value kama ukitaka kuiuza? Maana unaweza kuwa na gari halafu inakuwa kimeo kuiuza.

Mkuu......Rav4 haijawahi kuchuja....inauzika wakati wote.....kuhusu spare jaribu kufunga spare genuine.......utasahau ...... Zinapatikana kila mahali...binafsi kukushauri......go for it....
 
Ndugu wana JF,

Kwa wale wote ambao wamewahi kumiliki au wanamiliki Toyota RAV4 hizi tafadhali naomba uzoefu wenu kuhusu unywaji wa mafuta, uhimili wa gari katika barabara zetu za bongo, upatikanaji wa spea, na gharama za matunzo kwa ujumla.

1. Toyota RAV4 (1995 -1999, 3S-FE 2.0L engine, 4WD)

2. Toyota RAV4 (2000 - 2003, 1ZZ-FE 1.8L engine, 2WD)

Natanguliza shukrani zangu.

Mkuu hizo zote ni gari nzuri kwa maeneo tofauti

1995-1999 hii ni nzuri zaidi,unaweza itumia barabara nzuri na mbaya kwa uangalifu na zisikusumbue kabisa,hizi zote ni majembe kweli kweli ,kanisani inaenda kwenye harusi inaenda ,kazini ndio kwake,jumamosi shamba inaenda ,inabeba gunia tano za pumba,inaenda Moshi bila shaka,na mafuta kawaida ni cc1998.

2000-2003 huko garage zinaitwa Kili Time hizo ni lami kwa lami tuu ukizipeleka rafu road utaishi garage kila siku,ni gari nzuri sana very executive ila hazitaki shida mzigo wa wastani na barabara nzuri,Mbaya zaidi kuhusu hizi gari HAZIUZIKI,ukinunua ni yako mpaka ife,labda umpate mtu wa karibu umshawishi.
 
Mkuu......Rav4 haijawahi kuchuja....inauzika wakati wote.....kuhusu spare jaribu kufunga spare genuine.......utasahau ...... Zinapatikana kila mahali...binafsi kukushauri......go for it....

1995-1999 utauza tuu wako watu wanatoka mkoani wanazisaka sana za mikononi hawana hela za kutosha kwenda showroom

Ila 2000-2005 ukinunua ni yako mpaka ife labda uiuze kwa bei ya kutupa kila mtu anaogopa Kili Time
 
Mkuu Riwa kuna tofauti kubwa sana kati ya matumizi ya mjini (folen na mengine) na kusafiri masafa....
Mimi nilikua na escudo, matumizi ndani ya jiji la dar ilikua km 7 hadi 8 kwa lita, ila siku nilipoenda nayo moshi, fuel consumption ilipanda hadi km 12 kwa lita!
Sasa hiyo 11km/l ni matumizi yapi hasa.....nadhani interest kubwa ya Kongosho itakua kwa mjini (worst scenario).

Point of interuption huyu ni Korosho na si Kongosho umesomeka kiongozi.
 
Last edited by a moderator:
Shukrani Mkuu, lakini vipi kuhusu unywaji wa mafuta? Je ni gari ambayo mtu wa kipato cha kawaida anaweza kuimudu ?
Engine ya 3S ya kwenye hiyo gari ndio iko kwenye Noah za 1996-1999, ni engine nzuri sana. Haili sana mafuta. Kwa mwendo wa 60-80 kph inakwenda hadi kilometa 9-10 kwa lita. Ila kwa kuwa hiyo ya kwako ni full time 4WD, nadhani itakuwa chini ya hapo. Kuhusu vipuri, viko vingi sana. Uzuri wa Toyota ni kwamba gari nyingi zinatumia vipuri vinavyofanana, hasa vya engine. Nunua tu.
 
Back
Top Bottom